Barabara ya Goba mpakani, hii sio hujuma?

Mshobaa

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2013
Posts
1,714
Reaction score
677
Habari wakuu,

Mnamo mwaka Jana zilikuja taarifa hapa juu ya hii barabara ya Goba mpakani ilivyokuwa hatarishi kupitika baada ya kupigiwa kelele hapa hapa jamvini wahusika mara moja wakaenda kuichonga.

Sasa basi hii barabara kwa kweli ina hali mbaya sana kwa sasa, wahusika ni Kama hawaioni kabisa. Baada ya kufatilia hili suala kwa kina nimegundua yafuatayo..,

Kuna bajaj zipo eneo la Tegeta A zinafanya rout kutoka hapo hadi mwisho yani Goba mpakani, ambazo ni mradi wa kigogo mmoja wa eneo hilo mwenye mamlaka.

Barabara haichongwi kwa maslahi yake binafsi maana gharama ya usafiri kutoka hapo Tegeta A hadi Goba mpakani ni tsh 1500 had 2000 wakati hapo mwanzo nauli ilikuwa kati ya 500 hadi 800 tu.

Ombi langu kwa Tarura na halmashauri ya manispaa ya Ubungo muwe mnatembelea hizi barabara kujionea wenyewe badala ya kukaa maofisini na kusubiria kuletewa taarifa, hivi majuzi kuna lori kubwa la mchanga lilidumbukia kwenye mojawapo ya mashimo hayo na kupinduka miguu juu.

Bahati nzuri ilikuwa ni usiku ingekuwa mchana tungesema mengine hapa maana eneo hilo kuna watu wengi wanapita na kufanya shughuli zao.. Pia kesho yake gari ya abiria ikapinduka na abiria wake.. Tusisubirie hadi yatokee maafa ndio tuje kupeana pole za kinafiki hapa.......

Pia Soma:
- KERO - Serikali kupitia TARURA msikie kilio cha watu wa Goba mpakani (Tegeta A)
 
Jana tumezibiwa njia siku nzima na lori la mchanga lililodumbukia tena kwa mara nyingine hii ni laana walah
 
Dunia ya Leo habari bila picha au video clip sw hakuna.
 
Poleni sana Mkuu, unaweza kupiga picha eneo zinapopatia ajari?
 
Hii barabara hadi Sasa tumechanga zaidi ya milioni 16 wananchi wa goba kwa kauli ya “Task force team barabara Goba” na tarura wanasema wameanza ni wezi hawa
 
Hivi ni kwamba viongozi hawaoni au jeuri? Hatutaki waje kutupoza kipindi cha kampeni
 
Hii barabara tuliambiwa na TARURA kwamba mwezi June itaanza kujengwa. Leo tuko Agost hakuna hata dalili na insemekana kuna watu washapiga mzigo, mradi umekufa
 
Hii barabara ndiyo inaanzia pale Njia panda ya Tegeta A karibu na Skymart Supermarket? Mshobaa
 
Hii barabara tuliambiwa na TARURA kwamba mwezi June itaanza kujengwa. Leo tuko Agost hakuna hata dalili na insemekana kuna watu washapiga mzigo, mradi umekufa
Ni kweli ilisemekana ingewekwa lami kuanzia mwezi wa 4 ila mpaka sasa hamna kitu. Hivi sijui huyo mbunge wa Kibamba kazi yake ni nini huko bungeni..?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…