Mkuu kwanza nikupongeza kwa kuchukua step kubwa kwenda benk kuomba mkopo kwani ni wachache sana wenye huo ujasiri.
Pili usikasirike kwa kutopewa mkopo in your first attempt kwani umejifunza kitu kikubwa kuliko unavyodhani, wengi tumepitia njia hiyo wala usikate tamaa.
Unapokopa Bank, dhamana sio kitu pekee kinachokupa uhalali wa kupata mkopo, Bank wanaangalia historia ya biashara na mzunguko wa fedha katika biashara yako(Cash flow) na jinsi gani mzunguko huo utawathibitishia uwezo wako wa kurejesha mkopo.
Mfano mfanyakazi anapewa mkopo kirahisi kwa sababu bank inauhakika kila mwisho wa mwezi mfanyakazi ana mshahara hivyo ana uhakika wa kurejesha mkopo kila mwezi kwa mudo wote wa mkopo ukiachilia mbali risky za kifo ambazo zipo covered na insurance.
Mfano mwingine ni Mfanyabiasha aliye na Biashara tayari anakopesheka kirahisi kwasababu bank inaangalia historia ya biashara yake na mzunguko wa fedha kwenye hio biashara kwa muda fulani na kujiridhisha uwezo wa biashara hio kurejesha huo mkopo on monthly basis.
Bank hunapata wakati mgumu kukopesha biashara mpya kwasababu hawana historia ya hio biashara,hawana taarifa ya mzunguko wa fedha wa hio biashara na hawana ukakika kama hio biashara itaweza kusimama na hata ikisimama hawana uhakika kama itaendelea kusimama kwa muda wote mpaka mkopo wote urejeshwe.
Ushauri tu Kama biashara ni kilimo itabidi utafute njia nyingine ya kupata mtaji na ufanye kilimo chako kisasa huku ukirekodi vizuri mlolongo mzima wa biashara yako. Ikiwa na histotia nzuri ya uhakika especially ukiwa na potential buyers wa uhakika wa mazao yako unaweza rudi tena benki this time well prepared with all financial statements with you.
All the Best Mkuu katika kujifunza na Kuelekea mafaniko.
kwanza asante sana kwa maelezo mazur yenye kujenga yaan ni bonge la elim...pia nasisitiza posts za hapo juu ni za kijinga sana ni za kupiga ramli tu hazina lolote wanabwabwaja tu hawajui lolote mbona wameshindwa kuelimisha kama ulivyofanya sasa?,ni majuha tu maana wanasema vitu wasivyovijua mara pengine ana nyumba nan kamwambia nina nyumba?,mara hana business plan amejuaje kama sio ramli hyo?Mkuu, ujinga ni kudhani kuwa ukileta hoja ya kulalama humu wadau wote watakuonea huruma. Kwenye kutafuta elimu kuna kuchapwa viboko, matusi, kukatishwa tamaa na adhabu nyingine nyingi kutegemeana na medium of delivery na level yake. Unachokitafuta hapa wewe ni elimu kwa maana kwamba wewe ni mjinga katk masuala ya mikopo ya kibiashara, hujui vigezo vya kukufanya ukopesheke na taasisi za fedha. Hivyo, jitahidi kuwa na kifua cha kupokea changamoto na kuzitafsiri kwa mtazamo chanya utapata mengi ya kujifunza.
Hujui kama mabenki wanatumia utabiri kuamua kukukopesha au la..? Kama una business plan lazima utakuwa ume-include financial projections za biashara yako. Je, hizo projections sio utabiri wa namna gani biashara yako ita-perform kwa miaka 3 au zaidi ijayo..? Usiwe mwepesi wa kukata tamaa na kudhani umebaguliwa. Simama kwenye nafasi ya benki halafu mtu anakuja kwako humjui lakini anataka umkopeshe baada ya kusikia unatoa huduma hiyo. Wewe utamkopesha mara moja..? Nadhani hapana, lazima utajiridhisha katk yafuatayo:
Pia, tunatakiwa kujua kwamba pesa ya benki ni ya wateja wa fixed deposits na wanahisa, hivyo, BoT wanatoa guidelines kwa mabenki yote kulinda pesa za wateja na kuepuka kulipa fidia ikitokea benki imefilisika. Na hapo ndo urasimu unapoanzia au tuseme umakini katk utoaji mikopo. Mfanyabiashara siku zote ni mtu anayejishusha na ndiyo maana wasomi wengi kwa kujikweza hawawezi kufanya biashara. Ukikubali kujishusha utasaidiwa..!
- Utambulisho kwa vielelezo unavyovitaka (kwa benki ni; eneo la biashara, TIN na leseni ya biashara)
- Anataka mkopo kiasi gani na kwa ajili ya nini (kwa benki ni; business plan na sera ya benki kwa aina ya biashara inayoombewa mkopo i.e. si benki zote zinatoa mikopo kwa biashara ya kilimo)
- Historia na uwezo wa kurejesha mkopo katk muda mtakaokubaliana (kwa benki ni; financial records za biashara yako kwa kipindi flani i.e. hawakopeshi biashara inayoanza ili kupunguza risk kwa kufanyia kazi facts badala ya projections peke yake)
- Ikiwa atashindwa kurejesha katk mazingira ya kawaida kuna njia gani ya kurejesha pesa yako (kwa benki ni; dhamana au bima).
Eng. WFM
Nao wanafanya biashara..hawawezi kukupa tu mkopo kienyeji tu!! Lazima wajiridhishe ni namna gani utaweza kurejesha, mikopo siyo sadaka!!Inasikitisha sana....Bank hawataki kusikia kitu inaitwa entrepreneur[emoji24] [emoji24] [emoji24]