Msiojua biashara ni nini mtamcheka Aunt Ezekiel! Nadhani Wafanyabiashara mnaelewa Hustle ambazo huwa mnapitia hadi biasha isimame! Kuna muda kwenye Biashara Utapigwa matukio hadi utamani kuua mtaa mzimaa lakini unapiga moyo konde! Kuna Muda kwenye Biashara Unafilisika mara 10 lakini ukikata tamaa ndio umekwisha japo waaulimwengu hawawezi kosa Sababu!
Nachokijua Hawa wafanya biashara wakubwaa duniani hakuna aliefanikiwa chini ya Miaka 15 karibia wote wame hustle zaidi ya Miaka 15 hadi biashara zao kuja kusimama na kuendelea! Ninacho kiona hapa ni kwasababu Aunt Ezekiel ni Mtu anae fahamika ndio shida ila huko mtaani biashara nyingi tuu zinakufa na kuzaliwa hadi mtu atakapo kuja kufanikiwa! Ukichanganya na Masharti Ya Serikalii Biashara Tanzania Ni Ngumu sanaa hadi kufanikiwaa Unaweza kuta mtajii wote unaishia kwenye kutafuta Vibali! Ndio maana Wanasema Enterpreniuer yoyote lazima Uwe mbabe ili ufanikiwe! Usione Hizi hospital mnaenda kutibiwa mnapona Jua ameshafungiwa mara kadhaa ameshapigwa vita vya kila aina,Msione hizi bar mnaenda mnalewa mkazani zimeibuka tuu! Vitu ni Vingi! Watu Wenye Makanisa Tuu Wanapata Tabu Sembuse Bar? Kifupi Biashara ni Ngumu na inahitaji ujasiri na uvumilivu.
Ukiona Mtu amefunga biashara yake Usimchekee nenda kajifunze kwake itakusaidia! Sio kazi nyepesi! Huwa napenda sana kujifunza kupitia waliofanikiwa kujua changamoto kifupi changamoto ni nyingi usipo funga biashara yako basi polisi utaendaa either kwa kushtakiwa au kwa kushtaki!
Hakuna Mafanikio yanayo kuja by Chance! Kila kitu ni kupambana nikoona mwanamke kama Aunt anapambana namuheshimu sanaaa Nakumbuka Mama Angu alipambana kunilea kwa kuuza Nyasi za Kuezekea Nyumba! Mwisho wa Siku Maisha yailienda Jabo hiyo biashara pia alipigaa vita vilevile! Tumseme Mtu kwa Yote Kuhusu biashara acheni kama ilivyoo! Ukiona Umeanza leo kuuza nguo na kusema umefanikiwa ndani ya Wiki 1 jua biashara yako haitakuwa Kamwee!! Kuna Watu wanaacha Kazi maofisini wanalipwa millioni 5 lakini wanaenda kwenye biashara zinakufa mara kadhaa lakini wanasimama imara
Kwenye biashara mataifa haya nayapenda sana INDIA,ETHIOPIA,ZIMBABWE yaani Mmoja Akiwa Na Duka Atafanya kila namna amelete Mwenziee nae afanikiwe kwa njia yoyote ile ILA SIO TANZANIA akifanikiwa anataka afanikiwe yeye tuu ili amcheke mwenzie
AUNTY WAKUCHEKE,WAKUSEME USIKATE TAMAAA PAMBANAA HADI DAKIKA YA MWISHO IKIWEZEKANA ACHA KUIGIZAAA SIMAMIA BIASHARA YAKO.