Katika mfumo wa kupunguza foleni barabarani hapa Dar, inatakiwa kipaumbaele kiwekwe kwenye kujenga barabara za mzunguko (ring roads). Barabara mojawapo ni hii inayoanzia Mbezi Beach - Goba- Mbezi Louis - Kinyerezi hadi Uwanja wa Ndege wa Dar.
Waziri wa Ujenzi naona kaisahau hii barabara pamoja na kwamba daraja la mto Msimbazi linajengwa.
Hii barabara nakumbuka kwenye miaka ya 2006 - 2009 ilipigiwa debe sana ijengwe lakini baadaye sikuona chochote kufanyika zaidi ya kuweka nguzo kuonyesha eneo la barabara (road reserve). Hii barabara kwa sasa inapitisha magari mengi (traffic count) kiasi cha kuihalalisha kujengwa kwa kiwango cha lami.
Barabara hii ikijengwa kwa kiwango cha lami itapunguza sana magari yanayotoka mikoani kuja sehemu za Mbezi Beach hadi Tegeta na maeneo ya Kinyerezi, Tabata, Segerea , Ukonga na Gongo la Mboto!