Kwa barabara zetu kuu ( Highways) hivi hakuna kigezo kwa wakandarasi wa barabara kuweka vivuko vya watembea kwa miguu stahili zaidi ya kuchora mistari ya pundamilia? Nimeandika hivi kwa sababu barabara zetu kuu karibia zote zimejaa matuta na Zebra kitu ambacho nahisi kinaweza kuwa hata nje ya utaratibu wa kimataifa wa barabara kuu.
Kwa nini wasiweke vivuko vya miguu simple tu kama vya nchi za wenzetu (sitarajii mtu aje na madirio ya gharama ya likivuko kama lile la ubungo)