Barcelona yaishitaki PSG usajili wa Messi

Barcelona yaishitaki PSG usajili wa Messi

BigBro

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
3,585
Reaction score
11,601
Barcelona yafungua kesi Mahakami kupinga usajili wa Lionel Messi kujiunga na PSG, wakidai klabu hiyo haiwezi kumsajili mchezaji huyo kutokana na rekodi mbaya ya mapata na matumizi ya klabu hiyo, ambapo wanaamini wakifanya hivyo watavunja kanuni ya Financial Fair Play.

Mawakili wa Barcelona wamewasilisha malalamiko kwenye Mahakama ya Rufaa barani ulaya wakitaka PSG izuiliwe kufanya usajili wa Lionel Messi kutokana na takwimu za kiuchumi, kwa sasa Messi ni mchezaji huru na imeripotiwa kuwa mchezaji huyo bora wa Dunia mara 6 yupo kwenye hatua za mwisho za kujiunga na PSG.

Kwa mujibu wa malalamiko yaliyowasilishwa na Barcelona yanadai kwamba hali ya matumizi ya pesa ya PSG ni mabaya zaidi ukilinganisha na klabu yao, hivyo wanaamini PSG hawastahili kumsajili Messi kwa sababu watavunja kanuni ya (Financial fair Play) kanuni hii inavitaka vilabu barani ulaya vitumie pesa kulingana na kiwango cha pesa halali walizoingiza kutokana na shughuli za mpira.

Ripoti za mishahara ya PSG kwa msimu wa 2019-20 zinaonyesha kuwa wastani wa mishara ya wachezaji wa klabu hiyo ilikuwa imefikia asilimia 99% wakati FC Barcelona wastani wao ulikuwa ni asilimia 54 % na sasa inaaminika endapo kama PSG wakimsajili Messi basi watakuwa wamevunja kannuni hiyo kwani matumizi yao yatakuwa yamezidi kipato chao.

Barcelona wameshindwa kumpa La Purga mkataba mpya kwa sababu ya kanuni hiyo ya Finacial Fair Play, inaonyesha endapo kama mchezaji huyo angesaini mkataba mpya basi kiwango cha matumizi kwenye mshahara kingefika asilimia 110% na wangekuwa wamevunja kanuni hiyo kitu ambacho ni kinyume na kanuni za mapato na matumizi kwa vilabu barani Ulaya.
 
Barca wanaleta umama sasa, magine Perez nae angie kwenye harakati za kumtaka Messi watasema tu "teh teh[emoji16] tulikuwa tunatania PSG ndo klabu tuliyotaka Messi aende[emoji120][emoji24]"
 
  • Kicheko
Reactions: BAK
Barca wanaleta umama sasa, magine Perez nae angie kwenye harakati za kumtaka Messi watasema tu "teh teh[emoji16] tulikuwa tunatania PSG ndo klabu tuliyotaka Messi aende[emoji120][emoji24]"
Pérez anaomba usiku na mchana PSG Wamsajili Messi ili yeye aweze kumsajili Mbape, kwasababu anajua ili wa balance account zao ni lazima wamtoe mchezaji mkubwa na Mbape amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake so wanaweza kuona kuliko wamwachie aondoke kama free agent mwakani ni bora wakachukua tu pesa msimu huu.
 
Mnaonaje hi sheria ije bongo?
Bongo bado ligi yetu ni ya mchangani, wewe ulishaona team zetu zinafanya vipimo vya afya kwa wachezaji wake wapya ama kupima wakati wamerudi kambini kwa ajili na pre season?
 
Aende Wandamentropolitano akapige ndimu pale. Luiz Suarez ni mshkaji wake na el cholo ni mtu wake wakaribu.
La pulga abaki spain aendelee kuipendezesha la liga santander.
 
Barcelona nao wana kawivu

Nimeipenda sana hiyo avatar yako kamanda, huyo alikuwa ni mzee wa kazi, hana maskhara akiwa na mpira...ana world cup moja, magoli 289 katika mechi 425 alizocheza..(1973-2013)
1973–2013Argentina425(289)

YearsTeamApps(Gls)
1973–1978Boca Juniors189(132)
1978–1986Sevilla96(83)
1986–1993Instituto53(31)
1993–1998Real Madrid72(46)
1998–2005Barcelona89(32)
2005–2010Boca Juniors21(9)
2010–2014Hércules66(35)
2014–2015Kresmer SC6(3)
2016–2018Estudiantes[disambiguation needed]0(0)

Rekodi zake zimeenda shule kamanda.
 
Back
Top Bottom