chuo utapata ila uwe tayari hata kujaza vyuo vyenye ada kubwa maana bodi ya mikopo wameweka fixed rates za ada kwa kozi za ualimu hivyo vyuo vyenye ada ndogo kama SAUT na UDOM competition itakuwa kubwa. Mfano SAUT Ada yao ni sh. 950,000 wakati bodi watamlipia mwanafunzi sh. 475,000 tu hivyo mwanafunzi atalazimika kutop up sh 475,000. Lakini kwa vyuo kama Tumaini, TEKU, Makumila, nk ambavyo ada zao zipo juu nadhani nafasi zitapatikana kirahisi. Mfano Tumain ada yao ni sh. 2,300,000 kwa kozi ya BAED na bodi ya mkopo italipa sh. 500,000 tu hivyo mwanafunzi atalazimika kutop up sh. 1,800,000 ambazo ni hela nyingi sana. Kwa mtu ambaye hana uwezo kwa vyovyote vile atakimbilia kujaza SAUT kuliko Tumain. Hivyo kama uwezo wako wa kifedha ni mzuri kuwa strategic kwa kuangalia vyuo ambavyo competition itakuwa ndogo