Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Nimeona picha ya Baraza la Wazee wa TANU hapo juu.
Picha hii mimi ndiye niliye ‘’digitise’’ miaka ya mwanzoni 2000 na kuiweka mtandaoni kwa kila mtu aione ikiwa ushahidi wa mchango wa wazee wetu katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Hii ni moja katika picha adimu sana zinazomuonyesha Julius Nyerere Rais wa TANU akiwa na wazee wetu wakati wa kupigania uhuru.
Lakini wanaostahili kushukuriwa kwa kuweka kumbukumbu hii ni ukoo wa Mzee Jumbe Tambaza.
Nimejitahidi sana kupata picha za namna hii zilizopigwa miaka ile ya mwanzo ya TANU kutoka Maktaba ya iliyokuwa Tanganyika Standard lakini nilifahamishwa kuwa inahitajika kibali maalum.
Abdallah Tambaza ni rafiki yangu toka utoto wetu na siku moja nilimuomba anisadie nipate kuona nyaraka zozote zile ambazo zipo katika mikono ya ukoo wao.
Abdallah akanipeleka kwa ndugu yake anaitwa Msakala Mohamed Jumbe Tambaza anaishi Kinondoni si mbali ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
Msakala akatukaribisha katika ukumbi mzuri uliokuwa na makochi mazuri ya kupendeza.
Baada ya kusalimiana Abdallah akanitambulisha kwa Bwana Msakala na kumueleza shida yangu.
‘’Ninazo picha za marehemu babu Jumbe Tambaza nyingi tu nitakuonyesha lakini nyaraka zake itabidi unipe muda nizitafute kuna nyaraka muhimu sana ya kesi ya makaburi yetu yalipotaka kuchimbuliwa wakati wa ukoloni ili ijengwe barabara kutoka Mwembe Togwa kwenda Salender Bridge, hizi itabidi unipe muda nizitafute.’’
Nilisisimkwa kwa kusikia kisa cha kuchimbuliwa makaburi ya Tambaza, hii ni historia ambayo mara nyingi sisi tukiwa wadogo tuliwasikia wazee wetu wakihadithia kuhusu ugomvi kati ya Waingereza na Waislam kwa kutaka kuchimbua makaburi ili wapitishe barabara na kesi ilifika hadi mahakamani na katika masheikh wakubwa wa nyakati zile waliotakiwa kutoa fatwa alikuwa Sheikh Abdallah Saleh Farsi kutoka Zanzibar.
Mwalimu wangu Mzee Kissinger alipata kunipa mhadhara mzima kuhusu sakata hii ambayo ilipelekea migongano mikubwa baina ya masheikh wa hapa Dar es Salaam mmoja wao aliyehusika sana katika mgogoro huu akiwa Sheikh Hashl bin Hemed mwanafunzi wa Sheikh Idrissa bin Sa’ad.
Msakala akaniletea picha nyingi na katika picha ambayo iniligusa sana ni hiyo hapo chini ambayo inamuonesha Julius Nyerere akiwa na Baraza la Wazee wa TANU ambae mwenyekiti wa baraza hili alikuwa Sheikh Suleiman Takadir.
Picha hii iliipigwa mwezi August, 1957 katika harakati za kutoka taarifa ya Tanganyika mbele ya Ujumbe wa UNO kuhusu nchi zilizokuwa chini ya Udhamini wa Uingereza.
Naweka picha hii tena hapo chini kama ilivyo katika kitabu cha Saadan Abdu Kandoro, ‘’Mwito wa Uhuru,’’ (1961).
Ikiwa huwajui watu hawa wewe utaona watu tu ndani ya kanzu na kofia lakini ikiwa utawajua hapo ndipo utakapotuliza moyo wako kwani kila mmoja katika hao ana historia yake kubwa na ya kutukuka katika kuijenga TANU, kumuunga Nyerere mkono na kupigania uhuru wa Tanganyika.
Kwa kuwataja wachache, kuanzia, Jumbe Tambaza, Mshume Kiyate, Mwinjuma Mwinyikambi, Sheikh Issa Nassir, Sheikh Salum Subeti orodha ni ndefu kwani baraza lilikuwa na wajumbe 120 na zaidi kidogo.
Picha ya kwanza Baraza la Wazee wa TANU, Mzee Jumbe Tambaza, Kitabu cha Saadan Abdul Kandoro ''Mwito wa Uhuru,'' (1961), Baraza la wazee wa TANU ndani ya kitabu cha Kandoro na picha ambayo ina vijana wanane na kati ya hawa watano wazee wao walihusika moja kwa moja mstari wa mbele katika TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika: Kulia: Mohamed Said, Yusuf Zialor, Kleist Sykes, Bubby Bokhari, Abdallah Tambaza waliochutama Abdul Mtemvu, Wendo Mwapachu na Kessy 1967.