Barrick yapongezwa kwa kutekeleza sera ya Local content kwa vitendo na kunufaisha Watanzania

Barrick yapongezwa kwa kutekeleza sera ya Local content kwa vitendo na kunufaisha Watanzania

Blasio Kachuchu

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
366
Reaction score
243
1716388237536.png

Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Melkiory Ngido akisalimiana na Waziri wa Madini, Antony Mavunde alipotembelea banda la Barrick akiongoza ujumbe wa viongozi mbalimbali wa Serikali.​

Na Mwandishi Wetu.

Waziri wa Madini, Mh.Antony Mavunde, ameipongea kampuni ya dhahabu ya Barrick nchini kwa kutekeleza kwa vitendo sera ya ushirikishaji watanzania na kuwanufaisha kupitia mnyororo wa uwekezaji katika sekta ya madini (Local content).

Pongezi hizo zilitolewa wakati wa mkutano wa Jukwaa la tatu la utekelezaji na ushirikishaji watanzania katika sekta ya madini unaondelea katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.

Akiongea baada ya kutembelea banda la maonesho ya Barrick lililopo kwenye eneo la mkutano huo baada ya kupata maelezo jinsi kampuni inavyotekeleza sera hiyo kutoka kwa Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Melkiory Ngido, Waziri Mavunde ambaye alifungua rasmi mkutano huo amesema Barrick ni mfano wa kuigwa katika utekelezaji wa sera ya Local content kutokana na uwekezaji wake nchini kwa kwa na serikali kupitia kampuni ya Twiga Minerals.

Waziri Mavunde, alipongeza pia mchakato mzuri wa kufunga mgodi wa Barrick Buzwagi uliofanywa na Barrick kwa jinsi ambavyo tayari umeanza kufungua milango ya kiuchumi mkoani Shinyanga na mikoa mingine ya kanda ya ziwa na nchi jirani.

Awali akitoa maelezo kwa Waziri wa Madini aliyeongeza ujumbe wa viongozi mbalimbali wa Serikali,Meneja wa Barrick nchini,Melkiory alieleza jinsi kampuni ya Barrick inavyoendelea kunufaisha wazawa kupitia sera hii ya Local content ambapo asilimia kubwa ya manunuzi kwenye migodi yanafanyika kutoka kwa wazabuni wazawa.

Barrick imekuwa ikitekeleza sera hii kwa vitendo katika maeneo ya ajira ,utoaji wa zabuni sambamba na kufanikisha miradi ya kijamii katika maeneo yanayozunguka migodi kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR).

Barrick inayo programu ya kuwaendeleza wafanyabiashara wazawa (Local Business Development Programme) ambayo ni mhimili katika kusimamia sera hii na tayari wafanyabiashara wamekuwa wakipatiwa mafunzo katika awamu mbalimbali kupitia programu hii.
1716388278363.png
Waziri wa Madini, Mh.Antony Mavunde (wa kwanza kulia) akipata maelezo ya jinsi Barrick inavyowezesha watanzania kupitia uwekezaji wake kutoka kwa Meneja wa Barrick nchini Melkiory Ngido (kushoto) alipotembea banda la maonesho la kampuni hiyo kwenye mkutano wa Jukwaa la tatu la utekelezaji na ushirikishaji watanzania katika sekta ya madini unaondelea jijini Arusha katika ukumbi wa AICC.

1716388325516.png

Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Melkiory Ngido katika mkutano huo.
1716388372346.png

1716388391985.png

Wafanyakazi wa Barrick wanaoshiriki mkutano huo.​
 
Badala ya kusisitiza kupata vitofali vya dhahabu toka jumla nzima ya vitofali vya dhahabu vinavyozalishwa, serikali inalilia mgao huu
kampuni ya Barrick inavyoendelea kunufaisha wazawa kupitia sera hii ya Local content ambapo asilimia kubwa ya manunuzi kwenye migodi yanafanyika kutoka kwa wazabuni wazawa.

Barrick imekuwa ikitekeleza sera hii kwa vitendo katika maeneo ya ajira ,utoaji wa zabuni sambamba na kufanikisha miradi ya kijamii katika maeneo yanayozunguka migodi kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR).
Toka Maktaba :


Na mgawanyo uwe vitofali vya dhahabu, karai la Vito n.k au makubaliano baina ya mwananchi mnyonge mwenye kumiliki ardhi au baina ya kijiji kinachomiliki ardhi na mwekezaji.

1 Julai 2023

Chini ya mkataba mpya uliotangazwa Ijumaa, Botswana inapata sehemu kubwa ya mawe yasiyochorogwa ya almasi kutoka kwa ubia wao, Debswana.

Botswana na kampuni ya madini ya De Beers wametangaza mkataba mpya wa mauzo ya almasi.
1716387701295.png




Mkataba huo mpya, uliohitimishwa siku ya Ijumaa, unaipa Botswana sehemu kubwa ya almasi isiyo chorongwa kutoka kwa ubia wao.

Debswana , ubia wa awali kati ya kitengo cha Anglo American De Beers na serikali ya Botswana , inauza 75% ya pato lake kwa De Beers , huku salio likichukuliwa na kampuni ya serikali ya Okavango Diamond Co.

Makubaliano hayo mapya yanahusu mkataba wa mauzo wa miaka 10 wa uzalishaji wa almasi wa Debswana hadi 2033 na leseni ya miaka 25 ya uchimbaji madini ya Debswana .

Katika maandalizi ya makubaliano ya Ijumaa, Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi , ambaye anatarajiwa kugombea tena urais mwaka ujao, alikuwa ameshinikiza De Beers kupata sehemu kubwa ya pato la Debswana .

Mwezi Machi, Botswana ilitangaza kuwa itachukua asilimia 24 ya hisa katika kampuni ya Ubelgiji ya kusindika vito ya HB Antwerp katika hatua inayoonekana kama iliyoundwa kupunguza nguvu ya De Beers kwenye vito vya nchi hiyo.

Botswana inasambaza 70% ya almasi ya De Beers
 
Back
Top Bottom