Kalamu Nzito
JF-Expert Member
- Aug 13, 2015
- 349
- 805
Kange ni mtaa unaokua kwa kasi sana mkoani Tanga, wilaya ya Tanga mjini. Miaka michache mbeleni, vitega uchumi vingi vitahamia Kange kutokana na idadi ya watu wanaohamia kuongezeka kwa haraka.
Hata hivyo, wakazi wa Kange bado wana changamoto kubwa ya usafiri. Wakazi wa Kange-Kasera wamekua wakikosa huduma ya usafiri wa daladala kwa zaidi ya miezi sita (6) sasa. Hapo awali daladala zilikua zinawafikia lakini kutokana na ubovu wa barabara ambayo matengenezo yake huchukua muda mrefu, daladala zimeacha route, hasa barabara inayoelekea maduka sita,
Wananchi wanaokaa maduka sita na maeneo jirani wanalazimika kutembea umbali wa takribani kilomita moja kufuata usafiri wa daladala katika vituo vya Pembe, Kange Kituoni au Kange kwa Mmasai.
Wakati wa mvua changamoto ni kubwa zaidi na Caravat nyingi zilizowekwa hazina uwezo wa kuhimili mvua kubwa.
Kange ina viongozi wa Serikali. Naomba walione hili. Watambue thamani ya mtaa wao na wasiache aibu hii iendelee kuwatesa wananchi wa Kange-Kasera.
Nimeambatanisha picha ya eneo moja kama mfano wa maeneo mengi yenye hali mbaya. Hapo ni Kona ya tofali kuelekea maduka sita.