Barabara ya lami iliyokuwa inajengwa Kigamboni mnadani imekamilika lakini bado imefungwa kusubiri uzinduzi; Wakati wananchi wakiendelea kutaabika

Ndio Imefunguliwa kwasababu wamejiridhisha, na sio kwasababu ya ubwekaji 🗣 wako wa, Humu Jf.
watu wengine akili zenu ziko makalioni ! Huna hata aibu kuanika ujinga hadharani
 
Hizo barabara si ndo tunaambiwa maendeleo ya vitu hayafai! Kumbe zikifungwa mnatabika?
sijui hata uneuliza nini! kufunga njia watu wasipite Ni vitu au Ni Watu? au Ile barabara wanapita chama kimoja tuu?
 
Nilipita kipindi cha mvua apo nikatamani kugeuza kipande chenyewe kidogo sana sidhani kama kina 3km
Yani kipande chenyewe kidogo ivyo alafu mpk waje wazindue mbona tunaishi maisha ya shida sana
 
Yani kipande chenyewe kidogo ivyo alafu mpk waje wazindue mbona tunaishi maisha ya shida sana
Walianza wakazindua daraja likiwa linajengwa, lilipokamilika tena wakazindua, walipojenga ofs za nssf za kukatia tiket wakazindua, walipojenga Ile lami wakazindua, Yaani barabara moja uzinduzi Mara kibao
 
Ndio Imefunguliwa kwasababu wamejiridhisha, na sio kwasababu ya ubwekaji [emoji2788] wako wa, Humu Jf.
Tangu wamalize kuijenga siku moja kabla ya thread ya JF ndio wajiridhishe na kuifungua ? acha kua mpumbavu na wewe.
 
Tangu wamalize kuijenga siku moja kabla ya thread ya JF ndio wajiridhishe na kuifungua ? acha kua mpumbavu na wewe.
Kamtukane mama yako, nyumbu wewe.Kama unadhani mambo yanaendeshwa kienyeji namna hiyo, anzisha Uzi humu, ili Jambo lingine litekelezwe kesho, mpumbavu wewe.
 
Tangu wamalize kuijenga siku moja kabla ya thread ya JF ndio wajiridhishe na kuifungua ? acha kua mpumbavu na wewe.
Au we nyumbu, unadhani kujiridhisha kunachukua muda gani.?
 
Hizo barabara si ndo tunaambiwa maendeleo ya vitu hayafai! Kumbe zikifungwa mnatabika?
Mkuu suala sio Kushadadia Lami, Hicho kipande cha barabara ndio kiunganishi maeneo muhimu, kilikua na vumbi ndani ya mwaka mmoja na nusu watu tulipita vizuri , sasa lami imesababisha ifungwe na kufanya Ufikaji wa maeneo tofautitofauti uwe mgumu sana

Ungetembelea hilo eneo kabla na baada, Nawe Ungeguswa na hili ila Tunashukuru sasa imefunguliwa
 
Nakumbuka kuona kwenye taarifa ya habari ya Tarehe 1 mwezi wa 9. Siku ambayo, mkandarasi alitakiwa kukabidhi kazi.

Akasema, Wamemaliza kuweka lami jana yake, bado kuchora mistari. Lakini hawawezi kuchora kabla ya lami kukauka vizuri.

Akaomba wiki 2 ili aweze kukamilisha hiyo kitu.

Hayo mengine sijui ya kiki, nadhani ni mtazamo wako. Na hiyo ndiyo demokrasia.

Hivi, kiongozi gani kaenda kuzindua vile?? Au unajidai kuwa posti yako yenye comment 50 na kitu imewafikia wakaona kuifungua bila uzinduzi?? [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Wewe hujui chochote nyamaza! Eti lami haijakauka vizuri! HIVI KWA AKILI YAKO NDOGO UNAZANI LAMI Ni Kama nguo kwamba inahitaji mwezi kukauka!
Kama hujui uliza !
Baada ya kuwekwa layer zote lami huhitaji nusu saa tu baada ya kumwagwa! lami ikishapigwa upepo ikapoa tu tayali inaweza kupitika!
NDIYO MAANA KUNA SEHEMU lami inaewekwa upande mmoja Gari zinaruhusiwa kupita!
Lami siyo Kama zege la slab Elimika ndugu!
Kasome ASPHALTIC behavior
 
Basi Msamehee bro,kesha kusoma!!
 
Ndugu, raha ya siku hizi, huhitaji kutumia nguvu nyingi kubishana. Video zipo.

Bishana na hii video basi. Maana vyote nilivyo eleza kwenye posti yangu ya kwanza, vimeelezwa hapa.

Maana kila mtu anajidai mjujiaji.
Hii mitandao inaumbua sana.
Na just kukuelimisha New Asphalt inachukua 48 to 72 hours kukauka kiaina kwa ajili ya wapita kwa miguu na magari. Then ndiyo waanze kupiga mistari.

Hiyo ya kukauka nusu saa ni kama una resurface, yaani unaweka tena layer ya juu kwenye barabara ambayo ilikuwa nayo kabla.

Naomba urudi tena darasani.
 
Uko sahihi kabisa Ile barabara inayoendelea kwenda Kibada baada ya hicho kipande, lami iliwekwa magari yakapita nusu saa baadae na haikufungwa siku nzima
 
Uko sahihi kabisa Ile barabara inayoendelea kwenda Kibada baada ya hicho kipande, lami iliwekwa magari yakapita nusu saa baadae na haikufungwa siku nzima
Kama ni lami mpya, huchukua masaa 24 mpaka 72 kukauka ili watu na magari yaweze pita. Kama unaweka layer ya juu kwenye lami ambayo ilikuwepo, inachukua nusu saa kukauka.
 
BARABARA imefungwa zaidi ya wiki tatu! wewe unapiga kelele eti haijakauka!

Kwanza tambua kwamba Cha Mhimu katika barabara Ni zile layer kuanzia chini kabisa SUB GRADE CORE! material yanapiwekwa na kushindiliwa huwa yanategemea na aina ya udongo!

Mambo yooote yakishafanyika kabla ya kuweka lami Lazima iwekwe GUNDI MAALUM ambayo Ni primer coat ! Hii huchukua siku tatu 72hrs Hadi siku Saba kukauka,(Hii Ni Kama lami chafu ambayo wengi ukiwemo wewe mbishi huzania kuwa Ni ndo lami)
PRIMER IKISHAKAUKA ambayo ndiyo gundi kushikilia kokoto, Ndipo asphalt (lami) huwekwa juu yake kwaajili ya mseleleko! Lami Ni material maalum ambayo huchemshwa kwenye furnace kwa kuchanganywa na kokoto ndogo ndogo (chipping) ambayo huyeyuka kwenye joto Kali na Ikipoa huganda na kuwa ngumu!
Lami ikiwa exposed kupoa huchukua hata nusu saa ( tambua kwamba lami ubora wake Ni pale ikishapoa tu inakuwa tayali)

NOTE; Kazi ya lami siyo kuhimili UZITO WA MAGARI Bali Ni kurahisisha magurudumu kuzunguka kwa mseleleko ulio rahisi!
Ni Kama godoro na chaga! lami Ni kapeti la juu for easy trafficking!

KWAHIYO HICHO ULICHODESA HAPO JUU NI PRIMER (LAMI CHAFU) NDIYO HUHITAJI MDA MWINGI KUKAUKA !
Barabara Tunayoizungumzia hatua hizo ilishapita ndiyo maana wakaweka lami!

Kama hujaelewa! kaangalie hata wanapoweka vilaka barabarani wanapomaliza kusmooth lami magari hurusiwa siku ileile!
LAMI NI LAMI TU HAIJALISHI unajazia (OVERLAYING) AU UNAWEKA UPYA!

USIWE MBISHI
 
Kama ni lami mpya, huchukua masaa 24 mpaka 72 kukauka ili watu na magari yaweze pita. Kama unaweka layer ya juu kwenye lami ambayo ilikuwepo, inachukua nusu saa kukauka.
Layer ya juu ndo nini! LAMI NI ILEILE Iwe unafanya OVERLAYING AU IWE NI MPYA!
kazi ya lami siyo kubeba. mzigo Bali Ni kusmooth barabara!
Kinachochelewa kukauka ambacho unakizungumzia wewe Ni PRIMER!
hiyo Ni Kama lami chafu inayochanganywa na rude oil !
Haya Ni makapi ya mwisho katika uchakataji wa mafuta petrol!
Hii primer huchukua masaa 48 Hadi siku Saba kukauka! baada ya hapo ndipo lami huwekwa!
Lami Siri yake Ni ikishapoa tu tayali inakuwa tayali kupitika! Mara nyingi hukauka kuanzia nusu saa
UKIONA SEHEM WANAWEKA LAMI MAANAKE KAZI IMEKWISHA!
USIWE MBISHI

Lami ikipata joto Kali huyeyuka! na ndiyo maana magari yenye mizigo mizito yakipita sehem ambapo lami ikiwa imepata joto Kali hususani mchana wa jua Kali tairi hubonyeza lami kwasababu inakuwa imeyeyuka!

Natamani nikuelimishe zaidi uelewe kwanini LAMI NI NYEUSI ILA kwa ubishi wako hii inatosha
 
Ndugu acha ubishi.
Yaani unaanza kutoka kwenye mada kabisaa na kuongelea kazi ya lami.

Kubali mada yako haina mashiko.

Walitakiwa kukabidhi kazi tarehe 1 mwezi wa tisa, na ndiyo siku ya hiyo video hapo.

Na wao ndiyo wameomba waongezewe wiki mbili. Na mpaka kufunguliwa, haijafika hiyo wiki mbili. Wewe unakuja unazungumzia wiki 3.

YAANI KWA SABABU UNATAKA JAMBO LIONEKANE LA KISIASA BASI UNA KATAA MPAKA USHAHIDI WA VIDEO.

SASA UNALAZIMISHA KUHALALISHA MADA YA OVYO ULIYOANZISHA. KITU KIPO WAZI, KIMEELEZWA VIZURI KABISA KWENYE VIDEO. WEWE UNABISHA UNALETA MAELEZO YAKO.

Ukitaka leta mpaka definition za lami, magari ya ujenzi wa barabara, hell, ongea hata Kifaransa, lakini ukweli unabaki palepale. Hii posti ulikurupuka.

ETI WANATAFUTA KIKI YA KAMPENI.
BARABARA IMEFUNGULIWA NDANI YA HIZO WIKI MBILI. NA HAKUNA MGOMBEA ALIYEENDA KUZINDUA.

UCHA KULAZIMISHA UJINGA WAKO HAPA. WAPELEKEE UJINGA HUU WATU WENGINE.

JAMII FORUM INA WATU WANAO JIELEWA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…