Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
TUTEMBEE KWENYE BARABARA YA KUMBUKUMBU KUTOKA USUKUMANI KWA CHIEF MAKWAIA MOHAMED MWANDU (1905 - 1945) HADI KARIAKOO KWA ABDULWAHID KLEIST SYKES (1924 -1968)
Chief Makwaia Mohamed Mwandu ndiye baba yake Chief David Kidaha Makwaia.
Mtoto wa Chief Makwaia, Chief Kidaha (1922 - 2007) alifikiriwa kuongoza TAA mwaka 1951na waunde TANU mwaka unaofuatia yaani 1952 lakini haikuwa.
Hiki ni kisa kisichofahamika na wengi.
Chief Kidaha alikuwa chaguo la Abdul Sykes lakini Hamza Mwapachu (1913 - 1962) yeye alimtaka Julius Nyerere.
Sheikh Hassan bin Ameir (1880 - 1979) Mufti wa Tanganyika alisimama bega kwa bega na Nyerere akiitangaza TANU misikitini na kuuza kadi za chama katika darsa zake hadi uhuru ulipopatikana mwaka wa 1961.
Nani leo anaejua historia za wazalendo hawa?
Leo inapozungumzwa kumtanguliza Mungu ni muhimu sana kuwakumbuka masheikh wazalendo waliouza kadi za TANU misikitini na kufungua mikutano ya TANU tena ya hadhara kwa kusoma Qur'an.
Je, tunae kiongozi wa dini, mzalendo mfano wa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir?
Imekuwaje hatajwi katika historia?