Mohamed Ismail
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 224
- 236
BARUA WAZI KWA MPENZI WANGU
________________
Dear my love.
Leo ni siku yangu mbaya katika maisha yangu. Sikutegemea kama ingetokea ghafla mimi na wewe tukaachana. Tumepitia katika kipingi kigumu si masika , kiangazi , vuli na kipupwe kote tulikuwa pamoja. Kama ni jua lilituchoma wote, kama ni mvua wote ilitunyea vilevile kwenye kivuli tulikaa wote. Siyo tu huku kama ni shambani tulilima wote tulichokivuna tulikigawana sawasawa iwe hasara au faida.
Najua umevumilia mambo mengi kuhusu mlimwengu mimi watu walihisi mimi na wewe tutaachana lakini haikutokea hivyo. Uliweza kunivumilia kwenye shida na raha.
Wahenga wanasema ukitaka kuruka lazima uagane na nyonga na mimi leo nikiwa natazama magharibi ,mashariki, kaskazini na kusini hakuna namna lazima mimi na wewe tuachane. Ndio iwe kikomo chetu kumbukumbu acha zibakie kwenye gala la picha.
Najua umenivumilia mengi nilikuahidi kwamba mimi na wewe hatutaachana mbali na hivyo nilikuahidi mambo mengi ambayo ilibidi niyatekeleze lakini sikufanya hivyo na bado hukukata tamaa. Ila na mimi unajua ni binadamu sijakamilika leo naachana na wewe naamini utanipa baraka kwa mpenzi mpya nitakayempata awe mzuri kama wewe na ikiwezekana awe bora kukuzidi. Najua ni mapema sana ila naomba baraka zako. Nitalimiss sana joto lako kipindi cha baridi ulinikumbatia na kunipa faraja na nilipopata changamoto uliniambia kwa sauti ya chini Mlimwengu be strong you are a man. Nitakumbuka sana upendo wako na hukutaka kunitenganisha na rafiki zangu pamoja na ndugu zangu. Na wao kuanzia leo siyo shemeji yao wala wifi yao ingawa na wao wamesikitika sana lakini alipangalo Mungu huwezi kujua maana yeye ndio aliyekalia kiti cha ukuu.
Nichukue nafasi kudedicate wimbo wa Manhattan wa Lets kiss and say goodbye. Hili ni busu langu la mwisho kwako na ninaomba likawe baraka kwangu pamoja na kwako huko uendako. Mapenzi ya moto moto uliyonipa yalikuwa zaidi naweza kusema si mapenzi tu bali ni mahaba. Ulinifanya nijione mwanaume wa kweli waliposema kwamba Mlimwengu ni kitu gani ila wewe ulinivuta mkono na kunipiga kiss kwamba i am your one and only.
Nikuahidi makosa yangu mengi kwako naenda kuyafanyia marekebisho kwa mpenzi mpya. Nitamuhusudu na nitaheshimu sana muda wake na kile nitakachomuahidi nitajitahidi nikitekeleze kwa uharaka zaidi. Naomba pepo langu la kusema nitaanza kesho liishe leo maana kesho haijawahi kufika. Na siku zote nilikuwa nasema baby nitakuambia kesho kesho lakini siku zikawa zinapita na sikuambii. Nakumbuka kuja kukuambia leo. I am so sorry my love.
Mlimwengu mimi nilikuwa na mengi ya kusema hapa ninabubujikwa na machozi tu hadi nashindwa kuendelea. Machozi yangu yamegawanyika katika sehemu mbili. Jicho la kushoto linatoa machozi ya uchungu ya kuachana wewe na wakati bado ninakupenda lakini jicho la pili lina machozi ya furaha maana huku kwetu mvua na jua vikiwepo kwa pamoja tunasema simba anazaa. Mimi mwenyewe nyota yangu ya simba hivyo naamini mpenzi wangu mpya anazaliwa ambaye nitamlinda ni nitamtunza kama mboni ya jicho.
Mpenzi wangu 2019 kwaheri karibu laazizi wangu 2020.
Wako
Mlimwengumimi
Mohamed Ismail
Email:mohammedismail613@gmail.com
0762 07 03 61
31/12/ 2019
Sent using Jamii Forums mobile app