Mkuu benki ziko nyingi na zingine wala hazichukui muda kiasi hicho kufungua ama kufunga account. Au una agenda iliyofichika ambayo nao Barclays wameishtukia na wanaifanyia kazi? Watchout!
Bank zote zimeorodhesha masharti yake yote ya kujiunga kwenye karatasi kutegemeana na ni aina gani ya account unataka kufungua.
Zamani zamani wewe unajua una ishu sio Barkclays tuu, benki yoyote itakushtukia na siajabu hiyo cheque ikakudodea.
1. Unalipwaje kwa Cheque wakati huna account?.
2. Eti ni ya ki NGO, hii ndio account ngumu kufungua kuliko zote, lazima upeleke hati ya usajili maana NGO hazilipi kodi.
3. Hayo uliyajua, ndio mana ukataka kupenyeza rupia.
4. Inaonekana hiyo pesa imetoka nje kama imezidi!! Sh.10,000,000 benki yoyote haipokei cheki hiyo bila kupitia BOT kufanya authenticity ya ziliko toka hizo fedha.
5. Naamini aliyewalipa kabla haandika cheque, aliwaomba bank code ili afanye direct transifer, kwa vile huna account, na shida yako ni pesa, ukamconvince aandike cheque.
Tunaomba ukifanikiwa popote kufungua account na kudeposit hiyo hela na ikaclear tujulishe ili nasi tupitishie hiyo benki fedha zetu maana itakuwa ni laundry !.