Barbara Gonzalez: Simba SC haijawahi kumuhitaji Manyama

denooJ

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2020
Posts
18,509
Reaction score
68,228
Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba SC Barbara amezipuuza ripoti zinazodai Simba imezidiwa ujanja na Azam kwa kumsajili beki Manyama kutokea Ruvu Shooting.

Barbara amesema Simba haijawahi kufanya mazungumzo na timu yake au mchezaji mwenyewe kwa sababu hawajawahi kumuhitaji na hakuwepo kwenye mipango yao.

NOTE:
Ni vigumu sana Simba SC kushindwa kumpata mchezaji yeyote inayemuhitaji hapa Tanzania kutokana na uwezo wake kiuchumi, na mafanikio waliyofikia miaka ya karibuni uwanjani kwenye mashindano ya CAF, hivyo hii taarifa ya Barbara naiamini 100%
 
Kwenye uzi huu watajaa watu wa yanga wakijifariji kuwa Simba imezidiwa ujanja na Azam .

Swali dogo tu ni mchezaj gani kwa hapa tz asitake kucheza Simba kwa sasa?

Taarifa zenyew za manyama zilitoka kwa wachambuzi wa mpira makanjanja ambao kazi yao ni kumpa thaman mchezaj wao maana bila kuitaja Simba mchezaj hawezi kuwa na thaman kubwa kiivo ,so acha waendelee kuitumia simba ili wapate busta.

Mpaka Sasa hakuna anayejua habar za usajil wa Simba Zaid ya kuruka ruka na kuokoteza habar ,CEO kasema hawajawah kumtaka manyama, mtu mwingine anakuja et wamezidiwa ujanja na Azam ,mara sizitak mbichi izi ,acheni kelele za kipuuz mnapenda kujifariji kwenye vitu vidogo sana linapokuja swala la ubingwa mnaanza kulia lia ,Sasa manyama ni kitu gani kwa Simba ,kwahiyo manyama ndie analeta ubingwa? Mbona jk ruvu ametoka patupu bila ubingwa huyo manyama kama ana maajab sana kwenye mpira.achen kelele tukutane uwanjan
 
Wachambuzi wa bongo wajanja sana, yaani saivi kila taarifa lazima wahusishe simba, saivi naona wameanza kwa kibu denis, mara ooh yanga na simba wanamgombania, hapo yanga akisajili utasikia simba kazidiwa mabavu!!

Sasa jamani mtu kama kibu atacheza namba ipi pale simba? Manyama mwenyewe angecheza namba ipi pale simba, kiufupi simba kwa sasa , wanatakiwa watengeneze vijana wengi kwa ajili ya baadae! Sioni mchezaji hapa bongo anaeweza kucheza pale simba
 
Si kuna Uzi humu mlileta wenyewe mnaojua mambo ya mpira wa Tanzania mkammwagia sifa kama zote japokuwa sikumbuki Uzi ulipandishwa na nani lakini miongoni mwa supporters wakubwa ni wewe denooJ, vipi tena Msumali huoooo!
 
Wachambuzi wa bongo wajanja sana, yaani saivi kila taarifa lazima wahusishe simba, saivi naona wameanza kwa kibu denis, mara ooh yanga na simba wanamgombania./.
Football lazima awaguse Simba Ila music ni lazima wamguse Diamond a.k.a Simba 😁😁😁😁

Habari ya mjini hiyo. Huwezi kumgusa Kibaa na Utoooo Wala huwezi uza habari yako hapa bongo
 
Si kuna Uzi humu mlileta wenyewe mnaojua mambo ya mpira wa Tanzania mkammwagia sifa kama zote japokuwa sikumbuki Uzi ulipandishwa na nani lakini miongoni mwa supporters wakubwa ni wewe denooJ, vipi tena Msumali huoooo!
Sijawahi leta uzi wa aina hiyo, kama unao weka hapa kila mmoja ajionee, mimi huyo Manyama nilikuwa hata simjui anachezea timu gani, ndio nikaambiwa yuko Ruvu Shooting.
 
Sijawahi leta uzi wa aina hiyo, kama unao weka hapa kila mmoja ajionee, mimi huyo Manyama nilikuwa hata simjui anachezea timu gani, ndio nikaambiwa yuko Ruvu Shooting.
Uzi hukuuleta wewe lakini kuna shabiki aliupandisha na mkamuunga mkono sikumbuki ni nani ngoja niutafute!
 
Hata Manyama angekuwa mjinga kwenda anapojua hatapata namba
 
Kuna uzi huko Facebook nimeona unadai Riport ya Kocha Gomes inataka wachezaji wapya wawili tu tena Wakigeni.

Hakuna ingizo jipya la mchezaji wa ndani.
 
Kuna uzi huko Facebook nimeona unadai Riport ya Kocha Gomes inataka wachezaji wapya wawili tu tena Wakigeni.

Hakuna ingizo jipya la mchezaji wa ndani.
Waongo hao, wewe waulize source ya hiyo report ni wapi au ni nani? Hawanaga chanzo zaidi ya kutunga tu!!
 
Waongo hao, wewe waulize source ya hiyo report ni wapi au ni nani? Hawanaga chanzo zaidi ya kutunga tu!!
Ni kweli hapa Bongo tuna utamaduni wetu wa kuhabarisha watu vitu vya tetesi. Hata Magazeti ya Michezo yote kilasiku yana andika vitu vya uongo.

Mara utasikia Haji Manara alizimia mara tatu kule Sauzi. Kesho utasikia Ajib kashasaini Yanga kumbe ushuzi mtupu.
 
Simba ilishindwa kwa Mwamnyeto, na Sasa imeshindwa kwa Manyama.kunasiku Zaka za kazi alimwambia Magori kwamba hakuna mchezaji yoyote ambayo watamtaka alafu Simba iwashinde katika ku msain.
Akampa mfano wa Chikwende kwamba mchezaji mwenyewe alitamani kwenda Azam lakin kocha Lwandamina alimkataa wao Simba wakamsainisha tena kwa fedha nyingi.
Simba imeshindwa tena kwa Djuma Shabani. Huwezi kutambia fedha za familia ya MO wakati maamuzi ya matumizi mbaka wanafamily wakae.
 
She is right
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…