Sentence case: Kilio chetu kwako, Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
Sisi wananchi wa Musoma Vijijini, Tarafa ya Njanja Majita, tunapenda kuleta kilio chetu kwako, Mh. Rais. Tuliyekupigia kura wakati uchaguzi uliopita, na ambaye tutakupigia kura uchaguzi ujao wa 2010 ili uweze kumaliza kipindi chako cha miaka Kumi katika madaraka. Tunakuomba usome waraka huu vizuri kasha utujibu sisi wananchi, hata kupitia vyombo vya habari. Hatutaki Mbunge wetu aje aseme kwa niaba yako, kwani si mpenda maendeleo hasa huku Majita.
Tarafa ya Nyanja ina Kata 12, na kila kata kuna shule zaidi ya moja. Tarafa hii inasifika sana kwa uvuvi wa samaki na dagaa, hasa kule Busekera, na baadhi ya vijiji vilivyopo kando kando ya ziwa. Wananchi tunachangia kulipa kodi ya serikali kama itavyotakiwa, japokuwa hatujawahi kuambiwa ni kiasi gani cha kodi tumechangia katika mwaka wa fedha.
Tarafa yetu hii imekuwa na matatizo mengi sana na sugu ambayo yametufanya tuachwe nyuma kimaendeleo ukilinganisha na upande wa pili wa Musoma Vijijini, nazungumzia Butiama na vitongoji vyake. Nadhani hata wewe, Mheshimiwa Rais, ulipokuja kwenye Mkutano Mkuu wa Halmashauri ya Taifa miezi michache iliyopita, ulipata fursa ya kuonyeshwa maendeleo ya upande wa kwako, hasa kujengwa kwa shule za kisasa ambazo baadhi zao kuna kompyuta na madawati. Lakini kwa bahati mbaya, Mbunge wetu hakuchukua jukumu la kukuleta wewe au mawaziri wengine katika tarafa yetu ili waone nini amefanya. Huku Majita hakuna kabisa alichofanya zaidi ya kutoa misaada ya mabati na jenereta ambayo nayo ipo takribani miaka mitano na itaoza.
Matatizo tuliyonayo sisi wananchi ni mengi ambayo Mbunge wetu hajashindwa kuyatatua kabisa na kuegemea upande mmoja wa kwao. Naomba nianzie upande wa shule za Msingi; kwa ujumla, shule si nzuri na hazipo kwenye hali ya kuridhisha kabisa. Wanafunzi wanakaa nchi kutokana na ukosefu wa madawati, vyoo hakuna, na hata kama vyoo vipo, basi vimejaa tayari. Watoto wetu wanakuwa kwenye hatari ya kupata maambukizo kutokana na kutokuwepo na vyoo safi. Mbali na hilo, shule hazina madawati ya kutosha ambapo wanafunzi wanakaa kwenye mawe kama enzi ya Mkoloni. Walimu pia hakuna kabisa; mtoto anamaliza shule hafahamu hata kuandika au kuongea Kiingereza sababu kubwa wanadai uhaba wa walimu, vifaa vya kufundishia hakuna kabisa, japokuwa tunalipa kodi zetu kwa Serikali ili tuweze kunufaika na kodi yetu. Kwa kweli, Mh. Rais, kama kuondoa ujinga katika tarafa yetu hii itakuwa ni historia. Tunasikia kwenye radio kuwa kumetokea ubadilifu wa pesa za ualimu, Serikali inawasomi, kwani wasitatufe njia ya kufuatilia ni walimu wangapi wamelipoti kazini na pia kuwe na unique namba za ku track record za walimu.
Sekondari zipo 15 katika tarafa ya Njanja, tatizo ni uhaba wa walimu hakuna, vifaa hakuna vya kufundishia wanafunzi, mahabara kwa ajili ya kufanya practical hakuna kabisa. Watoto tunawalipia karo kila mwaka, lakini inapofika wakati wa kumaliza shule na matokeo yakitoka, ni zero ndiyo nyingi, na wachache tu hawafiki hata 20 ndiyo wanachaguliwa kuendelea na Kidato cha Tano. Ili tatizo limekuwa sugu, nenda rudi, lakini hakuna uvumbuzi wowote ule. Tumejaribu kumwambia Mbunge wetu, amekuwa ni Mbunge wa kuturidhisha na vijibati vichache, huku akiegemea kwake tu. Zaidi ya hilo, walimu hawaingii darasani kabisa na wanalipwa mishahara mwisho wa mwezi. Kumbuka pesa ya mshahara ni ya walipa kodi. Inaumiza kama mlipa kodi hapewi huduma ya kuridhisha. Kadhalika, amekuwa akijenga shule huko kwao tu na kupeleka wafadhili kuona maendeleo. Je, huku Majita hapaoni? Na kama wafadhili wanatoa misaada, je, wanatoa kwao? Rais, tusaidie ili na sisi Majita tuendelee.
Hospitali, ambayo ndiyo huduma muhimu hapa katika tarafa yetu ya Nyanja, cha kushangaza, tuna dahanati moja tu ya Mrangi ambayo imekuwepo hapa tangu enzi ya Mkoloni hadi leo, na haijawahi kufanyiwa marekebisho ya haina yoyote ya upanuzi. Kweli, Mh. Rais, fikiria tu. Tangu enzi ya Mkoloni, idadi ya watu itabakia kuwa ile ile? Hapana, idadi ya watu imeongezeka sana. Kwa hiyo, zahanati hii ni ndogo sana na haiwezi kukidhi huduma kwa jamii. Kwa hiyo, tunaishia kupoteza watu. Mbali na hilo, akina mama wajawazito wanakufa sana, hasa wakati wa kujifungua. Sababu kubwa ni ukosekanaji wa wakunga na vifaa, au wakunga hawapati mafunzo ya kutosha. Na siyo tu akina mama, watoto wetu wanafariki kila kukicha kutokana na kutokuwa na Zahanati nzuri na kubwa yenye huduma bora, zikiwemo na madawa. Zahanati yetu hii wakati wote haina madawa kabisa. Mbali na watoto, kuna magonjwa mengine yanatuumiza bila sisi wenyewe kufahamu. Mfano, kisukari, ugonjwa wa moyo, shinikizo la damu, malaria, na magonjwa ya kuambukiza. Kisa hakuna waganga, manesi, mahabara, madawa, pia choo hazitoshi kabisa. Kwa kifupi, huduma hakuna kabisa kwa wakina mama, watoto, wazee. Wanakufa kila kukicha. Kwa wale walio na ndugu wenye uwezo, ndiyo watasafirishwa kwenda Musoma Hospital kutibiwa, japo hospitali yenyewe mpaka ufahamiane na mtu.
Huduma ya maji hakuna kabisa. Bado wananchi wanasafiri maili 10 kwenda kuteka maji ili waje watoe huduma nyumbani. Kweli serikali inashindwa kupata wafadhili wa kusambaza maji Majita wakati ziwa lipo? Kama Musoma Mjini wamepata wafadhili kutoka Ufaransa na wametoa kiasi cha bilioni 14, je, sisi tunashindwa nini? Mbunge anafanya kazi gani? Yeye ni kwao tu. Tumechoka, Rais, na Mheshimiwa Mkono. Sisi wazee tunakuomba, baba, utuletee mfadhili wa kusambaza maji safi. Mpaka tunazeeka, hatujawahi kuona bomba, japo enzi za mkoloni kulikuwa na bomba.
Barabara bado ni mbovu sana, hasa ukizingatia tunatoa huduma ya uvuvi wa samaki huku. Wakati mvua zikinyesha, inakuwa shida kubwa sana. Kwa ujumla, barabara ni mbovu sana. Kwa hiyo, tunahitaji lami, kama itawezekana. Hatufahamu serikali inatoa kiasi gani cha pesa, hasa katika tarafa yetu hii. Sisi hatujui kabisa. Tunasemewa na viongozi tu ambao hata kufika huku hakuna. Report unayopewa ni ya uongo, kwa wakandarasi hawajawahi kufika huku kujionea taabu tunazopata.
Umeme hakuna, japokuwa tunasikia kwenye vyombo vya habari kuwa serikali ya Marekani ilitoa pesa kwa ajili ya kusambaza umeme vijijini. Lakini kama ni kweli, sisi wananchi hatupati taarifa kabisa, hata Mh. Mkono hase mi chochote. Haya ni baadhi ya huduma kwa jamii ambayo kwayo sisi wananchi wa Majita hatupati, na hatufahamu tunapata fedha kiasi gani katika bajeti.
Mh. Mbunge (Mkono) amekuwa akija kwetu hasa kwa sababu ya uchaguzi ambao umekaribia, na kutoa vijipesa vidogo kwa wananchi na kuhaidi kutuletea mabati kwenye mashule. Na pia kukutana na baadhi ya viongozi wa Tarafa na kuwapa pesa kidogo ili waanze kampeni taratibu kwa wananchi. Sisi tunasema hapana, hizi pesa chafu hatuzitaki kabisa na hazituletei maendeleo katika Tarafa ya Nyanja. Tunafahamu anazo pesa nyingi sana na anaweza kufanya chochote ili aendelee.
Mh. Rais, sisi wananchi, na hasa kupitia wazee wetu ambao hawana uwezo wa kujieleza hasa kwa Kiswahili, wameshindwa kuelewa uongozi wa huyu Mbunge tajiri Mkono. Kwani yeye ni Butiama tu na sehemu zake, hasa upande wa kwao, ndizo anazoendeleza na kutafuta wafadhili. Sisi hatutaki Mbunge tajiri tena mfanya biashara, kwa sababu hawa ndiyo chanzo cha kuwepo na vurugu, rushwa, na pia hawatusaidii. Tunadhani, kutoka na kauli yako, ulisema wabunge wafanya biashara ndiyo mwisho wao wa kugombea ubunge, kwani wanaharibu sifa ya nchi yetu Tanzania. Wanatumia pesa zao chafu kutuharibia nchi na amani na utulivu tulio nao. Tunawaomba, kama ikiwezekana, tume ya kudhibiti rushwa itumwe huku kwetu kutadhimini hali ya uchaguzi wa mwakani 2010. Pesa chafu zinanza kutembezwa. Tunafahamu Mkono ni mjumbe wa NEC, ila hasitumie ubavu wake ili kwamba kwenye kura za maoni apitishe. Wajita, tumechoka kununuliwa kwa pesa. Mh. Rais, tunahitaji maendeleo yanayoonekana na pia serikali iwe wazi inapotoa fedha, hasa kwenye tarafa yetu.
Kilio chetu tumekuwa nacho zaidi ya miaka 10, na hakuna ufumbuzi wa matatizo yetu. Inawezekana tunaletewa reporti yenye kupotosha. Kwa hiyo, sisi wananchi, kupitia wazee wetu, tumeona leo tuchukue jukumu la kukuletea wewe, Mh. Rais, ili jambo kabla ya mwaka kuisha, kwa kupitia vyombo vya habari. Tumemchoka Mbunge wetu kabisa, japokuwa anadai ya kuwa hakuna wa kumwondoa mpaka atakapoachia madaraka. Pesa anadai anayo, na viongozi hakuna wa kumtoa, hata wewe, Rais. Tukimpigia simu kutoa shida, anatujibu vibaya. Kiongozi gani asiye tujali sisi tuliomweka madarakani?
Mh. Rais, uchaguzi umekaribia sana. Tunafahamu sana utashinda tena kupitia tiketi ya CCM, na tutakupatia kura zote. Ila Mbunge wetu, hapana, tunaomba utupatie jina ili kwamba sisi wananchi tumchague. Tumechoka kununuliwa kwa pesa chafu ambazo hatujui zimetoka wapi. Sasa, Mh. Rais, tumeamka, na macho yetu yameona mbali. Tunasema, rushwa haina mahali pake tena. Sisi Tarafa ya Nyanja tunaomba wananchi wenzetu walio na matatizo kama yetu, hasa wa Vijijini, tusinunuliwe kwa rushwa ya baiskeli, kwani inatulemaza kabisa.
Rais, tunakuomba haya matatizo utupatie ufumbuzi wa kina hasa katika Tarafa yetu ya Nyanja, na pia tunakuomba, kabla ya kuanza kampeni, uje Tarafa ya Nyanja, na kama siyo wewe basi Waziri Mkuu.
Tunakutakia Heri ya Mwaka Mpya 2010.
Wananchi Tarafa ya Nyanja, Majita, Musoma Vijijini.