Barua kwa Mpendwa Mwalimu wangu

Barua kwa Mpendwa Mwalimu wangu

black abdu

Senior Member
Joined
Dec 2, 2022
Posts
156
Reaction score
212
Nimeona post imesambaa sana ya barua ya mapenzi iliyoandikwa na mwanafunzi kwenda kwa mwanafunzi mwingine...kwa Zama hizi hili linaonekana la ajabu lkn nyakati zetu halikuwa jambo la ajabu, binafsi nilikuwa bingwa wa kuandika barua za aina hiyo. Namuomba binti aniazime daftari, japo sina haja ya kulisoma, so naenda kuandika barua na kuiweka ndani ya daftari lile, ataikuta huko.

Sasa nikiwa darasa la sita ikitokea tu kumpenda ticha wangu mmoja, na hii pia ni shida ya kuanza shule na umri mkubwa kama ilivyokuwa kwa kipindi hicho.

Sasa huyu ticha nilivutiwa nae, japo sikuwa na hakika ningefanya nini na hisi hizo juu yake. Nilikuwa navizia muda yeye anakuja shule au anaondoka, nakuwa natembea nyuma yake hadi akiingia kwake mie napitiliza.

Ikatokea nikazoweana nae, mara kadhaa akawa ananituma, au nikikatisha mbele yake ananisemesha, hata siku moja akaniokoa kupata adhabu.

Hisia zikanizidi nikaandika barua kuelezea hisia zangu, na mpango ulikuwa muwahi shule na kuipenyeza chini ya mlango wa ofisi yake, ili akiingia tu ofisini akumbane nayo.

Sikuandika jina langu kwenye ile barua (kwa tahadhari) ila nikabainisha namna gani anaweza kunigundua, kuwa aangalie mwanfunzi anayemuangalia Sanaa akiwa mistarini.

Hata hivyo sijufanikisha kupitisha ile barua chini ya mlango wa ofisi kama nilivyopanga, nikawa natembea nayo ndani ya madaftari yangu....hadi siku nimeidondosha nyumbani bila kujua, ikaokotwa na mdogo wangu mdogo sana wakati huo.

Sister anamuona mtoto ameshika karatasi, akaichukua akaifunua, akaanza kuisoma kwa sauti. Salalaa ni ile barua yangu. Niliirukia kama nyau anavyorukia mjusi ukutani. Tukanyang'anyana sana hadi ikachanika-chanika na nikahakikisha naichoma moto baada ya kufanikiwa kuitwaa.

Hiyo ikawa salama yangu, ila laiti ingeokotwa tukiwa shule hivi, ingekuwa balaa na buluu.
 
Back
Top Bottom