Baraza la ardhi la kata na shauri la mirathi.

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,917
Reaction score
11,801
Nimeitwa kwenye baraza la ardhi la kata kuhusiana na shauri la mirathi, ipo hivi kuna baba yangu mdogo alikuwa anaumwa, nikampeleka hospitali akapona, baada ya kupona akaitisha kikao cha ukoo na familia akanipa shamba kama shukrani, baada ya yule mzee kufariki vijana wake wamewakataa nisilime lile shamba wakisema ni la kwao, wamenipeleka baraza la ardhi la kata, nimewaambia wale wazee kuwa shauri hili ni mirathi lakini Wamekataa na kung'ang'ania lisikilizwe pale.
Nifanyeje ndugu zangu.
 
Unao uthibitisho!
 
Mimi sidhani kama ni shauri la mirathi maana wanachokidai wao ni ardhi. Cha muhimu kwa kuwa ulipewa mbele ya kikao cha ukoo ni vema ukawaita wakiokuwepo watoe ushahidi kwamba ni kweli ulipewa shamba hilo na marehemu. Ikithibitika hivyo basi hilo shamba halitapaswa hata kuwa sehemu ya mali marehemu alizoacha kwa sababu alishakupa kabla hajafa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…