BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Baraza Kuu la Maaskofu wa Katoliki Kenya (KCCB) limeitaka Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuharakisha kujumlisha Kura za Urais ili kuepusha hisia mbaya zinazoweza kuzua migogoro.
Katika taarifa iliyotolewa leo Jumapili, Maaskofu hao wamesema kucheleweshwa kwa mchakato wa kujumlisha Kura kunajenga wasiwasi ambao unaweza kusababisha tetesi za mvutano zisizo za lazima na hisia kali miongoni mwa Wakenya.
KCCB imesema inapongeza juhudi na inatambua haja ya IEBC kujiridhisha kwenye mchakato huo, lakini inahimiza Tume kufanya kinachohitajika ili kuhitimisha mchakato wa Matokeo kwa wakati.
Baraza hilo pia limewataka Wagombea Urais na wafuasi wao kukubali Matokeo yoyote baada ya Tume kutangaza washindi.