Capital
JF-Expert Member
- Oct 12, 2010
- 1,468
- 1,063
Ndugu wana jamii intelligence (JI), nimekuwa nikijiuliza ni kitu gani kilocholikumba bara la Africa.. kiasi ambacho kwa miaka takriban 2000, bado ni bara omba omba, la hovyo kabisa na dhalili.. watu wake wakiwa hawana cha kujivunia? Wakati hali iko hivi.. mabara mengine yakiwa katika maendeleo makubwa kabisa.. wana elimu, mali na pesa nyingi sana, kwa ufupi wako akhera kama ile inayohubiriwa katika vitabu vya dini. Waafrica bado ni watu wanaoishi muda mfupi duniani, wakizongwa na kila aina ya hatari.. magonjwa ya kutisha, ajali za ovyo ovyo, njaa isiyo kifani na chuki baina yetu wenyewe..
Jambo ambalo nafikiri ni chanzo cha madhira haya ni kutofahamu tu kuwa bara la Africa lilitekwa miaka mingi iliyopita, na watu wake wakawa mateka. Kuwa mateka ni kitu kibaya sana hasa pale ambapo wahusika -yaani mateka hawajitambui kuwa wametekwa.. yaani wapo wapo tuu..
Africa ilitekwa kivipi?
Hapo awali.. bara la Africa lilikuwa na maendeleo makubwa sana.. walau kwa viwango vya wakati ule. Na maendeleo haya yalidumu kwa muda mrefu sana. Lakini pia yalitokea matatizo baina ya waafrica wa wakati huo ikiwemo vita baina ya koo na makabila, magonjwa na mabalaa mengine. Waafrika yumkini hawakuwa na mbinu au organizesheni ambayo ingewafanya wainuke kwa pamoja.. wao ilipotokea balaa, njia rahisi kwao ilikuwa ni kuhama tu kuelekea sehemu ya mbali na isiyojulikana.
Miaka ya 500-100 BC, huko Afrika ya kaskazini mambo ilikuwa moto.. Waafrika walikuwa wanendelea kudhoofika ndani kwa ndani lakini pia kimataifa. Wavamizi walianza kuingia, kwa vita kali kali. Hatimaye katika karne ya kwanza CE, Afrika hatukuwa na chetu.. wavamizi walishaanza kufanya Afrika kuwa maskani yao. Na kufuatia udhaifu uliokuwapo, wavamizi ws kirumi na kigiriki waliishi Afrika bila kipingamizi. Jiji kubwa kama Carthage liliharibiwa na wakazi wake kuhirikishwa kabisa..kwingineko, hali ilikuwa mbaya sana ikabidi watu wengi wa kaskazini wakimbilie kusini. Falme kubwa kubwa za Nubia, Kush zilipotezwa kutokana na vita kutoka kwa wageni.
Vile vile, watu weusi waliokuwa Ulaya walikutwa na fate zilishabihiana yaani genocide. Hadi kufikia 500CE.. Afrika kulikuwa kiimya.. watu wamechanganyikiwa, wanaishi maporini na mapangoni.. kiufupi wanaishi kama nyani. Katika miaka ya 600CE, uislam ulichukuwa sura mpya.. waafrika wakazidi kuwekwa chini ya ulinzi na kuwa mateka zaidi... nchi kama Somalia, Sudan, Morocco hadi Senegal ziliwekwa chini ya himaya ya wageni. Waafrika wasingeweza kutokeza ukinzani wowote badala yake walifuata kila walichoelekezwa..
Kwa kipindi kirefu wazungu wa ulaya walikuwa wamekaliwa vibaya na iliyokuwa ikijulikana kama Ottoman Empire
. Dola la kiislam lilotawala dunia Baada ya kufariki kwa Mtume Mohamed SAW.. ndipo karne ya 15 wakaibuka. Victim wa kwanza alikuwa Africa. Hawa wazungu waliingia hadi sehemu za mbali za Afrika, wakiharibu na kupora na kuuwa watu weusi kama nzi. Waafrika hawakuweza tena kutia ngumu.. tayari walishaisha. Hawa wavamizi wapya walijiingilia tu kadri walivyotaka. Falme kama za Zimbabwe na kwingineko ziliharibiwa kipindi kile. Hapa Tanzania mnakumbuka magofu ya Kilwa. Hii haikuwa bahati mbaya, ilkuwa ni vita kali kabisa yenye lengo moja, kuichukuwa Afrika mateka. Ni mlolongo mrefu sana wa matukio, ukiunganisha hata na utumwa.. ma ukoloni na ukoloni mamboleo.
Sasa tuko hapo
1. Sisi mateka tulikubali kila kitu walicho tuambia tufanye.. ikiwemo ni nini tuabudu, lugha gani tuabudu na wapi tuabudie.. mateka tukasema duhu shiida
2. Wakasema ni lazima mkasome lakini cha kusoma tunakijuwa sisi, hatukupinga na wala hatutapinga.. tunasema powaa
3. Wakasema madini tunataka halafu nyie mtaajiriwa tu.. hamnana matumizi nayo haya makitu.. tukasema.mmalize hata kesho.. kwani ya nini?
4. Wakasema ninyi ni maskini hamuwezi kutufikia tulipo.. na ni kupoteza muda.. kama kawa.. tumeridhiika kabisa.
Kutokana na athari hizi za kuishi kimateka mateka.. Waafrika ni watu waoga sana kwa vinavyojulikana na visivyojulikana, vinavyoonekana na visivyoonekana.
Hali ya umateka mateka imetufanya kutothaminiana (maana sote mateka) ila kuwathamini watu wa nje. Mfano wa wazi ni kuwa wahindi wa hapa Tanzania wanamiliki zaidi ya 80% ya uchumi wetu.. na hii iko karibia Afrika nzima. Ukienda South Africa.. Senegal, Kenya, Zambia.. uchumi umeshikiliwa na wageni.
Nini tufanye
Kiukweli ni vigumu kusahihisha makosa yaliyotendeka miaka 3000 iliyopita ndani ya kipindi kifupi.. hata kama ni miaka 100. Ila pa kuanzia ni haswa kutambua hali tuliyomo ya kuwa tumechuliwa mateka na kimsingi.. chochote tunachokifanya ni kulingana na matakwa ya aliyetuteka.. moja kwa moja au kinyume chake.
Tutafakari kwanza hapo.. nipo nitakuwa nawapa manondo kuhusiana na kadhia hii