Barabara ya Ilala Boma iwekwe mataa ya muda, ni hatari kwa watembea kwa miguu na wenye magari pia

Barabara ya Ilala Boma iwekwe mataa ya muda, ni hatari kwa watembea kwa miguu na wenye magari pia

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
593
Reaction score
1,376
Wakuu,

Barabara ya Ilala Boma eneo lile ambako ni karibu na karume kulikuwa na mataa ya kuongozea magari mwanzo, lakini baada ya kuanza ujenzi wa mwendokasi mataa hayo yalitolewa.

Sasa hivi kumekuwa vurugu mechi, ni hatari kwa wenye vyombo vya moto lakini ni hatari zaidi kwa watembea kwa miguu, maana magari, boda na bajaji ziapita ovyo ovyo tu kila mtu akiwa na haraka zake, usipokuwa makini unaweza kugongwa hivi hivi unajiona.

Lakini pia kunakuwa na foleni ambazo hazina hata maana, sababu muda wote trafiki inabidi awepo kutokana na kuwa hakuna mataa, asipokuwepo unakuta mnyonyoro wa maana.

Mamlaka husika fanyieni kazi hili, mbali na kuwa ni kero ni hatari pia kwa watumizi wa barabara hiyo.

Pia soma:
Pongezi kwa barabara ya Kilwa kuwekewa taa za kuongozea magari
 
Back
Top Bottom