Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Jimbo la Karagwe, Mkoani Kagera, Ndg. G.M. Kitonka
Mhe. Dk. Wilson Charles Mahera, Mkurugenzi wa Uchaguzi,
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dodoma,
YAH: KUENGULIWA KIHUNI KWA AMOS PETER KAHWA, MGOMBEA UDIWANI KATA YA KAYANGA, WILAYANI KARAGWE, MKOANI KAGERA
Somo hapo juu lahusika, na linaletwa kwako kwa njia ya dharula ili kukuomba uchukua hatua za makusudi kulinda heshima ya NEC mbele ya macho ya wapiga kura wa wilaya ya Karagwe.
Lakini kwanza nijitambulishe kwako. Naitwa Deusdedith Jovin Kahangwa, mkazi wa wilaya Karagwe, mkoani Kagera. Ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), na mshauri mkuu wa masuala ya uchaguzi ndani ya chama wilayani Karagwe. Kwa sababu ya nafasi yangu hii nimeshiriki moja kwa moja kwa kusimamia rufaa zote zilizokatwa na wagombea wa Chadema hapa wilayani, kama ifuatavyo:
Mosi, nimeshiriki katika kufanya kazi ya kufremu, kuandika kwa mkono na kwa kompyuta, na hatimaye kusajili rufaa ya mgombea ubunge wa Karagwe kupitia Chadema, Adol Pelleus Mukono, katika ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Karagwe. Tayari uamuzi wa rufaa umetolewa na ofisi yako. Nimeridhika kwamba ofisi yako imtenda haki katika kipengele hiki. Asante.
Pili, nimeshiriki katika kufanya kazi ya kufremu, kuandika na kusajili rufaa ya mgombea udiwani wa Kata ya Bweranyange. Kata hii iko kilometa 50 kutoka makao makuu ya wilaya. Msimamizi wa Wilaya ya Karagwe alimnyima nafasi ya kugombea na kuchelewa kumpa mgombea huyu majibu kwa siku tatu.
Hatimaye, majibu yalifikishwa nyumbani kwa mgombea saa mbili usiku kupitia kwa dereva wa bodaboda aliyekodiwa na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata ya Bweranyange.
Nilimwita mgombea huyo, tukajaza fomu ya rufaa, kwa kuandika tarehe na muda mgombea alipopata majibu kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi, yakiwa yamecheleweshwa kwa siku tatu. Uamuzi wa rufaa hii umetoka na mgombea wetu amerejeshwa ulingoni. Nakushukuru kwa kusimamia haki katika kipengele hiki. Ubarikiwe.
Na tatu, nimeshiriki katika kufanya kazi ya kufremu, kuandika na kusajili rufaa nyingine 12 za wagombea udiwani katika ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Karagwe.
Maamuzi ya rufaa hizi yametolewa tayari. Wagombea udiwani 8 kati ya 12 wamerejeshwa ulingoni. Nakushukuru kwa kusimamia utendaji wa haki kwa wagombea udiwani 8.
Kati ya wagombea udiwani wanne ambao ofisi yako imewaengua, nina manung'uniko ya haraka kuhusu wagombea wawili ambao uamuzi wa ofisi yako unaonekana kuwanyima nafasi ya kupanda jukwaani kihuni.
Naongelea wagombea udiwani wa kata za Kayanga na Chanika. Nimesoma barua za kuwaengua katika nafasi ya kugombea udiwani kama zilivyoandikwa na ofisi yako. Sababu zilizotolewa dhidi ya wagombea wawili Amos Kahwa na yule wa Chanika zinashangaza sana.
Kwa hapa najielekeza kwenye barua ya kumwengua Amos Kahwa ambayo inasema kwamba, rufaa yake imekataliwa kwa sababu "rufaa imewasilishwa nje ya muda" (tazama Kiambatanisho A). Barua hiyo imeandikwa na Tume tarehe 14 Septemba 2020 na kusainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi aitwaye Gerald G.J. Mwanilwa.
Hata hivyo, ushahidi uliowasilishwa kwenye ofisi ya NEC Dodoma, kwanza kupitia kwa Katibu wa Chadema wa Wilaya ya Karagwe, na pili kupitia Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Karagwe, unaonyesha kwamba, rufaa ya Amos Kahwa ilisajiliwa kwenye Tume tarehe 26 Agosti 2020 saa 9.25 mchana, ndani ya masaa 24 mara tu baada ya pingamizi kuwekwa dhidi ya Amos Kahwa. (Tazama Kiambatanisho B).
Wakati rufaa ya Amos inapokelewa na kusainiwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Karagwe nilikuwepo ofisi kwa Msimamizi wa Wilaya. Tunafahamiana vizuri hata kabla hajawa DED hapa Karagwe.
Hivyo basi, kwa heshima kubwa, napenda kukanusha na kuikosoa uamuzi wa NEC katika suala hili. Kwa ajili ya ufafanuzi, natumia mfano wa Amos Kahwa wa kata ya Kayanga, ni kama ifuatavyo:
Mosi, rufaa ya Amos Kahwa inatokana na uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi wa Kata ya Kayanga, John Kabika Bigemano, kukataa kumteua kama mgombea nafasi ya Udiwani wa Kata hiyo, kwa sababu ya madai kwamba Amos Kahwa ana hatia ya kukwepa kulipa kodi.
Pingamizi linasomeka hivi: "Mgombea hajatimiza sifa/masharti yote ya kuwa mgombea kwa mujibu wa sheria kutokana na kutotimiza kanuni ya 22(4) ya kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa (uchaguzi wa madiwani) 2020, katika tamko la kisheria la mgombea udiwani sehemu 'E' namba '7' ya fomu namba 8C." (Tazma Kiambatanisho C).
Kwa mujibu wa sehemu 'E (7)' katika fomu namba 8C, sababu inayodaiwa kumnyima Amos Kahwa nafasi ya kugombea ni hii:
"Katika kipindi cha miaka mitano kabla ya uchaguzi [amewawahi/hajawahi] kutiwa hatiani na mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya serikali." (Tazama kiambatanisho D).
Msimamizi wa Uchaguzi Msaidizi wa Kata ya Kayanga hakubainisha vielelezo kwa ajili ya kuthibitisha tuhuma yake hii.
Lakini, vyanzo mbalimbali vya kiuchunguzi vinaonyesha kuwa msingi wa pingamizi hili ni hukumu katika Kesi Na. 195/2014, katika Mahakama ya Wilaya Kayanga, iliyotolewa 28/05/2015 na kumtia hatiani Amos Kahwa chini ya kifungu cha 273(b) cha Kanuni ya Adhabu (Sura ya 16, Toleo la 2002). Alihukumiwa kifungo. (Tazama kiambatanisho E).
Lakini kupitia hukumu ya rufaa na. 48/2015, iliyotolewa 12/11/2015 katika Mahakama Kuu ya Bukoba, Amos Kahwa aliachiwa huru na kusafishwa tuhuma zote. (Tazama kiambatanisho F).
Nikiwa nayafahamu haya yote, siku ya uteuzi wa wagombea udiwani nilifika katika Ofisi za Kata ya Kayanga nikitaka kujua mchakato wa uteuzi unaendeleaje chini ya kofia yangu kama mwandishi wa habari.
Lakini, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata alinikataa kujibu maswali yangu kwa sababu kwamba, kulingana na kitabu cha mwongozo wa uchaguzi mkuu alichopewa "hana mamlaka ya kuongea na waandishi wa habari."
Pili, rufaa ya Amos Kahwa ni miongoni mwa rufaa 12 za kwanza tulizozisajili kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa Uchaguzi Karagwe KWA WAKATI MMOJA.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Karagwe, Ndg. G.M. Kitonka, alisaini nakala ya fomu ya Amosi Kahwa na kuandika muda rufaa husika ilipowasilishwa kwake, fomu ambayo imewasilishwa kwenye ofisi za NEC Dodoma kama kielelezo.
Tatu, rufaa baki 10 ambazo ziliwasili pamoja na rufaa ya Amos Kahwa zimefanyiwa uamuzi, na hakuna rufaa hata moja kati yake iliyokataliwa kwa sababu kwamba ilisajiliwa nje ya muda.
Nne, rufaa ya mgombea wa Kata ya Bweranyange iliyosajiliwa ya mwisho, ikiwa nje ya muda kwa siku tatu, lakini kwa sababu ya ujanja ujanja katika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Karagwe, tayari imefanyiwa uamuzi na mgombea wetu amerudishwa bila kuambiwa kwamba rufaa yake ilisajiliwa nje ya muda.
Na tano, uamuzi wa awali kuhusu rufaa ya Amos Kahwa uliotolewa na NEC Dodoma ulionyesha kwamba "Amos Kahwa wa Kata ya Kayanga iliyoko Ukerewe" ameenguliwa kutoka kwenye kinyang'anyiro.
Lakini tukafanya utafiti na kujiridhisha kwamba katika Jimbo la Ukerewe iliyoko mkoani Mwanza hakuna Kata yenye jina la "Kayanga," na kwamba huko hakuna mgombea anayeitwa "Amos Kahwa."
Hivyo, tukaamua kumshauri Amos Kahwa afike Makao Makuu ya NEC Dodoma kuleta malalamiko juu ya ujanja huu uliofanywa dhidi yake. Alifanikiwa kuingia ofisi za NEC Dodoma na kuelekezwa kuweka malalamiko yake kwa maandishi.
Nilishiriki kufremu na kuandika malalamiko haya. Pia nilimsindikiza Amos kahwa hadi Dodoma kwenye Ofisi za NEC. Hatimaye malalamiko yake yalisajiliwa katika ofisi za NEC Dodoma.
Katika malalamiko haya ya mwisho Amos alisisitiza maomba yaje kwa kuitaka NEC kubatilisha uhuni uliofanywa dhidi yake kwa sababu ya madai kwamba "japo Amos Kahwa aliwahi kufungwa, na kutoka gerezani kwa njia ya rufaa aliyoishinda, lakini bado, kwa mujibu wa mshtaka yaliyompeleka kifungoni, tayari alikuwa amekwisha ikosesha kodi serikali."
Hili ndilo pingamizi alilowekewa na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata ya Kayanga. Ni pingamizi la hovyo kimantiki, kisheria na kimaadili. Na kwa hakika, maelezo ya Amos Kahwa niliyoshiriki kuyaandika yameweka hoja yake vizuri sana.
Kwa sababu hizi zote, inafuata kimantiki kwamba, kuna njama zimefanywa kupitia ofisi za NEC Karagwe na Dodoma kuhakikisha kwamba mgombea udiwani Kata ya Kayanga, Amos Kahwa, hapati nafasi ya kupanda jukwaani.
Napenda ufahamu kuwa, kata ya Kayanga ndiko yaliko makao makuu ya wilaya, yaani Boma la DC, Godfrey Mheruka. Lakini, ni kata ambayo imekuwa mikononi mwa upinzani kwa muda mrefu. Mwaka 2010 ilianguka mikononi mwa CUF; mwaka 2015 ikaanguka mikononi mwa Chadema.
Na sasa mazingira yanaonyesha kwamba kuna mkakati haramu wa kuzima matakwa ya wapiga kura wa Kata ya Kayanga. Hata kata ya Chanika ni kata iliyokuwa mikononi mwa Chadema tangu 2015.
Pia yafaa ufahamu historia ya ukatili wa kisiasa Karagwe ili uweze kuona sababu ya kulipatia uzito suala hili. Mwaka 2014, Chadema iliwekewa mapingamizi kwenye vitongozi 36 vya tarafa ya Bushangaro na kushinda kesi. Uchaguzi haukufanyika mpaka mwaka 2019, mwaka ambao uchaguzi haukufanyika tena.
Yaani, Karagwe kuna wezi wa haki za wapiga kura kwa muda mrefu. Wananchi wanataka tabia hii ikome tangu sasa kupitia mikono yako. Tayari umeonyesha dalili nzuri za kutenda haki, kadiri Karagwe unavyohusika. Usikubali kula ng'ombe lakini ukashindwa mkia.
Hivyo, napenda kukuomba upitie mafaili yako na kusafisaha ofisi yako kwa kumrejesha Amos Kahwa jukwaani bila masharti yoyote. Kama ofisi yako itahitaji ushahidi wa ziada niko tayari kuuwasilisha. Nimejizuia kuuweka hapa kwa kuwa naamini kwamba UNAWEZA.
Namalizia barua hii kwa sala maalum inayoongozwa na dhana ya " kuufanya upya uso wa dunia," maneno yaliyoko katika Zaburi ya 104, ibara ya 30, kama ifuatavyo:
“Ewe Mungu, tunakuita kwa sauti ya kilio, sisi ambao ni wazaliwa katika ardhi ya Karagwe, na ambao pia ni wapiga kura wenye haki ya kujichaguliwa viongozi wa kisiasa. Tunakuita kwa sauti inayowakilisha vilio vyote vya watu wenye kiu ya haki katika milenia hii ya tatu.
"Tunakuita kwa sauti ya kilio katika novena ya siku 30 kuelekea kwenye uchaguzi mkuu tarehe 28 Oktoba 2020. Tunakuomba umtume Roho wako Mtakatifu ashuke duniani! Umruhusu Roho wako Mtakatifu ateremke duniani na kutenda muujiza.
"Tunaomba asiacha mwaka huu upite bila kutenda muujiza wa ukombozi wa Karagwe dhidi ya ukatili wa kiafya, ukatili wa kielimu, ukatili wa kiikolojia, ukatili wa ofisini, na ukatili wa kiuchumi.
Tuonyeshe hasira zetu dhidi ya uhuni huu kwa kumpa Lissu kura za kimbunga. CCM iwe na madiwani hao wa dhuluma na Upinzani uwe na Rais. Tuonane 28 Oct 2020.

JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.