KERO Barabara ya Goba Tegeta A/Kulangwa bado inatia mashaka mvua zikianza school bus zinapita sehemu hatarishi

KERO Barabara ya Goba Tegeta A/Kulangwa bado inatia mashaka mvua zikianza school bus zinapita sehemu hatarishi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Ms Billionaire

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2020
Posts
2,452
Reaction score
4,955
Habari ya leo wadau.

Salamu kwa Rais Samia.

Mimi ni Mwanachi wako mkazi wa Goba mwaka wa 12 huu. naleta malalamiko kuhusu njia ya Tegeta A iliyoungana na Kulangwa Nimeishi huku miaka mingi na changamoto yetu kubwa ni barabara.

Nilileta malalamiko yangu miezi michache iliyopita kuhusu barabara za Tegeta A na Kulangwa ila changamoto tunayoihofia ni kipindi cha mvua hatuna CARAVAT inayoeleweka tegeta A karibu na KITUO CHA AFYA cha ST YOHANE.

Goba kuna shule nyingi sana kama Victory Adonai, Victory Christian Center na nyingine nyingi, school bus nyingi sana zinapita kwenye hili caravat ninalo lilalamikia asubuhi na jioni, ni hatari kwa schoolbus za watoto wetu hata kipindi hiki ambacho sio cha mvua ni hatarishi vipi pakizidisha unyevu na udongo ukamomonyoka?

Serikali tunaomba itusaidie KUTANUA hili daraja na waweke caravat imara na lenye upana ili watoto wetu wapite vizuri bila hofu matukio ni mengi na kinga ni bora kuliko tiba msije sema hatukuwaambia mapema.

Rais Samia tunaomba utusaidie kuwakumbusha viongozi uhai wa watoto wetu ni muhimu sana hii ni hatari na hatuna njia nyingine ya kupitisha watoto wetu. Ikiwezekana hii njia ichongwe hadi mwishoni kule kanisa la Roman Catholic Tegeta A karibu na hiyo shule ya Victory Christian.

Soma Pia: Changamoto ya barabara mbovu Goba Kulangwa/Tegeta a Serikali inapuuza?

Siku nimeenda shuleni kwa mwanangu nimepita kwenye hilo caravat moyo ulitetemeka nikasema watoto zaidi ya mia wanapita hapa kwenye schoolbus tofauti kwanini hatuwekei uzito wa hili caravat kutengenezwa? Kwasababu mimi nakaa upande wa kulangwa lakini watoto wanasoma Tegeta A lazima nitetee haki ya wote hata kama mimi situmii hiyo njia. Watoto watasemewa na nani?
IMG_0667.jpeg
Iliwahi kutokea changamoto ya school Bus ya watoto kunusurika kuleta maafa. Ila maafa ya hili caravat ni mabaya kuliko kawaida tunaomba litengenezwe upya.

Hatutaweza kuvumilia kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa muongelee mambo mengine wakati hatari kama hizi hamzi solve.

Rais Samia kwa maelekezo mazuri tu nikuelezee watoto wetu na school bus zinapopita kwenye caravat mbovu ni ile njia ya Goba Kulangwa/Tegeta A inachepua kushoto kabla ya skymart supermarket kama umetokea njia nne ile njia inayoenda St Yohanne Health center na Victoria Adonai school inanyooka hadi makanisa ya Anglikana na katoliki kuelekea madawa.

Tunaomba msaada ile njia ichongwe vizuri maana hiyo ndo njia yenye caravat bovu lipo karibu na kituo cha afya ya ST Yohanne hata ukituma watu wako wanaweza kwenda kuliona. Ni hatari mno kwa watoto wetu.

Jengeni daraja kubwa wekeni na kingo pembeni.
Nawasalisha
 
Hilo lilijengwa na mhandisi? Tuna safari ndefu kufikia malengo.
 
Haya mambo siku likitokea tukio zito hapo utaona viongozi wote wa manispaa wanakusanyana na tarura wao, wakati sasa hivi wana nafasi ya kuzuia kabla ya maafa.
 
Hii ni Goba ingine au ile ile watu wanaosema ni ya kishua?
 
Haya mambo siku likitokea tukio zito hapo utaona viongozi wote wa manispaa wanakusanyana na tarura wao, wakati sasa hivi wana nafasi ya kuzuia kabla ya maafa.
Mimi sielewi kwanini wanashindwa ku take precautions na kelele zote hizi tunazopiga. Sijui viongozi wa mitaa wanapita njia gani kama hili hawalioni
 
Ni hatari MNO!!





KAZI ni kipimo cha UTU
 
Back
Top Bottom