Ipo hivi, kwa nchi kubwa na yenye nguvu kiuchumi kama Marekani kupandisha riba kuna impact kubwa sana ya mda mrefu na mda mfupi.
Ki nadharia kutokana na kwamba tupo ulimwengu wa utandawazi ambapo mtaji unaweza kutoka nchi moja kwenda nyingine ina maanisha kwamba kwa riba kutoka 0.25% na kupanda mpaka 0.5% kunapelekea riba katika saving na borrowing kupanda. Nikiwa na maana kwamba hata kwenye zile yields za dhamana za madeni bonds and bills nazo zitapanda.
Kupanda kwa yields na saving rate kwenye taasisi za fadha za Marekani kutapelekea Capital inflow nyingi kwenye nchi ya Marekani kwa sababu sasa wawekezaji watakuwa na uhakika wa kupata returns kubwa kwenye uwekezaji wao kwa sababu riba imependa. Sasa nchi inavokuwa inapokea mitaji kutoka nje (capital inflow) ina maana kwamba ili mitaji hiyo iweze kuingia ina maana mahitaji ya sarafu ya nchi husika yatakuwa ni makubwa na kupelekea bei yako kupanda. Na ndio maana dakika chache baada ya tangazo la kupanda kwa riba sarafu za Euro, Yen na Pound zimeporomoka kwa kasi ndani ya mda mfupi ikiwa na maana sarafu ya dollar ilikuwa inanunuliwa kwa kasi sana.
Na kwa nchi kama Tanzania sidhani kama tunaweza kuepuka hii nguvu dola iliyopata kwa usiku huu. Ni suala la kuanza kuhabarishana kuanzia kesho kwamba dola itakuwa inanunuliwa kwa shilingi ngapi. Maana hata na hivo bado viashiria vya ndani ya nchi yetu bado ni dhaifu hivo natarajia kuporomoka kwa shilingi pia kwa siku za usoni kuanzia kesho.
Kitu kingine ikumbukwe pia nchi zinazochipukia ki uchumi zina madeni ya taasisi kubwa za kifedha na kitendo cha kupanda kwa riba kinamaanisha ule mzigo wa madeni ya riba lazima utakuwa juu na pia uwezekano wa kupatikana mikopo mipya kwa nchi nyingi masikini utakuwa ni mdogo kwa hiyo kwa namna moja au nyingine tunaweza kutegemea slow down ya chumi nyingi ambazo zinachipukia na zilikuwa zinategemea wahisani.
Suala lingine ni kuwa wakati interest inapopanda ina maana decisions za individual zinaelekezwa sana kwenye ku save na kununua asset ambazo kwa wakati huu zitakuwa na return kubwa kama bonds na bills. Kwa ku save zaidi ina maana households wa nchi nyingi za magharibi ambao huwa tunawategemea kuja huku ku spend huenda wakapunguza matumizi ambayo yalikuwa ni kama luxury mfano utalii kwenye nchi zetu kama Tanzania. Hivo ki nadharia ni kwamba uamuzi huu kidogo unaweza kuumiza sector ya utalii kwa nchi nyingi zinazochipukia kama Tanzania. Na ikumbukwe pia kudorora kwa utalii nayo ni sababu ya shilingi yetu ya Tanzania kuzidi kunywea dhidi ya dola.
Kwa sasa ni hayo tu ila tutazidi kufahamishana kadri mda utavozidi kwenda maana ndo kwanza tukio limetokea mda mchache uliopita.