Banyamrenge, walowezi wa kitutsi nchini Congo DR ambao wanadai ardhi ili waanzishe taifa lao

Kutoka kwenye bandiko lako,Kikundi cha kwanza cha Banyamulenge kilihamia mwaka 1850,kikundi cha pili mwaka 1880.
Kama ni hivi kwanini unawaita walowezi?Mwaka 1850 na 1880 kulikuwa na Congo?
Kwa mujibu wa historia rasmi Congo ilianza 1885 baada ya mkutano wa Berlin,manake ni kuwa wao hawakuhamia Congo kwasababu haikuwepo ila walihamia sehemu ambayo baadae ilikuja kujulikana kama Congo manake Congo imewakuta wao wakiwa kwenye hiyo ardhi.

Kikundi cha nne ni watutsi jamii ya Wanyakarama wao ardhi yao ilikuwa Burundi na cha tano ni Wahema wao ardhi yao ilikuwa Uganda ila mipaka mipya 1899 ikahamishia hizo ardhi kuwa sehemu ya Congo tena bila shaka pasipo wao kushirikishwa, sasa ni vipi hawa watu wanaitwa walowezi? Kwa maoni yangu ni indigenious.
 
Hao Banyamurenge ndio waliomsaidia Kabila kumwondoa Mobutu , na walifanya hivyo ili kuhakikishiwa usalama wao na uraia wao maana Mobutu aliwatesa sana, Kabila baada ya kusaidiwa akawageuka na kuanza kuwaua, wapo Congo more than 100 years kabla ya uhuru leo unawaondolea haki zote na kuwaita walowezi, wafrica wapuuzi sana na ukabila wao, Nyerere alikuwa na akili sana alitangaza siku ya uhuru yeyote ambaye atakuwepo kwenye ardhi ya Tanzania siku ya uhuru atakuwa raia huru na kamili wa Tanzania, ilisaidia sana kuondoa ukabila na matatizo ya uraia kwa wananchi
 
Tanz
Tanzania ikitenga watu wa kigoma na Ngara wakawaita waRundi na kuwaua eti warundi kwao basi na wao watadai kutudi na maeneo yao.
 
Wakola!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…