Uchaguzi 2020 "Bao la mkono" uchaguzi 2020 lina nafasi bado?

Uchaguzi 2020 "Bao la mkono" uchaguzi 2020 lina nafasi bado?

AVRAM

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2017
Posts
616
Reaction score
885
Hivi Watanzania mnahisi kulingana na mazingira ya kisiasa yalivyo hivi sasa, hili linaloitwa "Bao la mkono" linaweza kutumika kuhakikisha ushindi wa chama tawala katika uchaguzi wa mwaka 2020?

Hoja kuhusu Bao la Mkono, imeibuka ghafla kutoka kwa Mbunge wa Tandahimba kupitia tiketi ya chama cha CUF, Katani. Mhe. Mbunge alisema "Bao la mono mmeljfanya kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Uchaguzi mkuu lile bao haliwezi kupatikana Tandahimba, natoa rai, mapema sana, Nyinyi wakubwa mnaotumwa mnaosimamia uchaguzi, mkidhani tunavyokwenda kwenye uchaguzi mkuu, mtapewa maelekezo yale mnayoyafanya, mihuri ya vyama vya siasa inajuilikana na vyama vinajulikana, Msiseme wagombea wa CUF hawana sifa. Pasipo na haki hakuna hiyo amani mnayoisema".



KUMBUKUMBU

Stori za bao la mkono zilikuwa hivi baada ya uchaguzi Mkuu 2015 kumalizika na kutokea yaliyowahi kutokea.

‘Bao la Mkono’ lamtoa chozi Nape

Nape Nnauye, Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi sasa anajutia kauli yake ‘bao la mkono’ aliyoitoa miaka minne iliyopita........

Mheshimiwa Nape aliwahi kuzungumza na kituo kimoja cha Runinga hapa nchini tarehe 18 Februari 2019. Nape amesema, kati ya alama atakazokwenda nazo kaburini ni kauli yake ya ‘bao la moko.’

Kumbukumbu zinaonesha kauli hiyo aliitoa wakati wa mkutano wa hadhara Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika kwenye Viwanja vya Nyehunge, Sengerema mkoani Mwanza tarehe 22 Juni 2015.

Alikuwa katika ziara zilizoandaliwa na Abdurahman Kinana, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM kwa ajili ya kukagua utekelezwaji wa Ilani ya chama hicho kwa kioindi cha mwaka 2000 - 2015 kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015.

Mhe. Nape alisema “Sitaki kujitetea katika hili, ingawa nia yangu haikuwa mbaya. Nami nimeshakubali, kama ni alama iliyo mgongoni kwangu ambayo nitaenda nayo kaburini, ni hii ya bao la mkono,”

Akionekana kujutia kauli hiyo Nape amesema, kabla ya vyombo vya habari kulishikilia suala hilo, Mhe. Kinana kama mtu mzina, alimwambia kuwa amekosea na kwamba, ajiandaye kwa tafsiri tofauti kutoka kwa jamii.

Mhe. Nape aliongeza kuwa “Sikuwa na tafsiri ile, ni kama mpira, hivyo kunaweza kutokea mazingira ya aliyefungwa kutoridhishwa na matokeo ya kufungwa, lakini kama refarii (Muamuzi) hakuona kosa, unabakia kuwa ushindi,” amesema Nape aliyewahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM na kuongeza;

“Unaposhindana na mtu, anaweza kusogeza kura na kushinda kama mazingira yanaridhisha na katika mataifa makubwa kama Marekani wanafanya hivyo.”

Nape anasema, kauli yake hiyo ilipinduliwa na kutafsiriwa kwamba, CCM ilijipanga kushinda kwa kuiba kura.
 

Attachments

  • Instagram(1).mp4
    2.9 MB
Back
Top Bottom