SoC04 Barabara zote za Wilaya kuunganishwa na Makao Makuu ya mkoa kwa kiwango cha lami inawezekana ndani ya miaka 25

SoC04 Barabara zote za Wilaya kuunganishwa na Makao Makuu ya mkoa kwa kiwango cha lami inawezekana ndani ya miaka 25

Tanzania Tuitakayo competition threads

Aweking

New Member
Joined
Mar 10, 2019
Posts
4
Reaction score
0
Tanzania imekuwa na sera na mipango mbalimbali ya miaka kadha mbele na imepiga hatua katika hilo.

Mifano ya sera na mipango iliyofanikiwa ni
Sera ya uwepo wa shule za sekandari kata ,
Sera ya maji vijijini ,
Sera ya umeme vijijini kupitia REA,

Sasa kuna haja ya serikali kuandaa sera madhubuti kwa ajili ya kuunganisha miundo mbinu ya barabara za wilaya na makao makuu ya mkoa.

Serikali iunde wakala au kupitia TARURA ikaanda sera na mipango katika kutekeleza sera na mipango ya kuunganisha barabara zote za wilaya na makao makuu ya mkoa.

Hii itasaidia na kukukuza maendeleo ya baadhi ya vijiji ambavyo barabara hizo zitakuwa zimepita.

Pia itasaidia katika shughuli za utalii ,kilimo biashara pamoja na uwekezaji wa viwanda katika maeneo mbalimbali ya vijijini.

Serikali itapunguza gharama ya matengenezo ya barabara ambayo kila mwaka barabara hizo zinaharibiwa na mvua , maana barabara za lami hudumu zaidi ya miaka 20.

Serikali itajiongezea mapato kupitia tozo mbalimbali inayohusu usafirishaji wa malighafi pamoja biashara ya usafirishaji

Barabara hizo zitarahisishs shughuli za kijamii , pamoja na uchumi wa wananchi.

SERA NA MIPANGO
Serikali/ TARURA kutoa takwimu za barabara za wilaya zinazopewa kipaumbele katika awamu ya kwanza
Halmashauri kutenga bajeti kwa ajili ya utekelezwaji wa miradi hiyo.

Serikali kutoa ruzuku kwa kila halmashauri kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo.

Wakandarasi wa ndani kupewa kipaumbele katika kutekeleza miradi hiyo.

TANZANIA YA MIAKA 25 IJAYO NI TANZANIA INAYOFIKIKA KILA WILAYA .
 
Upvote 4
Back
Top Bottom