Barrick Gold wants tax refund from Tanzania Government!

Kipindi cha Nyerere bora yeye alijenga makambi ya majeshi juu ya haya madini mpaka pale vijana wataifa la kesho wajue ulimu yake na kuya toa huko. Sasa wasomi wameongezeka mbona tena tunabolonga tu hivihivi. Unakuta mtu amesoma accounting wee mpaka cpa ndo anataka awe ndiye anashuulikia madini kwavile inalipa alafu anawazibia wale waliosomea madini na degree zao ndo hapo wanaingia mikataba hewa.hawajui hili wala lile kuhusu madini. Ni sawasawa unamwambia lawyer afanye operesheni ya apendexi unajua matokeyo yatakuwaje atatoa mpaka utumbo na ashonee vitu vingine huko ndani. Ndo hawa wakuu wetu wanapeana mahali pa kula bila elimu za mambo wanayoingilia alafu tunapata madili hewa. Mtu anapewa repory ina kurasa 20 ye anaenda ya mwisho na kuweka sahihi tuu kwisha kazi manake hajui kinachoongelewa ndani lugha kama ya madini na vipimo vyake. Kwa hii yeye mkuu anaenda tu page ya mwisho na kuweka sahini yake. Mwishoni mwa siku unaambiwa unatakiwa ulipe mamia ya mamilioni si uliweka sahii hata hawajui walitakiwa walipe.
 
Hizi post zingine jamani!!! siku yangu ilianza vizuri lakini imekwisha haribika sijui nini kimenifanya niifungue maana jana niliipotezea ili nisiharibu mapumziko yangu
 

Hakuna cha kukosea hapo mkuu, kila sheria ukiona inatugwa au mkataba kusainiwa, usanii wote unakua ulishatengenezwa tokea mapema. Walijua haya yatatokea fika na ndiko wanakofaidia wenyewe CCM
 
Yaani hasira nilizo nazo naomba musienelee kuongea maana mi naweza kurukia mtu hapa nikaua.
 
Tax refund????? hii mbona inataka kufanana tena na malipo ya Dowans jamani?. Kuna tatizo kubwa la mikataba ambayo serikali inaingia na kuifanya kudaiwa mabilioni ya fedha ambazo zingeweza kufanya shughuli nyingi za kimaendeleo.

Pia ninaiona hii kama dili ya serikali na hawa jamaa ya kuchota fedha za serikali kulipia madeni ya wakati wa uchaguzi pamoja na kugharamia uendeshaji wa CCM. Kwa hiyo ndugu zangu msishangae huu ukawa ufisadi mwingine wa kutisha ambao lazima wapenda nchi na wanaharakati wahakikishe wanavalia njuga.
 
Here we go again .....Ngeleja & Co. mpoooo?
 
hatuna haja ya kuendelea kuwapa msamaha wa kodi kwani wao wanapata 97% ya mapato wakati nchi inapata 3% tu, huoni huo ni unyanyaji wa wazi wa hawa mabeberu? lazima tubadilike na kuitetea nchi yetu kwa dhati. tumechoka kuwa ombaomba kwenye nchi yetu wakati tunazo rasilimali ambazo zinaweza kutuletea maisha bora. Lazima kwani hawa jamaa wanaendelee kupata msamaha wa kodi na kutunyonya kumbuka wakati ulipoingiwa mkataba bei ya carret moja ilikuwa $ 240 lakini sasa ni zaidi ya $1,200 huoni huo unyonyaji, wakati wanapata faidi zaidi ya 400% HII NI BIASHARA KICHAA. Watanzania tuamke na kuwaondoa hawa mafisadi ndio maana Mwl. Nyerere aliwakataa na wakasubiri mpaka baada ya kefo cha Mwl ndio wakaja na mikataba km ya Chief Mangungu wa Msowelo!! WATANZANIA NI WAKATI WA KUAMKA NA KUPINGA HUU UFISADI

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Hii nchi ya ajabu sana wao wanatulipa sie 3% of the production wakati sie tunawarudishia wao tax refunds. it does take an intelligent person to know something is fishy somewhere. This tax refunds hawa wachimbaji madini wanaweza kuwa hawazihitaji (afterall they are getting 97% of their production) bali ikawa mrija wa wazee wa 10%.
 
Iko wapi wizara ya nishati na madini, iko wapi kamati ya bunge watupe ufafanuzi?yuko wapi zito kabwe aliyeibua skendo za madini na kunyamazishwa kwa kuteuliwa katika kamati ya madini?




 
Hivi ile mambo za uraia wa nchi mbili zaanza lini tena maana nshachola sasa:A S angry::A S angry::A S angry::A S angry::A S angry::A S angry:
 
inasikitisha kwa kweli sina cha kuchangia hapa nayaacha kama yalivyo..........:frusty::frusty::crying::crying:
 
Hivi hii nchi jamani inatatizo gani? tunawatawala wa namna gani jamani? hawa watawala wetu mbona hawana uchungu na hii nchi?
Ndio maana huwa namfagilia sana Mzee mgabe,yeye habemberezi mwekezaji,hutaki funga vilago ondoka,madini hayaozi,lakini hapa Tanzania ni kama Mbwa na Chatu,tunawatetemekea wawekezaji hatimae wanatuumiza na bado tunakenua meno na kufurahi

Yaani nashindwa kuelewa kabisa,hao jamaa kwanza wametuulia watu wetu kwa kuwaanguza na tindikali,wengine wame mchoma ndugu yetu moto pale DSM,lakini bado tunaendelea kuwalipa mabilini ya pesa.

Umefika wakati sasa watawala husika waachie ngazi,tumechoka na madudu ya hii
Watanzania tunasubiri nini? ama tumelizika na hali hii?
 
Tax Refund is very normal practice!! Lakini kwa nini refunds ziliachwa zika-accumulate to this extent?

Some where something is wrong!! I surely suspect a kind of downstream for monies squanderers!!!
 
Tax Refund is very normal practice!! Lakini kwa nini refunds ziliachwa zika-accumulate to this extent?

Some where something is wrong!! I surely suspect a kind of downstream for monies squanderers!!!
 
Jasusi vitu vingine muhimu lakini bora kufa kuliko kivisikia... khaa!!! jamani yani chozi linataka kutoka lakini basi najitahidi kuvumilia maana mimi mtu mzima, lakini ukweli wajuu wetu watayachapa viboko makaburi yetu, hivi hatuwezi kuwaiga hata hao bushmen wa Botswana?? Maana wenzetu wanafaidi rasilimali zao
 
Hawa Jamaa hawata kaa na kuripoti faida hata siku moja kwenye mahesabu yao. Mimi nimeshakuwa consultant katika migodi ya Barrick and Angro, hawa ni wahuni sana. Wanatransfer faida mapema sana kwa kutumia manunuzi. Yaani wananunua spares na Equipment toka kwenye makampuni tanzu yao kwa bei za juu sana. As a result wanakuza expenses kwenye mahesabu, na kushusha faida. Mara nyingi wanatumia sana non tangible assets kama Computer Softwares na kadhalika, ambazo wanajua TRA au Watz wanashindwa kujua gharama halisi. Utakuta wanaweza kubadili software kila mwaka. Wanatumia consultancy services za kutoka kwenye kampunzi tanzu zao kwa bei kubwa hata kama utaalamu huo unaweza kupatikana nchini. Tatizo la Viongozi wetu hata ukiwatonya, ndio kwanza wao wanaenda kuvujisha siri iliwavute chochote. Kutrace hasabe zao ni vigumu sana kwani Ofisi za wahasibu zinafanywa nje ya nchi, hapa wahasibu kazi yao ni kuscan document na kusend basi.
 
Chapakazi;
Point...lakini mh, kumbuka kuwa resources sio kitu kinachoisha. In the longrun, you hold the bargaining power! Hicho ndicho kitu ambacho hatujajifunza! Tatizo ni hawa viongozi wetu WAJINGA wasiokuwa na upeo. Wao wanawaza leo, leo, leo, na tumbo langu, tumbo langu, tumbo langu. Ingali ningepata nafasi ya uongozi...bongo mngelia! Sipendi ujinga kabisa!!!

Mkuu madini ardhini huwa kwani yanazaliana? Siku ya siku yakiisha wataondoka na kutuachia mashimo tu. Tanzania tuna hatari kwakweli. Sijaona nchi yenye viongozi wanaopenda kujilimbikizia mali kama TZ, wanaamua kuingiza nchi kwenye hasara kama hizi kwa faida ya matumbo yao.
 

Yaani inauma kweli mkuu. Hii kitu wanatufanyia hawa jamaa wa makampuni ya madini ni sawa na kumkamua panya. Lol! Jamaa hata huruma hawana. Yaani wanavyochukua hadi mchanga wa dhahabu na kurusha kwa ndege zao moja kwa moja toka kwenye viwanja vyao huko migodini bado tena wanakuja na lingine. Ina maana jamaa wanachukua madini halafu serikali inawalipa on top of that. Kwa kifupi ni kwamba wamekuja kuchukua hata pesa za walipa kodi wetu mbali ya hayo madini. Mbaya sana hii.
 
Mungu wangu weeeeeeee nahisi tumbo la kuhara, nitarudi badae kukoment
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…