Barack Obama amuomboleza bibi yake kutoka Kenya kwa kuandika maneno haya

Barack Obama amuomboleza bibi yake kutoka Kenya kwa kuandika maneno haya

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289
Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amesema yeye binafsi na familia yake wanaomboleza kifo cha bibi (nyanya) yao, Sarah Ogwel Onyango Obama, ambaye anafahamika na wengi kama “Mama Sarah” lakini anayefahamika kwetu kama “Dani” au Granny.

633fd5ba-154a-4585-87a9-4bdc2de34ac7.jpeg


Katika ujumbe wake wa Twitter ulioambatana na picha yake akiwa na Mama Saraha Obama alipoitembelea Kenya kwa mara ya kwanza, Bw Obama amesema ‘’Tutammis sana, lakini tutasherehekea kwa shukran maisha yake marefu’’.

IMG_6994.jpg

Bibi wa Kambo wa Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, Sarah Obama amefariki katika hospitali nchini Kenya akiwa na umri wa miaka 99, familia yake imenukuliwa na vyombo vya habari vya nchini humo

Mama Sarah amekuwa mgonjwa kwa muda na amefariki alipokuwa akipokea matibabu.
 
Yeah kwetu hatufichi ooh mara changamoto la kupumua, mara ugonjwa wa moyo, tunaisema tu kama ilivyo maana corona sio gonjwa la aibu. Hivyo kama kweli kafa kwa corona, itasemwa tu usiwe na wasiwasi.
Yaani mpaka sasa hawajasema?Huoni kama wanaficha,manake ukitangaza kifo cha mtu,lazima useme sababu,sasa nyinyi mnasubiri nini.

Manake anazikwa leo.
 
Yeah kwetu hatufichi ooh mara changamoto la kupumua, mara ugonjwa wa moyo, tunaisema tu kama ilivyo maana corona sio gonjwa la aibu. Hivyo kama kweli kafa kwa corona, itasemwa tu usiwe na wasiwasi.


Wasife wazee sasa kila kifo ni corona, yaani bibi kama huyo mwenye mjukuu wa 64yrs afe mnamalizia tu corona hiyo.

ujinga ni mzigo mkubwa.
 
Wewe unafyatuka, wapi tumesema ni corona, nimekuambia sisi hatufichi kama mnavyofanya, ikiwa kafa kwa corona itasemwa tu.
Mkorinto ni mwehu asikusumbue. Mambo ya Obama anajibu kwa hasira . Si hii peke yake kuna Uzi mwingine huko amejaa sumu dhidi ya Obama.

Odhis *
 
Back
Top Bottom