KERO Barabara za Mwanagati hazipitiki msimu huu wa mvua. Magari yanaharibika. Daladala zinalazimika kupandisha nauli

KERO Barabara za Mwanagati hazipitiki msimu huu wa mvua. Magari yanaharibika. Daladala zinalazimika kupandisha nauli

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Habari,

Licha ya kuwepo Malalamiko ya mara kwa mara kuhusu adha ya ubovu wa barabara Maeneo ya kuanzia Juu kidogo kwa Mpalange mpaka Kituo Cha Mwisho Mwanagati lakini hakuna hatua zinachukuliwa. Soma malalamiko Hapa

Barabara ya Maeneo haya imekuwa shida kubwa na haipitiki kwa urahisi kiasi ambacho daladala, bajaji na pikipiki wanalazimika kupandisha nauli kama fidia ya vyombo vyao vya usafiri.

Barabara hii imekuwa mbovu kwa kiasi ambacho sehemu unayoweza kusafiki dakika kumi unalazimika kusafiki muda zaidi kwa sababu magari yanalazimika kutembea taratibu sana.

Imekuwa kawaida kukuta magari na bajaji zimekwama kwenye madimbwi makubwa ya maji. Pia, imekuwa kawaida vyombo vya usafiri kukwepa njia Kuu kuingia mitaani mwa watu Ili kuyaepuka madimbwi hayo.

Mbunge wetu Jerry Silaa huoni jambo hili kweli? Mbona umekuwa unashughulikia migogoro ya ardhi lakini tatizo kubwa kama hili kwenye Jimbo lako hutaki kulitatua.

Wakazi wa Mwanagati nasi tunalipa Kodi tunaomba mtuboreshee barabara hii tuache kulalamika kila Leo.

Jamiiforums tunaomba mtusaidie kupaza sauti hii ujumbe ufike.

Hizi hapa Chini ni baadhi ya picha nilizopiga Leo. Imagine hapa mvua haijanyesha Pako hivi. Mvua ikipiga hapatamaniki zaidi.

UPDATE
- Baada ya malalamiko mengi hatimaye barabara ya Mwanagati imemwagwa vifusi na kusawazishwa



1712845504219.png

1712845525528.png

1712845569525.png

1712845590209.png

1712845628589.png

1712845645295.png

1712845741196.png

1712846349852.png

1712846424029.png

1712846572796.png

1712846632316.png

1712846765087.png

1712846999314.png


 
Hilo Jimbo la Ukonga linaongoza Kwa barabara mbovu hapa DAR.

Kutoka kivule Hadi fremukumi sitapita tena hata iweje sijawahi kuona mabwawa barabarani kama Jimbo hilo
 
Kitu pekee kinachoweza kutatua hilo tatizo ni hii👇
GK4x45RXIAABuZh.jpeg
 
Naomba barabara kutoka Banana kwenda Kitunda magole na Mwanagati ipewe kipaumbele kwenye awamu ya kwanza mpsngo wa DMDP 2.hali ni tete mno.
 
Back
Top Bottom