Boda boda msomi
Member
- Oct 7, 2024
- 9
- 10
Hii barabara ya Kilwa kipande cha kushuka hapa Kokoto kuja daraja la Mzinga mpaka Kongowe imeshakuwa kero kubwa sana kwa wakazi wa huku maana foleni haziishi sababu barabara ni nyembamba kiasi gari likiharibika hapo ni majanga inabidi mkae foleni mpaka either gari litolewe au askari wasimamishe na kuruhusu magari ya upande mmoja mmoja huku muda ukiendelea kupotea kwa sisi tunaotegemea kuitumia kila siku.
Barabara pia ina mashimo mengi mno na mkandarasi anaweka viraka tu tena kwa muda anaotaka yeye, kama hivi sasa amekata mashimo ya viraka kayatelekeza bila kujali kwamba yanasababisha usumbufu na ajali kwa watumiaji.
Pia daraja la mto Mzinga pale ni la chuma limepata kutu sana kutokana na kukaa muda mrefu, ukipita sehemu za watembea kwa miguu unaona lilivyoanza kumegeka ni hatari pia daraja ni jembamba sana ukilinganisha na aina na idadi ya magari yanayopita pale ambaye mengi yanasafirisha mizigo.
Soma Pia: Barabara ya Kilwa kipande cha Mzinga Kongowe kinatumaliza
Jamani mamlaka zinazohusika ziangalie barabara hii wasisubiri yatokee maafa ndio waje na salamu za kiunafiki wananchi tunaumia.
Naomba kuwasilisha