Banyamulenge ni wahanga wa Kagame

Banyamulenge ni wahanga wa Kagame

jMali

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2010
Posts
8,404
Reaction score
4,973
Kwa wasiojua, Banyamulenge ni watu wenye asili ya kitutsi wanaopatikana DRC kabla hata ya mipaka ya wazungu, kama ambavyo Wamasai wako Kenya na Tanzania. Tunaongelea zaidi ya miaka 200. Kagame anavyofanya fujo Africa Mashariki watu wote wenye asili ya Rwanda/Burundi wanajikuta wahanga. Hata hapa Tanzania kuna Watanzania wa makabila hayo ambayo wapo kabla hata ya Uhuru lakini ilipotokea chokochoko wakati ule na wao wakaonekana kama mamluki, wakati hata hawajui asili yao nyingine yoyote isipokuwa Tanzania. Yaani fikiria kama sisi tungekuwa Kenya ambayo tumepakana na Somalia, halafu kuna vita, hivi unadhani hapo kwenye vijiji vya mipakani ambapo wasomali wameua, wamebaka, wamejeruhi etc wenyeji watajali kama watu kama Aden Rage na Hussein Bashe ni wahapahapa?

In fact hata hili jina la Banyamulenge hawa wacongo walijipa wenyewe ili watofautishwe na watutsi wa Rwanda na Burundi. Hii ni kutokana na fujo za watutsi wa Rwanda na Burundi ikiwemo Genocide ambayo Watutsi walifanya dhidi ya Wahutu huko Burundi miaka ya 70. Sasa Wahutu wakija ukimbizini Congo halafu wakute tena sampuli za watu wale wale waliowakimbia ingeweza kuleta shida. Hivyo Banyamulenge walijipa hili jina ili kutuliza mizuka ya hata wenyeji ambao nao walishaanza kuwa na wasiwasi dhidi yao. Vile vile wengi hawajui kuwa Banyamulenge hawapatani na Wanyarwanda wa Kagame kwa kuwa wao huona DRC ni nyumbani.

Kagame hutumia mbinu hii ya kutumia watu wenye asili ya Kitutsi hapa East Africa ili kutanua influence yake. Kwa mfano hapo Uganda RPA wali-recruit waganda wenye asili ya kitutsi ambao hawakuwa na any connection to Rwanda isipokuwa lugha tu na wakamsaidia Museveni (another mu-Hima), halafu kuvamia Rwanda na kupindua serikali ya Habyarimana, halafu wakaingia congo DRC waka-recruit baadhi ya hawa Banyamulenge wakampindua Mobutu. Halafu from time to time anatumia uwepo wa hawahawa wenyeji wenye asili ya Rwanda kuingiza majeshi yake na kujifanya ni waasi wa jeshi la Congo. Matokeo yake lazima kutakuwa na visasi visivyo halali dhidi ya Watutsi wasio na hatia.

Vile vile Kagame huwa anahonga watu wenye asili ya Kitutsi kwa nafasi kubwa mbalimbali nchini mwake. Alitengeneza sera ya Wanyarwanda kurudi nyumbani freely, yaani unachohitaji ni kuunda unda historia tu kuwa babu yako alitokea Rwanda anakupa uraia fasta. Yaani kama vile Mngoni adai leo adai anarudi kwao South Africa! Lakini sera hii obviously ni kwa ajili ya Watutsi tu kwa kuwa wao hata muonekano wao huwa ni dhahiri. Kupitia sera hii watu wenye asili ya Kitutsi from all over the world, including baadhi ya Banyamulenge, ‘wamerudi’ Rwanda ‘kuendeleza nchi yao’. Sasa hii nayo imeleta shida kwani wenyeji hawawezi kuamini kuwa Banyamulenge ni wacongo wakati kuna washikaji wamezaliwa nao, wamesoma nao halafu ghafla wanapewa uwaziri huko Rwanda, ni mabosi wa makampuni ya Umma n.k halafu M23(Rwanda) wakivamia DRC, Banyamulenge wa DRC wadai kuwa wao sio Wanyarwanda.
Ukweli ni kuwa Banyamulenge walio wengi hawaungi mkono M23 kabisa, lakini ndio ngumu kuaminika kama ambavyo hata hapa nyumbani kuna watu wanaweza kuwa wabunge hata mawaziri lakini siku wakichukua fomu za Urais kila mtu atawacheka.

Lakini yeye hilo hajali kwani ndio hutumia matukio hayo kuhadaa ulimwengu kuwa sasa anakwenda kusimamisha Genocide kuokoa maisha ya Watutsi n.k. Na hili analifanya kwa kutumia media. Kwa bahati mbaya sana amekuwa expert wa media manipulation toka zamani. Anaanzisha mashambulizi halafu anasambaza matukio ya majibu ya uchokozi wake (sio kwamba naunga mkono), ili aungwe mkono. Matokeo yake historia ya Rwanda na Burundi, Watutsi na Wahutu imepinda kuelekea upande chanya kwa Watutsi kuliko uhalisia.

Sasa hivi kumeenea video mitandaoni zikionyesha Banyamulenge wakiwa wanafanyiwa ukatili huko DRC. Hakuna shaka kwangu mimi kuwa video hizo ni za kweli na hakuna chochote kinachoweza kuhalalisha ukatili tunaouona kwenye video hizo.

Lakini tusifike mahali tukasahau kufikiri kwa makini kama Great Thinkers namna ambavyo media inatumika kufifisha upande mmoja na kukuza mwingine mfano:

  • M23 wamepiga DRC mpaka kufikia kukalia baadhi ya miji lakini hakuna video hata moja ya mauaji yao dhidi ya wenyeji, tunasikia stori tu na malalamiko toka kwa serikali na wananchi wa Congo. Je Wacongo wakiwa wanapigwa simu huwa hazifanyi kazi au hawana bando?
  • Kwa nini hawa ‘wacongo’ wanachukua video za uhalifu wao dhidi ya Banyamulenge? Kwa ajili gani? Ukumbusho? What’s the purpose? Seems to me kama vile kuna nguvu kubwa inatumika kufanya mauaji haya mbele ya kamera ili zisambazwe mitandaoni!
  • Jamii zote duniani hazikosi wavuta bangi ambao wanaweza kutumika/kuchochewa. Sidhani Mcongo hata mwenye hasira kiasi gani anaweza kuua mtu hadharani kwa sababu tu ni Banyamulenge, halafu ajitoe mpaka sura yake kashika mapanga. Mauaji haya kwa maoni yangu yanaonekana kuratibiwa na far more intelligent entities zaidi ya hawa mapanya-road tunaowaona kwa malengo maalum.
  • Ukidhani kama naleta conspiracy theory kumbuka hili:
  • Mauaji ya Watutsi Rwanda mwaka 1994 yalifanywa na Interahamwe. Lakini hao Interahamwe kiongozi wao alikuwa Mtutsi (Robert Kajuga, unaweza kumgoogle), aliyejifanya kuwa yeye ni Mhutu. Tena alichukua ndugu zake akawatorosha kwenye usalama, halafu akaingia mtaani kuongoza Interahamwe nyumba hadi nyumba. Mauaji yakafanyika Kagame akapata huruma ya dunia kuwa anazuia Genocide!
  • Hili la kuwa Interahamwe waliongozwa na hata kufadhiliwa pesa na Watutsi huwa Media halikumbuki badala yake wanakumbuka watu waliochochewa na kutekeleza mauaji kuwa ni Wahutu.
Mauaji ya aina zote hayakubaliki lakini tufikiri kwa mapana zaidi we are Great Thinkers.
 
Daaah!, upo kiongozi? Ulipotea sana mkuu. Karibu sana jukwaani.
 
Hapo uliposema mtutsi kafadhili mauaji ya watutsi umenichanganya.
Interahamwe kilikuwa kikundi cha ndani ya chama tawala kama vile UVCCM huku bongo, baadhi ya wafadhili walikuwa Watutsi (kabla ya Genocide). Baada ya Genocide, Media inachoelezea ni kana kwamba Interahamwe ilianzishwa ili ichinje Watutsi tu.
 
Nipo sana tu majukumu mengi
Pamoja sana.

Kagame ni spin doctor grade ya juu sana, Baada ya Habyarimana kuuawa na Kagame kuchukua nchi, aliandika historia aliyotaka yeye, yenye propaganda na uwongo mwingi, akaiaminisha dunia.

Naona sasa washirika wake wa magharibi wanaanza kukaa kando, siku zake zinaelekea ukingoni.
 
Kagame Ndio spy Master wa Western country hapa east Africa bro. Hivyo vyote havitokei kwa bahat mbaya. Cku wazungu wakimchoka ndio utauona uovu wake watauweka hadharan. Wanamtumia kuiba hapo Congo. Kitu kimoja anakosea zaid ni kule kuendelea kuwaweka watusi mbele kwenye kila nafasi za kaz matokeo yake kuna chuki za chinichin za wahutu ni suala kumuomba Mungu tu aepushie mbali ila inawezekana ikaja kutokea genocide nyingine.
 
Kwa wasiojua, Banyamulenge ni watu wenye asili ya kitutsi wanaopatikana DRC kabla hata ya mipaka ya wazungu
Nimesoma hiki tu nikachukia post yako, unapigia chapuo Kagame na watutsi. Mi naamini watutsi si watu wazuri kwa wakongo@least
 
Daah bosss upo karibu sana kiongozi na ahsante kwa kitu kikali chenye shahidi mbalimbali uko deep kaka daah kumbe yote tuliaminishwa tofauti aisee lakini siku za slim zimekaribia CIA ndani ya Kigali kazi maalumu kumnyorosha acha mvua inyeshee
 
hapa kwetu mmoja kutoka Mkoa wa Magharibi mwa nchi kidogo tu ajichanganye alilia kama Mambuzi
 
Kwa wasiojua, Banyamulenge ni watu wenye asili ya kitutsi wanaopatikana DRC kabla hata ya mipaka ya wazungu, kama ambavyo Wamasai wako Kenya na Tanzania. Tunaongelea zaidi ya miaka 200. Kagame anavyofanya fujo Africa Mashariki watu wote wenye asili ya Rwanda/Burundi wanajikuta wahanga. Hata hapa Tanzania kuna Watanzania wa makabila hayo ambayo wapo kabla hata ya Uhuru lakini ilipotokea chokochoko wakati ule na wao wakaonekana kama mamluki, wakati hata hawajui asili yao nyingine yoyote isipokuwa Tanzania. Yaani fikiria kama sisi tungekuwa Kenya ambayo tumepakana na Somalia, halafu kuna vita, hivi unadhani hapo kwenye vijiji vya mipakani ambapo wasomali wameua, wamebaka, wamejeruhi etc wenyeji watajali kama watu kama Aden Rage na Hussein Bashe ni wahapahapa?

In fact hata hili jina la Banyamulenge hawa wacongo walijipa wenyewe ili watofautishwe na watutsi wa Rwanda na Burundi. Hii ni kutokana na fujo za watutsi wa Rwanda na Burundi ikiwemo Genocide ambayo Watutsi walifanya dhidi ya Wahutu huko Burundi miaka ya 70. Sasa Wahutu wakija ukimbizini Congo halafu wakute tena sampuli za watu wale wale waliowakimbia ingeweza kuleta shida. Hivyo Banyamulenge walijipa hili jina ili kutuliza mizuka ya hata wenyeji ambao nao walishaanza kuwa na wasiwasi dhidi yao. Vile vile wengi hawajui kuwa Banyamulenge hawapatani na Wanyarwanda wa Kagame kwa kuwa wao huona DRC ni nyumbani.

Kagame hutumia mbinu hii ya kutumia watu wenye asili ya Kitutsi hapa East Africa ili kutanua influence yake. Kwa mfano hapo Uganda RPA wali-recruit waganda wenye asili ya kitutsi ambao hawakuwa na any connection to Rwanda isipokuwa lugha tu na wakamsaidia Museveni (another mu-Hima), halafu kuvamia Rwanda na kupindua serikali ya Habyarimana, halafu wakaingia congo DRC waka-recruit baadhi ya hawa Banyamulenge wakampindua Mobutu. Halafu from time to time anatumia uwepo wa hawahawa wenyeji wenye asili ya Rwanda kuingiza majeshi yake na kujifanya ni waasi wa jeshi la Congo. Matokeo yake lazima kutakuwa na visasi visivyo halali dhidi ya Watutsi wasio na hatia.

Vile vile Kagame huwa anahonga watu wenye asili ya Kitutsi kwa nafasi kubwa mbalimbali nchini mwake. Alitengeneza sera ya Wanyarwanda kurudi nyumbani freely, yaani unachohitaji ni kuunda unda historia tu kuwa babu yako alitokea Rwanda anakupa uraia fasta. Yaani kama vile Mngoni adai leo adai anarudi kwao South Africa! Lakini sera hii obviously ni kwa ajili ya Watutsi tu kwa kuwa wao hata muonekano wao huwa ni dhahiri. Kupitia sera hii watu wenye asili ya Kitutsi from all over the world, including baadhi ya Banyamulenge, ‘wamerudi’ Rwanda ‘kuendeleza nchi yao’. Sasa hii nayo imeleta shida kwani wenyeji hawawezi kuamini kuwa Banyamulenge ni wacongo wakati kuna washikaji wamezaliwa nao, wamesoma nao halafu ghafla wanapewa uwaziri huko Rwanda, ni mabosi wa makampuni ya Umma n.k halafu M23(Rwanda) wakivamia DRC, Banyamulenge wa DRC wadai kuwa wao sio Wanyarwanda.
Ukweli ni kuwa Banyamulenge walio wengi hawaungi mkono M23 kabisa, lakini ndio ngumu kuaminika kama ambavyo hata hapa nyumbani kuna watu wanaweza kuwa wabunge hata mawaziri lakini siku wakichukua fomu za Urais kila mtu atawacheka.

Lakini yeye hilo hajali kwani ndio hutumia matukio hayo kuhadaa ulimwengu kuwa sasa anakwenda kusimamisha Genocide kuokoa maisha ya Watutsi n.k. Na hili analifanya kwa kutumia media. Kwa bahati mbaya sana amekuwa expert wa media manipulation toka zamani. Anaanzisha mashambulizi halafu anasambaza matukio ya majibu ya uchokozi wake (sio kwamba naunga mkono), ili aungwe mkono. Matokeo yake historia ya Rwanda na Burundi, Watutsi na Wahutu imepinda kuelekea upande chanya kwa Watutsi kuliko uhalisia.

Sasa hivi kumeenea video mitandaoni zikionyesha Banyamulenge wakiwa wanafanyiwa ukatili huko DRC. Hakuna shaka kwangu mimi kuwa video hizo ni za kweli na hakuna chochote kinachoweza kuhalalisha ukatili tunaouona kwenye video hizo.

Lakini tusifike mahali tukasahau kufikiri kwa makini kama Great Thinkers namna ambavyo media inatumika kufifisha upande mmoja na kukuza mwingine mfano:

  • M23 wamepiga DRC mpaka kufikia kukalia baadhi ya miji lakini hakuna video hata moja ya mauaji yao dhidi ya wenyeji, tunasikia stori tu na malalamiko toka kwa serikali na wananchi wa Congo. Je Wacongo wakiwa wanapigwa simu huwa hazifanyi kazi au hawana bando?
  • Kwa nini hawa ‘wacongo’ wanachukua video za uhalifu wao dhidi ya Banyamulenge? Kwa ajili gani? Ukumbusho? What’s the purpose? Seems to me kama vile kuna nguvu kubwa inatumika kufanya mauaji haya mbele ya kamera ili zisambazwe mitandaoni!
  • Jamii zote duniani hazikosi wavuta bangi ambao wanaweza kutumika/kuchochewa. Sidhani Mcongo hata mwenye hasira kiasi gani anaweza kuua mtu hadharani kwa sababu tu ni Banyamulenge, halafu ajitoe mpaka sura yake kashika mapanga. Mauaji haya kwa maoni yangu yanaonekana kuratibiwa na far more intelligent entities zaidi ya hawa mapanya-road tunaowaona kwa malengo maalum.
  • Ukidhani kama naleta conspiracy theory kumbuka hili:
  • Mauaji ya Watutsi Rwanda mwaka 1994 yalifanywa na Interahamwe. Lakini hao Interahamwe kiongozi wao alikuwa Mtutsi (Robert Kajuga, unaweza kumgoogle), aliyejifanya kuwa yeye ni Mhutu. Tena alichukua ndugu zake akawatorosha kwenye usalama, halafu akaingia mtaani kuongoza Interahamwe nyumba hadi nyumba. Mauaji yakafanyika Kagame akapata huruma ya dunia kuwa anazuia Genocide!
  • Hili la kuwa Interahamwe waliongozwa na hata kufadhiliwa pesa na Watutsi huwa Media halikumbuki badala yake wanakumbuka watu waliochochewa na kutekeleza mauaji kuwa ni Wahutu.
Mauaji ya aina zote hayakubaliki lakini tufikiri kwa mapana zaidi we are Great Thinkers.
Mkuu kwa iyo Pasco Ntaganda na Lauret Nkunda ni Banyamulenge?
 
Hapo uliposema mtutsi kafadhili mauaji ya watutsi umenichanganya.
Madam Robert kajuga alikuwa ni mtutsi, Baba take alikuwa mtutsi pure.
Ila alitumia fake ID ili kumuonyesha kuwa yeye ni muhutu ndie alikuwa kiongozi wa interahamwe.
Kajuga-1.jpg
D4Dz-ywXoAASElA.jpg
Screenshot_20221229-183511_Chrome.jpg

Angalia tuu sehemu ya mwanzoni.
 
Kagame Ndio spy Master wa Western country hapa east Africa bro. Hivyo vyote havitokei kwa bahat mbaya. Cku wazungu wakimchoka ndio utauona uovu wake watauweka hadharan. Wanamtumia kuiba hapo Congo. Kitu kimoja anakosea zaid ni kule kuendelea kuwaweka watusi mbele kwenye kila nafasi za kaz matokeo yake kuna chuki za chinichin za wahutu ni suala kumuomba Mungu tu aepushie mbali ila inawezekana ikaja kutokea genocide nyingine.
Ninajua kuwa wazungu wanafumbia macho mauaji yake na udikteta kwa sababu wanashirikiana kuiba rasilimali za DRC, Ukisema kwamba ni spy wao inawezekana kabisa, dots zinakubali kuunganika.

Juzijuzi wameanza kumsanua kuhusiana na m23 yake, hapa kuna mawili. Inawezekana wanaanza kumchoka ama tunazugwa tu akina sisi ili tusielewe kwamba wako pamoja.
 
Uzi umeandikwa kwa utulivu.
Hapo kwenye fomu za urais nimekumbuka story ya Salim.
 
Back
Top Bottom