Banki tano zote zimeniambia sikopesheki japo nina asset kama dhamana

Kajole

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2011
Posts
1,668
Reaction score
1,643
Leo nlipita ktk bank 5 tofauti kuulizia taarifa za mikopo kwa wajasiliamali:niliwatembelea CRDB,NMB,TPB.Barclays na MUCOBA, kifuatacho ndicho nilichokipata:

1. CRDB,NMB,TPB na MUCOBA

Hawa jamaa wanakopesha wafanyakazi wa serikali au mfanyabiashara mwenye biashara tayari inamaana kwa sisi tunaohitaji mtaji kwaajili ya kuanza biashara hatuna nafasi regardless una asset gani ya dhamana..

Mfano mimi nina kiwanja kimepimwa pia kinajengwa lakini wamesema sina nafasi kwakuwa sina biashara inayorun.

2. Barclays wao ndo hawana mpango kabisa wa kukopesha mjasiliamali.
Kiukwel nimehuzunika sana kwa ubaguzi huu nina asset to be used as security bado nafanya kilimo lakin sikopesheki?, dah tufanyaje sisi??
 
Last week me yalinikuta ayo sina ham nao tena mtu anakujibu bila ya aibu ukijitambulisha to kua ww ni mjasilia mali ushapoteza sifa sijui kwa nn?
 
Kweli taasisi za kifedha hazina urafiki kabisaaa na wajasimali kikubwa anza na mtaji wako huo huo mdogo wa Kilimo ipo siku itakuwa kubwa stay focus and keep on moving
 
HAKUNA BENKI YEYOYE inayotoa mkopo kwa startup business. Labda kama Wana special program for start up. Bank huwa zinatoa existing business kwasababu ukianza biashara na kufanya kwa miezi kadhaa au mwaka etc ni rahisi kujua hali ya biashara na sales na wao rahisi kuona mkopo unaweza lipika etc. Nakushauri Anza Kidogo kidogo au tafuta kwa ndugu. Ukisha fanya vizuri ndio uende bank watakupa
 
Wako sahihi wao hawakopeshi kwa kuangalia dhamana yako wanaangalia biashara yako ambayo ndo itakuwa inaludisha ule mkopo wakikupa kwa dhamana ukishindwa kulipa utakuwa umeludi nyuma kimaendeleo!!
 
Kiwango chako cha elimu tafadhali????
 
Wako sahihi wao hawakopeshi kwa kuangalia dhamana yako wanaangalia biashara yako ambayo ndo itakuwa inaludisha ule mkopo wakikupa kwa dhamana ukishindwa kulipa utakuwa umeludi nyuma kimaendeleo!!


Siku zote ngonjera vijana wajiajiri na ufukunyuku wooote unaoelezwa na viongozi wa serikali huwa wanaongea kumfurahisha nani? Nisaidieni kuwaambie wale wanaopanda majukwaani kuwaambia vijana waliotoka vyuoni wajiajiri kuwa wanapaswa kupimwa akili
 

Haujamwelewa!

Bank zimeanzishwa kwa malengo tofauti. Kwa Tanzania bank nyingi ni za biashara na huo ndiyo mwelekeo wa kile alichoandika. Mambo ya serikali kuongelea wananchi kujiajiri siyo mlengo wa bank lakini wakishajiajiri bank na kufanya vizuri bank inawapa fursa kukua zaidi. Lakini ni bank chache sana zinazoshughulika na watu wanaoanza biashara na kama hata zilizopo masharti yake ni makubwa na yana mlengo wa watu wenye project kubwa na siyo wajasiriamali. Fursa za mitaji kwa wajasiriamali hutolewa na serikali (ambayo imeshindwa kwa kiasi kikubwa) au mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO's)
 
Kuna vitu vingi bank znaangalia ilizikukopeshe siokwenda na kiwajatu,,,ni vizuri ukajikongoja uanzishe biashara then utaweza kukopesheka,,,au kma una idea nzuri tafta venture capital fund.....
 
Kuna vitu vingi bank znaangalia ilizikukopeshe siokwenda na kiwajatu,,,ni vizuri ukajikongoja uanzishe biashara then utaweza kukopesheka,,,au kma una idea nzuri tafta venture capital fund.....
bora mnaoshaur kitaalam lkn kuna wengne wanakurupuka
 
Umenikumbisha Economics niliyosoma katike level ya Certificate. Hii imenikaa sana kwamba ili uanzishe biashara yako lazina kwanza uajiriwe upate kipato.

Income (I) = Consumption (C) + Savings (S)
Savings (S) = Investment.

Wakopeshaji huangalia uwezo wako wa kurejesha mkopo kutokana na biashara unayoombea pesa ni wazo la biashara na dhamana uliyo nayo. Suala la dhamana huja baada ya kujiridhisha una shughuli ya kiuchumi itakayokuwezesha kurejesha mkopo.
 
Benki kukopesha, haitizami dhamana peke yake na si cha muhimu saana, kibenki haswa unaweza kopeshwa hata bila dhamani. Kitu muhimu ni waridhike kuwa mradi unaokopea pesa utalipa mkopo na kukupa faida.

Tunajua kwa Tanzania kuna benki zinatanguliza dhamana, ijapokua ikijua haitakiwi kumpa mteja mkopo wa kufanya mradi, ikijua wazi mteja hautofanikiwa. Kwahiyo wao hawakutizama kiwanja chako, ila pesa unataka za nini? na utarejeshaje huo mkopo na inaonekana hawakuridhika una manufaa na wewe wakakutalia.
 
dhamana haitoi marejesho hua inatumika kama ukishindwa lipa sasa kwa benk wao wanaangalia sana ni nini kitakachokuwezesha wewe kulipa rejesho ni vigumu sana kukopesha wazo lako la biashara ni ngumu kujihakikishia linaweza lipa huo mkopo.
2.wanaogopa sana kwa sasa kwa mtu ambaye ni mjasiliamali kwa kua biashara kwa sasa hazina faida na mzunguko wake ni mdogo sana wengi wanashindwa na kuleta usumbufu mkubwa sana kwa benk
3. watashindw kukukadilia ni kiasi gani cha rejesho kwa mwezi kwa kuwa pato la biashara yako kwa mwezi halijulikani na benk.
4.Hizo dhamana za nyumba ni usumbufu sana wengi sio wa kweli mkisha kopa mnashindwa kulipa nyumba ikitaka kuuzwa mnakimbilia mahakamani na kudai ni matrimonial na hakuna asent ya spouse
5. ni bora kumkopesha mwajiliwa wa serikali au kampuni kubwa mwenye mwenye dhamana ya ajira na dhamana ya pension kwa vyovyote mkopo unalipika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…