KERO Barabara kubwa ya Kilwa ni changamoto. Mamlaka wawajibike

KERO Barabara kubwa ya Kilwa ni changamoto. Mamlaka wawajibike

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Hali ya barabara hii, kwa kweli ni aibu.

Miaka nenda miaka rudi hakuna anayeliona hili. Tuna viwanda vikubwa katika barabara hii ya Kilwa kuanzia Mbagala kokoto barabara haifaii aibu, kila kukicha ajali haziishi, wananchi kuchelewa kutokana na foleni. TANROAD, Iko wapi? Kwanini hamwajibiki na majukumu yenu?

Barabara yenyewe finyu, aaahhh jamani mnatia aibu kila siku kutupa mabilioni kwa ujenzi wa barabara zingine huku Kilwa road mmeitelekeza au mnataka hapo pia mze Said Salim Bakhresa awekeze hela atakayepita hapo alipie huduma ya kujengewa? Kodi tunazotozwa zinaenda wapi?

Serikali nayo imekaa ikitizama ufisadi huu?

 
Kutoka Mbagala kwenda Kongowe tu hapo mtu aliyetoka Dar kwenda Moro na Abood anaweza kufika akakuwahi. Ni aibu sana!
 
Back
Top Bottom