Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Naanza kuamini kwamba mwendokasi ulikuwa uongo mwingine wa wanasiasa, kwamba wanataka kuondoa kero za usafiri jijini kwa ajili ya wananchi. Hizi barabara zilitengenezwa kwa ajili yao kukwepa bugudha za barabara za kawaida.
Nimeona kwamba barabara za mwekasi zinatumiwa zaidi na magari ya setikali kuliko mabasi yaliyokusudiwa kusaidia wananchi.
Labda ukweli ni kwamba kuna viongozi wa serikali wanafanya makusudi kutoweka mabasi ya mwendokasi barabarani ili barabara hizi wazitumie wao na magari yao ya ST na kadhalika.
Ni kama wanajua ikiwa mabasi ya mwendokasi yatakuwa mengi, hawataweza tena kutumia barabara hizi, na hivyo kunakuwa na jitihada za makusudi kuhakikisha hakuna uendelevu wa huduma ya mabasi ya mwendokasi
Sintashangaa siku moja nikisikia serikali imetoa tamko rasmi kwamba gari za serikali sasa ni rasmi kuruhusiwa kupita barabara za mwendokasi!