HOJA Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT) mtihani wa Pre-Internship ufanyike Desemba 2026 badala ya kusubiri Aprili 2027

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Habari za kazi. Nina ombi kwa Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT).

Kwa heshima na unyenyekevu, tunaomba Baraza lizingatie uwezekano wa kufanya mtihani wa Pre-Internship kwa kundi la pili (Batch 2) mwezi Desemba 2026, badala ya kusubiri hadi Aprili 2027.

Hii itawapa fursa wahitimu ambao hawakupata nafasi ya kufanya mtihani wa tarehe 28 Oktoba 2026 na kuwasaidia kuendelea na hatua inayofuata ya taaluma yao kwa wakati.

Tunaelewa na kuheshimu taratibu za Baraza, hivyo tunaomba ombi letu lizingatiwe kwa huruma na uzito unaostahili.

Asanteni sana kwa kutusikiliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…