Barnaba: Diamond sio Mwanamuziki

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
1,016
Reaction score
2,195


Jana, Wakati akihojiwa na Mwanadada Shadee kwenye Kipindi cha Clouds E cha Clouds TV, Msanii 'Fundi wa Muziki' kutoka nyumba ya vipaji THT, Barnaba Elias 'Barnaba', pamoja na mambo mengi aliyozungumzia, alitoa maelezo kuhusu wasanii watano anaowakubali na sifa zao Kimuziki ambapo alimtaja Msanii wa BongoFleva Diamond Platnumz kuwa sio 'Mwanamuziki' mwenye kujua kuimba muziki kiufundi.

Akifafanua kauli yake kwa mapana , Barnaba alieleza kwamba Diamond hajui kuimba kufuatana na alama zote muhimu za muziki, bali hutumia mtindo flani wa kuimba 'kiujanja', mtindo ambao kwa wanaojua kuimba muziki technically huwa wanautumia pale wanapofeli kufuata kanuni za uimbaji wakati wakiimba.

Hata hivyo, alimsifia kwa kuwa 'mjanja' na kuweza kufanya muziki wake kuvutia na kuleta ladha.

Orodha ya wasanii ambao aliwatolea maoni na kusema ni wasanii anaowakubali sana ni pamoja na, Diamond, Ally Kiba, Ditto, Amini na yeye mwenyewe.
 
Diamond mimi namuona ni mtunzi mzuri wa nyimbo, pamoja na kushambulia jukwaa, lakini kuimba kwa kweli sio kiviile. Ukitaka kujua Diamond ni wa kawaida kwenye uimbaji sikiliza wimbo wake wa "Ukimuona" jinsi ulivyoimbwa na Christan Bella, ule wa kwake original hamna kitu.
 
Mbona yuko sahihi kabisa. wala hakuuna kejeli hapo,, kaongea kitaalamu. kuweza kuimba haimaanishi ni kuwa mwanamuziki. wasanii wengi wa bongo wanaimba tu lakini si wanamuziki.
 
Mimi bado S ijaelewa mwanamuziki ni yule anayejua kuimba kwa noten if my spelling is correct au yule mwenye sauti Nzuri hata kama ni cabbo snoppy yule chizi wa Angola.?
 
Inawezekana jamaa aliongea kwa nia njema tu, ila inatengenezewa mazingira ieleweke kivingine.

Diamond anapigwa vita kinoma adondoke, tusichojua wabongo ni kuwa mshkaji akidondoka tunadondoka pia sisi. Chalii ametuweka kwenye ramani ya muziki ambayo hatukuifikiria kwa miaka ya karibuni kwa juhudi zake, ila sisi badala ya kum-support ndio kwanza tunampiga mawe hatari. Kuna nchi kibao hapa Africa kitu kizuri pekee wanachojua kutoka bongo ni Diamond na ushiriki wetu Big brother.

Binafsi dogo siuelewi muziki wala pozi zake, ila kila nikiskia kapiga hatua flani nafarijika kama Mtanzania na namuheshimu.

Ila sio issue, tumshushe tu halafu tuanze upya kuwapandisha tunaowapenda, tukishindwa tuanze kulaumu jinsi Nigeria walivyo-dominate game, si ndio zetu.
 
Diamond ni msanii anaejua kufakamia jukwaa tu
 
namuunga mkono barnaba pale kwa chibu hakuna mziki ndio nilisema juzi kuwa anabebwa na mapromo tu watu wakanishambulia hatari,nikasema aende kwa KIBA afundishwe mziki bado nikashambuliwa haya sasa barnaba nae kasema mshambulieni nae
 
Mwaka huu mondi hapati tuzo kilimanjaro, chezea wabongo wasivyopenda mashauzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…