Barrick Gold mining license renewed for 15 years

cha ajabu Kamati ya Bunge na hata

wanasiasa opportunist habari wataipatia hapa
 
Ni sababu mojawapo, pamoja na zingine ambazo wawekezaji hulia nazo kama

Miundombinu ya barabara Vs Treni, upatikanaji wa maji kwa ajili ya shughuli za uchimbaji, urasimu kwenye taratibu za vibali serikalini, upatikanani rahisi wavitendea kazi vingine na nyingine nyiiingi tu.

Lakini, punguzo wanalopewa linalingana na vigezo??

Hivi unikute mie dukani kwangu, unatanunua nguo ila bahati mbaya imetoka kifungo, hivi kweli nikupunguzie bei kwa 75%? Nafanya biashara ya faida ama nacheza?

Ningekuwa na uwezo ningewashauri wanabodi wote walau tuteue siku moja tujadili suala la umeme. Ni muhimu sana. Uchimbaji unategemea umeme leo wewe unaona umeme haina umuhimu kwenye kulilia discount
 
Haya ni matokeo ya ile safari ya Canada na mkokoteni wa Farasi,hata Muhongo alikuwepo kwenye ile trip...
 
Umiliki wao wa vitalu kwa maana ya terms and conditions za mkataba?Database ya umiliki wa vitalu inayolipiwa dola 100 ili kuweza kuiona ina information gani usefull?Wewe unadhani hizo taarifa zitaelewekaje kama zikipatikana,whats in the details?
 
Yale yale!

Unakubaliana na Zitto mikataba iwekwe wazi halafu unauliza "is this the real solution?"..."ikiwekwa wazi tutazuia vipi....?" Wewe ndio unakubaliana nae halafu huelewi kwa nini unakubaliana nae! Doesn't make any sense...
Any fool can know,the point is to understand!
 
sie ni wakuibiwa tu mpaka tupate akili. Huku mtaani bado sana. sijui lini tutatafika.
 

Mkuu BAK huyu waziri kiukweli anayo nia njema sana ya kuleta mabadiliko pale wizarani kwa manufaa ya taifa lakini nahisi bosi wake anamuwekea mizengwe. Kama utakumbuka pia alikaririwa akisema kuwa mikataba ya gesi yote inabidi ipitiwe upya kwa manufaa ya taifa, lakini cha kushangaza siku chache baadaye katibu wake mkuu akasema watu hawakumwelewa vizuri waziri na serikali haina mpango wa kupitia mikataa hiyo (wanatufanya sisi wajinga kweli). Sasa ukiangalia kwa undani hapa unaona kuwa kulikuwa na agizo toka juu la kukanusha kauli hiyo ya waziri in favour of the so called wawekezaji (majangili wa mali zetu). Pia Muhongo alishaanza kuwatemea cheche Symbion kuhusu mabilioni wanayolipwa lakini baadaye katulizwa na wakubwa wake. Kwa kifupi JK na CCM yake ni janga la kitaifa.
 
Reactions: BAK
What next? The way forward pleaseee...mie nishachoka na manunguniko plus lawama za kila siku za watz...niambieni tufanye nini sasa?

Next ni Watanzania kuacha kunung'unika na kuchukua maamuzi kwa faida ya vizazi vijavyo.

Maamuzi hayo yanakuja na risks. Ndizo hizi risks ambazo Watanzania wengi wanaziogopa.

Wanaziogopa kwa sababu they have not tried them, though kwa wenzetu ni vitu normal.
 
Uzi waenye tija kwa nchi yetu kama huu huwezi waona wakina , nchemba, nape, na vijana wake wa lumumba, au tutentemeke....
Nchi imekwisha tunaingalia tu!!
Nini kifanyike??

Siyo nini kifanyike, bali wewe ufanye nini?
 
Hebu niulize, tulitaka wanyimwe?
Kwa kutumia sheria na taratibu zipi??

Si sheria za mikataba? Kwani mie na wewe tukiingia kwenye mkataba halafu ukiisha, utanilazimisha tu-renew?

Unless kama kwenye mkataba wa awali tulikubaliana kuwa ukiisha lazima tu-renew tena under the same terms and conditions.

But ina maana tokea mwaka 2000 there was no any changes of circumstances to afffecting the original terms of the license?
 
Mkuu rmashauri unachosema kinawezekana kabisa kikawa kwamba pingamizi kubwa la Wizara ya Nishati na Madini kufanya vizuri ni DHAIFU. Kutokana na mizengwe (labda ni shareholder mkubwa sana) yake pale wizarani ikiwemo mikataba ya gesi na uchimbaji wa madini kama hawa watendaji wanaona DHAIFU ndiye anayekwamisha juhudi zao za kuhakikisha Tanzania inafaidika kwa kiwango cha juu kutokana na gesi na madini mbali mbali yanayopatikana nchini, kwanini wasimlipue na kuanika uozo wote wanaouona ambao unasababisha hali hii miaka nenda miaka rudi hadharani? Tuliambiwa huy jamaa ni kichwa sana. Na mara baada ya kuchaguliwa akatoa kauli ambazo wengi tulizifurahia na kuona kwamba sasa pale nishati na madini kapatikana mkombozi machapa kazi ambaye atahakikisha vilio vya Watanzania vinafanyiwa kazi. Sasa ameanza kutoa kauli fyongo ambazo zinapingana na kauli zake za nyuma na hivyo kutokuwepo na tofauti yoyote tangu alipoteuliwa na wakati wa Ngeleja. Muhongo mchapa kazi amepotelea wapi!? au naye kishashikishwa kitu chake ameamua kuunga behewa kwa DHAIFU!?

 
Unless kama kwenye mkataba wa awali tulikubaliana kuwa ukiisha lazima tu-renew tena under the same terms and conditions.
Basi ni bora huo mkataba wako ungesema "huu mkataba ni wa milele, hauna mwisho"! Kuna maana gani ya kuwa na termination clause iwapo mkataba lazima uongezwe kila unapoisha? No such thing in contracts.
 
Basi ni bora huo mkataba wako ungesema "huu mkataba ni wa milele, hauna mwisho"! Kuna maana gani ya kuwa na termination clause iwapo mkataba lazima uongezwe kila unapoisha? No such thing in contracts.

Unaposema kuwa "no such thing in contracts" unaonyesha kuwa you don't even know about the law of contract.

You seem to think that contracts are regulated by public law.

Mkataba ni baina ya pande mbili. Mnaweza kukubaliana kuwa kusiwe na termiantion clause.

Pia mnaweza kukubaliana mkataba uongezwe on the same terms kama ukiisha.

Kama ukiingia kwenye mkataba wenye terms mbovu kama hizo the law will not protect you.
 


Since the issue of the original SML 12 years ago, the mine had produced over 2-million ounces of gold and had a further 3.5-million ounces of gold remaining in reserves.

Duuh.. Imewachukua miaka 12 kuchimba 2 million ounces.. Wamepewa another 15 years kumalizia hiyo reserve ya 3.5 million ounces iliyobakia..! Baada ya hapo tutabaki na mashimo yetu kama mahandaki.. Najaribu kujiuliza kitu gani ambacho kitaweza kuwa kama halalisho hapo baadae kwa kukubali madini ambayo Mwenyezi Mungu kwa makusudi aliyaweka kwenye nchi yetu kuja kuchimbwa na kuchukuliwa..! Itakuwa ni miundo mbinu..? Viwanda..? Shule.. vyuo na mahospitali kwa viwango vya ubora vinavyofanana na thamani ya madini yetu..? So far cijaona any of it..!

Damn.. We'r doomed meeeen..!
 
Subiri watauzia Wachina huo mgodi.

Hapo ndo kitakapokuwapo kilio na kusaga meno..

Wachina ndio wamekuwa wezi ciku hizi kuliko.. Yaani wameharibika kwanza wanaongoza kwa kutoa rushwa.. Halafu ni mabingwa wa kuwapunja wafanyakazi wazawa..! China ya Mao iliosheheni maadili imeshakufa..
 
unaonyesha kuwa you don't even know about the law of contract.
Sasa unapoteza staha. Kisa, umekosolewa, unataka kupachafua hapa.

Mkataba ni baina ya pande mbili.
Not necessarily, mkataba si lazima uwe kati ya pande mbili. Unapotumia lugha za "hata hujui kuhusu the law of contracts" hakikisha na wewe huchemki chemki, you don't want to be dubbed a bush lawyer!

Mnaweza kukubaliana kuwa kusiwe na termiantion clause.

Pia mnaweza kukubaliana mkataba uongezwe on the same terms kama ukiisha.
Hujasema chochote kuhusu hoja yangu. Narudia: Unaposema watu wanaweza kukubaliana kwamba "mkataba huu ukiisha ni lazima uongezwe" hauleti maana. Kutakuwa na maana gani kuuwekee mkataba muda wa kuisha kama ukiisha ni lazima uongezwe? You are just not making any sense, hakuna kitu kama hicho kwenye mikataba!

Nimetofautiana na wewe, ukaleta kashfa, sasa kaa mkao wa kupata shule. Mkataba ni makubaliano huria yanayotambulika kisheria, lakini hamuwezi kujiamulia kukubaliana chochote kile, kwa sababu kuu mbili. Moja, kuna vitu vingine ni kinyume cha sheria kukubaliana, kwa mfano, mkataba wa kupangisha nyumba kwa matumizi ya biashara ya danguro ni mkataba haramu.

Sababu ya pili, kwa kuwa mkataba ni makubaliano ambayo yanatambulika kisheria, sheria ya mikataba inaweka misingi ya makubaliano ambayo yatalindwa na sheria, na hivyo mkijiamulia amulia kukubaliana mambo bila kufuata misingi hiyo mtatoka patupu. Kwa mfano, baadhi ya mikataba lazima iandikwe, kama vile mikataba ya fungo. Msingi mwingine, mkiandikiana vitu ambavyo havieleweki eleweki, havi make sense, basi makubaliano hayo ni batili. Msingi huo umeanishwa katika sura ya 345 ya sheria ya Tanzania, ibara ya 29.

Unaposema, kwa mfano, "mkataba huu ukiisha lazima uongezwe" haueleweki,
hakuna lawyer worth his name ataandika termination clause kama hiyo. Kurahisisha mambo, bora ungesema "mkataba huu utakuwepo mpaka kiama kitasimama," tujue moja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…