kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Miradi na mikakati ya miradi hii iliyofeli ndani ya miaka kumi ni kielelezo tosha kwamba hatutaendelea Kama tusipoamua kujitathimini na kusimamia mambo machache.
1. Tulitumia fedha nyingi sana kwenye agenda ya Big result Now, tukanunua trektaa na vitendea kazi vingi lakini leo hii hatusikii big result now.
2. Tulitumia fedha nyingi kutoa elimu na kuwaelekeza watanzania waanzishe viwanda kwa kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda, tukaambiwa nchi yoyote inahitaji viwanda iendelee ila kwa Tanzania tumeichukua agenda hii kisiasa na siyo kitaalamu...mara paap imefungwa baada tu ya mwijage kuondolewa.
3. Mradi wa bomba la mafuta ni muhimu sana kwa Taifa ila lazima tuangalie namna yakuweka sawa mikataba ili wananchi wanaopitiwa na mradi huu wanufaike japo kwa kujenga nyumba za maana watoto wao wakue wakiuheshimu na kuulinda mradi wakitambua wanapolala ni mchango wa mradi huu...nao pia tumeuchukua kisiasa zaidi kuliko kitafiti na kimkakati.
4. Ununuzi wa ndege ni muhimu na ninapongeza, lakini soko la usafiri wa anga limeathiriwa kwa kiasi kikubwa na Corona, Kama walivyohasa watu hasa wasomi, hatuna umuhimu wakuendelea kuwekeza fedha kununua ndege Sasa, tusubiri soko lirudi mahali pazuri tutaagiza....Duniani wanunuzi wa ndege mpya kwa Sasa niwachache na viwanda vinafanyia kazi oda za zamani...tuzizungushe fedha za ndege kwenye maeneo yakimkakati tupate faida ambayo tutanunulia ndege muda ukifika.
5. Tumewekeza kwenye mradi wa kukusanya mapato hasa kwa kuwekeza kwenye teknologia ya ukusanyaji mapato, ni Jambo jema ila tatizo kubwa lililopo kwa Sasa nikuwaondoa uaskari wakusanya mapato nakuwavisha diplomasia na professionalim. Teknohama na Askari kwenye Kodi haviendi pamoja, mamlaka iwekeze kwenye vijana wenye intelligence ndani yao ambao kazi yao kubwa itakuwa kuishi kwa wafanyabiashara na kukusanya taarifa kuhusu ukwepaja Kodi,. Then wanaobainika waitwe kwa barua tu kisha wakifika mamlaka Wapewe fact za wizi waliofanya kisha wapigwe faini. Mbinu hii itawafanya wafanyabiashara kuchukua taadhari kwa sababu hawajui nani wamwamini. Ndipo Dunia ilipo Sasa.
Kinachoendelea Sasa hapa nchi ni watu kujivika mamlaka na kwenda kuwapoka watu fedha kwa njia za rushwa na usipokubali kushirikiana nao wanakutengenea zengwe unaitwa muhujumu uchumu, then from there hakuna ushahidi unaohitajika zaidi ya kukutupa ndani. Wakiona unatapa wanasema unafadhil upinzani kisha wanaanza kupambana nawewe.....tutaiua nchi kwa mbinu hizi.
6. Mradi wa mwisho uliofeli ni mradi wakurejesha imani ya wageni kuhusu usalama wa rasilimali zao wanazowekeza na wanazotaka kuwekeza hapa nchini. Huu mradi umerudisha nyuma sana maendeleo ya Taifa letu...tuwekeze kurejesha imani.
7. Tukubali kushindwa na tueleze wazi tunahitaji msaada pale tunapohitaji msaada wa maarifa, teknologia au rasilimali nyingine. Tukiri tunatengeneza mazingira ya kuwa nchi inayojitegemea na si kusema tunajitegemea.