KERO Barabara ya Ndungu-Lugulu bado haijatengenezwa tangu mvua za mwaka 2023, Serikali iingilie kati

KERO Barabara ya Ndungu-Lugulu bado haijatengenezwa tangu mvua za mwaka 2023, Serikali iingilie kati

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

ngwanduu

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2018
Posts
621
Reaction score
478
Nikuhusu barabara ya Ndungu-Lugulu. Barabara hii, tangu iharibiwe na mvua za El Nino mwaka 2023, haijawahi kutengenezwa.

Barabara hii ni muhimu sana kwa wakazi wa kata ya Lugulu na kata ya Mtii, hasa wakati wa mavuno ya tangawizi. Kwa sasa, hakuna gari linaloweza kupita katika barabara hii.

Ombi letu ni kwa Serikali, Waziri wa Miundombinu Abdallah Hamis Ulega, na Mbunge wa Same Mashariki Anne Kilango: Wakazi wa kata hizi mbili, Lugulu na Mtii, tunaomba mtutengenezee barabara hii ili kurejesha urahisi wa usafiri na kuimarisha uchumi wa maeneo yetu, tunawaomba mtusaidie kwa haraka.
 
Nikuhusu barabara ya NDUNGU- LUGULU barabara hii tangu iharibiwe na mvua za elimino mwaka 2023 haikuwahi kutengenezwa ,barabara hii ina umuhimu sana kwawakazi wa kata ya lugulu na kata ya mtii hasa kipindi cha mavuno ya Tangawizi ,kwasasa hakuna gari inayoweza kupita katika barabara hii ,Ombi kwa serekali na waziri wa miundombinu Abdallah ulega na mbunge wasame mashariki ,Wakazi wakata hizi mbili Lugulu na mtii tunaomba mtutengenezee hii barabara.
Nahavache kaka.
 
Back
Top Bottom