KERO Baraza la Uuguzi na Ukunga (TNMC) mtusaidie tupate Leseni mapema, fursa zinatupita Mtaani

KERO Baraza la Uuguzi na Ukunga (TNMC) mtusaidie tupate Leseni mapema, fursa zinatupita Mtaani

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ni takribanii wiki kadhaa tangu matokeo ya Mtihani wa Leseni yatoke mpaka sasa bado tunasubiri kutangaziwa siku ya kwenda kuchukua Leseni. Hili sio shida kwa sababu huenda ni Maandalizi yanafanyika kuweka mahafali hii kwa ukubwa na ufanisi zaidi, lakini, baadhi wamekuwa wakipitia changamoto kadhaa kuhusu kutafuta kazi katika taasisi mbalimbali kwa kutokuwa na Leseni.

Maana hata ukiwaonesha matokeo yako baadhi ya Waajiri kuwa umefaulu bado hawana haja na wewe mpaka waone Leseni, hivyo, wamekuwa wakipitia changamoto kadhaa ikiwemo kukosa nafasi hizo.

Nilikuwa natamani japo mngeruhusu katika mifumo ya TNMCI ili waonekane tayari ni ALLOWED TO PRACTICE ili japo wawe na cha kujitetea pindi wanapojitafutia nafasi hizo katika sehemu mbalimbali.

Majibu ya TNMCI soma hapa ~ Baraza la Uuguzi na Ukunga (TNMC): Wahitimu wanaosubiri Leseni wawe watulivu, tupo kwenye mchakato
 
Back
Top Bottom