Baraza la Michezo la Tanzania lakana kutambua ukodishwaji wa Yanga

Baraza la Michezo la Tanzania lakana kutambua ukodishwaji wa Yanga

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Habari wanaJF,

Sasa kumekucha wapenda michezo wenzangu hii ni kufuatia Baraza la Michezo Tanzania (BMT) leo limetangaza rasmi kutotambua ukodishwaji wa Klabu ya soka ya Yanga

Baraza la BMT lasema ni kinyume na Katiba ya Klabu hiyo.

======
UPDATE:

Baraza la michezo Tanzania (BMT) limetangaza kujitambua ukodishwaji wa klabu ya Yanga kwa kuwa ni kinyume na katiba ya klabu hiyo.

Katibu mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja amesema kuwa mkataba huo kati ya Baraza la Wadhamini wa Yanga na kampuni iliyoikodi klabu hiyo, haukufuata taratibu.

"Ili Yanga iweze kubadili jina na kuitwa Yanga Yetu ni lazima ipite kwa msajili. Wao hawajaenda kwa msajili wanaanza kutangaza jina jipya. Huko ni kupinga katiba," alisema Kiganja.
 
Inaniwia vigumu kuamini kwamba katibu mkuu katoa kauli hiyo.
Ina maana hajaelewa hiyo yanga yetu ltd ni kampuni inayokodi yanga?
 
Kwani yanga imebadilishwa jina? Huyu si alikurupuka na uchaguzi wa yanga wakampiga za mbavu sasa hivi kaibuka bila hata kujua anaongelea nini kutumika huku dah
 
Huyu katibu wa BMT hajielewi timu haijabadilishwa jina .......... Yanga Yetu ni jina la kampuni ..... ni aibu kuzungumza utumbu kama huo.
 
hahaha sasa wangeiita Ndala fc ndio jina linalofahamika na msajili
 
Hizi habari zinatupoteza uelewa. Yanga yetu ni jina la kampuni inayokodi timu ya yanga au ndo jina la timu sasa hivi?
 
Back
Top Bottom