Banza anahitaji msaada: Asha

Banza anahitaji msaada: Asha

Junius

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Posts
3,181
Reaction score
144
na Khadija Kalili

MKURUGENZI wa Kampuni ya African Stars Entertainment (ASET), Asha Baraka, ametoa wito kwa wadau wa muziki nchini kumsaidia mwanamuziki mahiri, Ramadhani Masanja ‘Banza Stone’ aliyelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika Hospitali ya Mwananyamala jana, Asha alitoa wito kwa kila mdau kuguswa na matatizo yaliyomkuta msanii huyo, ambayo yangeweza kumkuta yeyote.

Asha aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Banza Stone kabla ya msanii huyo kujiunga na bendi ya Bambino Sound, alisema kwa sasa msanii huyo anahitaji msaada mkubwa katika kupigania uhai.

Alisema, mara kadhaa msanii huyo alipoumwa, ASET ndiyo iliyokuwa ikigharamia matibabu yake katika Hospitali ya Burhani ya jijini Dar es Salaam, hivyo anahitaji kusaidiwa.

Alisema, kwa mazingira na tabia ya Banza Stone, anastahili kupata usimamizi wa karibu katika ufuatiliaji wa tiba, kula na udhibiti wa utumiaji wa bangi, vitu ambavyo vinazidi kumuathiri.

Alisema, wakati akiwa chini yake, alikuwa akijitahidi kumdhibiti, lakini baada ya kuondoka, Banza Stone amekosa usimamizi wa karibu.

Aidha, mkurugenzi huyo alisema kwa matatizo ya msanii huyo, hastahili kulaumiwa kwa sababu wanaotakiwa kumsaidia kwa sasa ni Bambino Sound, si ASET.

“Viongozi wa Bambino Sound ndio wa kulaumiwa, kwani walimchukua kwa ahadi ya kumtibu nchini Ujerumani, lakini hadi sasa ndiyo hivyo,” alisema Asha.

Asha alisema, pamoja na hayo, kamwe hawezi kumtupa Banza Stone, kwani hata msanii huyo analijua hilo na ndiyo maana akiwa nje, aliwahi kumtumia tiketi ya ndege kurejea nchini.

“Kuna wakati nilikuwa namgharamia matibabu, lakini leo hii watu wanasema tumemtupa, hii siyo kweli, kwani hata Kapteni John Komba aliwahi kutaka kutoa msaada wa kumhamishia Hospitali ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Lugalo, lakini mgonjwa mwenyewe alikataa,” alisema.

Alisema baada ya Banza Stone kurejea nchini, alionekana kudhoofika, hivyo ASET wakampeleka Muhimbili kwa vipimo na kubainika anakabiliwa na ugonjwa wa kifua kikuu (TB), kwa kumjali, Asha alikuwa akienda kumchukulia dawa za ugonjwa huo katika hospitali ya kitengo hicho, iliyoko mkabala na Kituo Kikuu cha Polisi.

Msanii amaelazwa katika wodi namba tano ya hospitali ya Mw'nyamala.
 
Hiyo mibangi itawamaliza wasanii wetu......but Get well soon Banza!
 
Duh pole sana Banza..! Kuna link yeyote na yule mcheza shoo aliyekuwa hoi buguruni mwishoni mwa mwaka jana ambaye baada ya kuhojiwa na gezeti moja la udaku aliwahi kusema anashangaa wanamuziki wenzake wanamtupa lakini wajue wako njia moja kama yeye. Kama sikosei aliwataja banza, ali choki etc...nae pia alikuwa na TB (wimbo ulio bora, mengine hawayataji)
 
Bangi+Coke= Chali. Take care man, its not too late to the road of recovery. Ninakuombea.
 
bangi+coke= chali. Take care man, its not too late to the road of recovery. Ninakuombea.

true mkuu ma-ppoowwwder yanamharibu, lakini hiyo tb aliyo nayo haijaletwa na bangi, his immunity is low na banza anajua tatizo lake

wenzake wameanza dawa na sasa wanadunda, aanze art huyo atapona
 
ma-powder yanamuharibu,bangi inamzuru,immunity is low,sijui mwanamziki gani kasema wengi watamfuata.mbona hiki kiswahili mnatuchanganya what is what?
 
Pole sana Banza.

Kama ni TB..I guess anaweza kuwa na upungufu wa Kinga mwilini. Who knows?

Aende hospitali achukue vile vipimo vikubwa. Kama ana upungufu wa kinga, anaweza kuanza dawa mara moja. Akifuata masharti, he is sure to be around for the next twenty years. Inshallah.

Mi naamini imefika point, watanzania tukubaliane na hali halisi ya haya magonjwa. Tunavyozidi kuficha ficha ndo tunazidi kuweka stigma na waathirika wanaona vibaya kupima. LAKINI I believe kwa manpower ambayo taifa letu limeipoteza kwa huu ugonjwa ni vyema tupigane na silence hii. Sijui kwa nini mpaka leo tunaona upungufu wa Kinga kama gonjwa la aibu. Can we do something to adress this? Perhaps we can.

Pole Banza. Jitahidi upime vipimo vyote. Kama hujawa mwathirika naamini utapona na uanze kuchukua tahadhari. Kama umeshaathirka siyo mwisho wa maisha. There is another round. Muone na fuata ushauri wa daktari.

Kila lakheri na pole sana.
 
True Masanja. Haina hata maana ya kudanganya, maana unakuwa unajidanganya mwenyewe. Being hiv+ is not the end of your life. Watu wako fit zaidi ya wazima , sababu kila mara wako kwenye control, na mwili unafwatiliwa. Na sisi lazima tubadili tabia, unyanyasaji baada ya kujua xy ni hiv+. Watu wako tayari kufanya mapenzi bila vifanyio, lkn kushare glass na mtu ambaye ni hiv+ shida. lol!
 
Poor Banza!....for sure, Banza was my favorite musian in Dansi music.

Get well soon Bro!
 
Banza Stone

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=8TM4uJx8rnY"]Mtu pesa[/ame]
 
Nadhani hapa Banza haitaji msaada mkubwa zaidi ya ushauri nasaa. Sisi tulioko mbali it could be just difficult to offer counselling, ila natumaini wale mlio karibu na M'nyamala sio mbaya mkipita hapo leo jioni na kumfariji.

Pole sana Mwana-Masanja as you once said/imba "Kabla hujafa hujasifiwa"!
 
Nakumbuka enzi enzi za... aungurumapo simba mcheza nani, nguruma...nguruma, Abu Semuhando, Baba Diana, Luiza Mbutu..


... Twanga pepeta ninavyoipenda nitakunywa sumu juu yako...

Wimbo huu ukipigwa Clouds FM katika Afrika Bambataa, ukishereheshwa na mwenyewe Chaz Mwamiji na Marehemu Amina Chifupa. Mwili ulikuwa ukisisimka, nadhani wengi wanakumbuka miaka hiyo ya mwishoni wa tisini na mwanzoni mwa 2000, Banza alitukonga haswaa.

Pona Banza.
 
Masikini kwa kweli inasikitisha sana maana hizi bangi zitamaliza wengi, inabidi wengine waone mwisho wake ulivyombaya, wajitahidi kuiacha.

Tunaoweza tujitahidi kumsaidia
 
Back
Top Bottom