MANILABHONA
JF-Expert Member
- Apr 1, 2015
- 462
- 350
Shikamoo babu
Salaam kutoka duniani
Tunapoazimisha miaka 20 toka mwenyezi mungu akuvune baada ya kumaliza kazi tunasikitika sana kuona tulio wengi tumesahau uliyotuasa, tumesahau wosia wako.
Nakumbuka pale ulipoona uhuru wa Tanzania si uhuru kama nchi nyingine za afrika haziko huru, ukaongoza mapambano ya kuhakikisha nchi zingine nazo zinapata uhuru. Nakumbuka ulipomuona mwafrika mwingine yeyote kuwa ni ndugu na afrika ni moja .
Nakumbuka ulipotoa sehemu ya nchi uliyoiongoza maeneo ya Mpanda,Tabora, Kigoma, Kongwa, Mpwapwa, Mtwara na hata Morogoro kutumiwa na ndugu zako waafrika kwa matumizi mbalimbali. Wengi walizaliana hapa na kupata uraia hata sasa tuna viongozi wengi serikalini na wanasiasa waliozaliwa na kulelewa katika makambi hayo.
Nakumbuka wakati fulani uliwaambia wamarekani weusi warudi nyumbani-Afrika na ukawakaribisha Tanzania kama nyumbani kwao
Ninakumbuka ulipotuasa tusibaguane kwa namna yoyote ile iwe kidini,kikabila kikanda n.k kwani ubaguzi hauna tofauti na kula nyama ya mtu mara tutakapoanza kubaguana tu tutaendelea hivyo bila kukoma-dhambi ya ubaguzi itatutafuna, ukaatolea mfano Tanzania na Zanzibar halafu Pemba na Unguja n.k.
Ukaongelea maendeleo yasiyogusa watu walio wengi si maendeleo, ukasema maendeleo lazima yawe ya watu si vitu. Haya na mengine mengi uliyataja kama nyufa. Ulituasa tuchague viongozi wanaoyaona matatizo yetu kama tunavyoyaona sisi. Wewe ulijenga uzalendo, uliishi uzalendo, ulikuwa mzalendo
Siku hizi mambo yamebadilika sana, tunafukuzana wenyewe kwa wenyewe tena kwa aibu, waafrika wanaua wenzao kisa eti wamepora fursa au nafasi za ajira, wengine wamefikishwa mahakamani kwa visingizio kuwa si raia wa nchi, pamoja na kwamba kwa kumtazama tu sura yake unaona ni mwenzetu, ni mwafrika halisi. Wapo waliotishiwa uhai na wengine kupotea na kupoteza uhai kwa sababu zisizo wazi
Ubaguzi sasa ni dhahiri, sio ufa tena bali ni ukuta umebomoka, zimebaki nguzo tu ulizotuwekea. Sijui nazo zikianguka itakuwaje. Tunabaguana kwa ukanda ,kwa makabila. Tumeanza kupanda mabasi ya ukabila.
Haya yanajionesha wazi katika chaguzi na hata katika teuzi bila hata aibu wala woga. Sio ajabu sasa kuona eneo fulani la nchi wanachagua kiongozi kwa misingi ya unasaba na kiongozi husika au uteuzi kuhusisha watu wa aina fulani tu na kusahau sehamu kubwa ya nchi.
Siku hizi viongozi wanayajua sana matatizo ya wananchi na wanayaona kwa namna yao na si wayaonavyo wananchi.
Siku hizi viongozi ndio wanasifia wajibu unaofanywa na serikali au wajibu wanaoufanya wao, sio tena wanyonge kuisifia serikali yao kwa kazi ilizofanya kama ilivokuwa awali wananchi walipotunga nyimbo na kuimba nyimbo za sifa kwa serikali yao, siku hizi ukiona mtu katunga wimbo wa kusifia Serikali ujue ni kwa ajil ya kitu fulani si bure kama awali.
Si ajabu siku hizi kusikia kiongozi akijisifia tumejenga hospitali mia moja, badala ya wananchi kusifia serikali imetujengea hospitali tunaishukuru-wananchi hawasikiki tena kama ilivokuwa awali.
Siku hizi uzalendo hauonekani , udugu haupo tena, tuna waheshimiwa (watwana) na wanyonge, hatuitani ndugu tena.
Kila mtu anapambana kujaza tumbo lake na matumbo ya wanaomzunguka
Tunatamani Mungu angekurejesha duniani angalau hata kwa sekunde tano uyaone ya sasa na utupe wosia mwingine au utuelekeze
Wasalaamu