WAPEKEE_
Member
- May 23, 2024
- 21
- 28
BARAZA LA MAADILI LA TAIFA KULINDA KIZAZI KIJACHO.
Suala la maadili, ni hoja mtambuka, ni suala nyeti katika jamii lenye kubeba taswira ya aina ya jamii tuliyonayo. Maadili sio kama wengi wanavyodhani , kuwa labda ni vile kuvaa mavazi ya heshima , kusalimiana na labda mdogo na Mkubwa kuheshimiana, na kadha wa kadha. La hasha, Maadili yana gusa Kila sehemu ya mwanadamu . Kuanzia siku anazaliwa mpaka anakufa.
MAADILI NGAZI YA FAMILIA
Haya ndio maadili Mama, yenye kuandaa na kukuza KIZAZI husika. Makuzi na Malezi ndiyo yanaamua aina ya Jamii tuliyonayo.
Ni ukweli usiopunguka kuwa Mmomonyoko wa Maadili umekuwa kwa kiasi kikubwa kushuhudiwa pengine kuliko wakati wowote ule , na hii kwasababu ya MABADILIKO na MAENDELEO ya Sayansi na Teknolojia, yenye kutengeneza KIZAZI Cha kidijitali au KIZAZI Cha Dot Kom. Mwingiliano wa kitamaduni za Dunia nzima imesababisha maadili na tamaduni zetu kupotea kwa kuathiriwa na tamaduni za wenzetu.
MAADILI YA UONGOZI NA UTUMISHI WA UMMA
Ongezeko la Rushwa, Kukosekana kwa UWAJIBIKAJI, Uadilifu, Huduma Bora na Maadili kwenye UTUMISHI wa Umma yamepungua kwa Kasi Huku jamii ikiteseka kwenye umasikini Mkubwa kwa kukosa maadili na Uzalendo kwenye kuhudumia jamii.
Nchi hasa zinazoendelea , nchi Afrika na zile maskini duniani ,Moja ya changamoto kubwa ni Kukosekana kwa UWAJIBIKAJI kwa watumishi wa Umma ambao Wana dhamana ya kuhudumia jamii, na kufanya jamii zisipate maendeleo yao.
Hata hapa Tanzania pamoja na uwepo wa Wizara ya UTUMISHI wa Umma, kutoka kwenye ofisi Ya Rais, lakini bado kuna changamoto kubwa za Rushwa, UWAJIBIKAJI, Maadili, na Ukosefu wa huduma Bora kwa jamii.
BARAZA MAALUMU LA MAADILI.
Lazima tuanzishe BARAZA MAALUMU la MAADILI Tanzania. Kama kweli tunataka kuijenga kiazi KIJACHO chenye UWAJIBIKAJI na MAENDELEO, basi tuwe na chombo maalumu chenye mamlaka ya kusimamia Maadili ngazi ya Familia na Serikali. BARAZA hili litashirikiana na Taasisi za kimakakati kwenye Maadili kama vile Serikali, Asasi za Kiraia, Taasisi za dini, Taasisi za KIJAMII kama vile Viongozi wa Kimila na Desturi na Taasisi za Elimu.
BARAZA na chombo hiki hakipaswi kuwa Cha Kisiasa , katika uanzishwaji na uendeshwaji wake. Kama tunataka KULINDA jamii yetu kwa maadili ya KIJAMII na UTUMISHI wa Umma, basi Chombo hiki kiwe huru na chenye mamlaka ya dhati kwenye kusimamia Kanuni na Misingi ya maadili.
Chombo hiki kiwe kina nguvu ya KISHERIA ya KULINDA , KUWAJIBISHA, KUTETEA NA KUSIMAMIA Misingi ya maadili katika nchi.
Chombo hiki kitashiriiiana na Mahakama KULINDA Kanuni zake. Itashirikiana na Wizara Mbalimbali za msingi kama vile , Wizara ya Katiba na Sheria , Wizara ya UTUMISHI na Utawala Bora, Wizara ya Jinsia , Wanawake na watoto, Wizara ya Elimu, Bunge na Serikali kwa ujumla kulinda maslahi ya Nchi.
UWAJIBIKAJI lazima uanzie juu , kama UWAJIBIKAJI Serikalini ukiwa wenye nguvu, hata ngazi za familia na jamii zitabadilika kwasababu wahusika na watumishi wanaowakilisha jamii watasaidia kuimarisha Maadili na Uadilifu wa JAMII.
TAASISI ZA DINI.
Kwenye BARAZA hili la maadili Tanzania, litakuwa na Idara Mbalimblai ikiwemo Idara ya Taasisi za dini. Dini imebebaba zaidi ya asilimia 80% ya mfumo wa maisha ya Dunia, hivyo lazima , Idara hii iweponlatoka utendaji wa uimarishaii wa Maadili hasa kwenye ngazi ya familia na jamii.
Lazima jamii iwajibike katika maadili kwenye Taasisi za dini. Viongozi wa dini wahubiri upendo , amani na Uadilifu ili kukemea uvunjifu wa Maadili na makuzi.
TAASISI hii inawapokea WANANCHI tangu wakiwa wachanga mpaka kujua kwako, hivyo wananafasi kubwa ya kuijenga jamii Bora.
SHERIA KALI .
Kupitia Mahakama watu wawajibishwe kwa uvunjifu wa Maadili kwenye jamii na UTUMISHI wa Umma. Vifungo na faini Kali zitarudisha UWAJIBIKAJI.
VYOMBO VYA HABARI
BARAZA LA MAADILI litafanya kazi kwa karibu na kuwa na Idara ya kusimamia Vyombo vya habari kwenye masuala la maadili. Lazima vyombo vya habari viwajibike na viwajibishwe kwenye masuala ya maadili. Kwasasa vyombo vya habari vina nguvu kubwa ya kusambaza Ajenda za kimaadili na kama hakutakuwa na usimamizi basi jamii itaharibika kupitia vyombo vya habari ikiwemo Radio, Televisheni na Magazeti.
MITANDAO YA KIJAMII.
Baraza hili litaisimamia MITANDAO ya KIJAMII kwa kutoa tathmini na miongozo ya Maadili kwa watumiaji wake kwenye jamii. Mashirika ya kimataifa yamekuwa mstari wa mbele kulazimisha, mitindo na tamaduni hatarishi kwenye jamii zetu za kiafrika , lakini serikali zetu zimekuwa na uoga wa kupinga hadharani Ukosefu wa Maadili kama vile ushoga kwasababu za kidiplomasia na kiuchumi zaidi. Lakini tukiwa na Baraza hurulitakuwa na nguvu ya kupambana na vita vya nje bila kugusa masuala ya kidiplomasia na uchumi wa kimataifa.
Hivyo MITANDAO ya KIJAMII Itadhibitiwa na sio serikali, Bali chombo huru kisichoingiliwa na mamlaka za Kisiasa ili kulinda maadili ya Taifa.
SANAA NA WASANII.
Ni wazi Baraza la Sanaa La Taifa ( BASATA ) Limeshindwa kikamilifu, kuwawajibisha wasanii wanaoharibu maadili ya jamii kupitia Sanaa. Na ni kwasababu ni chombo Cha serikali , ambacho uhuru wake unategemea mitazamo ya Kisiasa zaidi. Lakini kwakweli BARAZA LA MAADILI LA TAIFA , litakuwa mwarobaini na tiba ya Mmomonyoko wa Maadili kupitia SANAA
.
MWISHO.
Tanzania na Afrika lazima tuanzishe vyombo viaivyokuwa vya Kisiasa KULINDA maslahi yake ya kiuchumi na KIJAMII kwa miaka 25 na vizazi vijavyo. Naitwa WAPEKEE KEPHAS YOHANA.
SIMU NA WHATSAPP: +255 694 024 888

Upvote
2