KERO Barabara ya Silent Inn mpaka Freedom Lodge Sakina Arusha ni Janga

KERO Barabara ya Silent Inn mpaka Freedom Lodge Sakina Arusha ni Janga

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Barabara ya Silent Inn kuelekea kanisani Kiranyi na freedom lodge Sakina Arusha,iko kwenye hali mbaya mkandarasi aliyepewa kazi ya matengenezo anasua sua sana tangu mwaka jana ameshafanya kazi ya mitaro lakin amelundika vifusi vikubwa barabarani kiasi kwamba njia hii imeharibika pakubwa.

Tumeshawasilisha malalamiko yetu kwa viongozi lakin hakuna marekebisho yaliyofanya ya kusambaza vifusi hivi.

Njia hii inahudumia wakazi wengi kiasi kwamba nyakati za usiku na asubuhi inakuwa haipitiki kwani msongamano wa magari unakuwa mkubwa sana.

Tunaomba Halmashauri pamoja na Mkoa wafanyie kazi changamoto hii ili kuondoa adha hii inayotukabili wananchi.
 
Back
Top Bottom