Barua Maalum kwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dr Shein: Usikubali damu za wananchi wako wa Zanzibar zimwagwe sababu ya dhulma

Barua Maalum kwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dr Shein: Usikubali damu za wananchi wako wa Zanzibar zimwagwe sababu ya dhulma

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Mheshimiwa Dkt. Shein:

Nakusalimia kwa salamu ya Amani, Amani ya ALLAH iwe nawe

Barua hii ni kutoka kwa mwananchi na naanza kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma.

Usikubali damu ya Wazanzibari imwagike chini ya uangalizi wako. Unafahamu vizuri historia ya nchi yako, harakati za watu wako, Kiu yao ya muda mrefu ya kisiasa. kiuchumi na kijamii na subira waliyofanya kwa muda wote huu hata wewe ukawa rais kwa vipindi viwili. Basi kwa heshima waliyokupa na wewe kwa kutambua hili kabla hujastaafu watendee wema wananchi wako, walipe haki badala ya dhulma, walipe amani badala ya kumwaga damu zao.

Ndugu rais Shein wewe ni muislamu na Allah amesema kwenye Qur'an yafuatayo

1. Amekataza kumwaga damu isiyo na hsatia
2. Aliwakataza wana wa Israel kumwaga damu ya mtu yeyote asiye na hatia maana kufanya hivyo ni sawa na kuua watu wa dunia nzima, na kuponya mtu mmoja ni sawa na kuponya dunia nzima

Ndugu rais Shein kwa kuwa wewe ni muislamu, basi zingatia hizo aya juu kisha amua mwenyewe kama unataka kuruhusu dhulma ifanyike kwa watu wako au la

Lakini Ndugu Rais Shein, wakati unaapishwa kwa ajili ya urais, uliapishwa wewe huku umeshika Qur'an tukufu na ukaahidi mbele ya ALLAH mtukufu kuwa utatenda haki, hutoonea wala kubagua yeyote basi nakutaka utimize kiapo chako kwa kuwapa wazanzibar haki kwenye uchaguzi.

Ndugu Rais Shein, wewe ni mlinzi mkuu wa Maslahi ya wazanzibar ndani ya muungano, Uchaguzi mkuu wa ubunge na urais wa Jamhuri ya Muungano unalenga kulinda maslahi ya watu wako ndani ya huu muungano. Nakusihi kwa unyenyekevu mkubwa SIMAMA KIDETE KUZUIA DHULMA DHIDI YA WATU WAKO. Ndugu raisi Shein, hakuna kazi kubwa ya heshima kwako kama kulinda na kutetea maslahi na haki za watu wako.

Ndugu Rais, NEC ni chombo cha Muungano, lakini wewe ndiye rais wa Zanzibar, hakiwezi kufanya kazi hata huko Zanzibar bila ridhaa yako, Basi Zuia nia ovu ya baadhi ya watendaji wa chombo hiki kuwanyima haki wananchi wako.

Ndugu Shein, wape Wananchi wako nafasi ya kumchagua rais wa Zanzibar na wawakilishi kwa haki kabisa, Usikubali kuruhusu udhalimu ufanyike chini ya uangalizi wako.

Ndugu rais Shein, Mtume Muhammad alisema. "Ukiuona uovu unatendeka, uondoe kwa mkono wako, ukishindwa kemea na kama kukemea huwezi basi chukia, ila kuchukia peke yake bia kufanya jambo ni udhaifu wa imani". Nakusihi ndugu rais Shein Wasaidie watu wako kuwakinga dhidi ya dhulma hii ya kunyimwa haki ya kuchagua wamtakaye.

Ndugu rais Shein napenda tu kukufahamisha, Dhulma hii inayoonekana kusukwa, haisukwi kwa maslahi ya kulinda muungano, haisukwi kwa maslahi ya ustawi wa Zanzibar, bali ukiangalia kwa jicho la mbali inasukwa kwa ajili ya ambition ya kisiasa ya mtu mmoja tu ambaye naye aliapa kulinda katiba na kutenda haki vitu ambavyo havifanyi kwa mujibu wa kiapo chake na sasa kwa kuwa Zanzibar ni kikwazo katika azma yake hiyo basi anataka kuwatumia wazanzibar kama ngazi ya kufikia malengo yake. Anahitaji kura za wabunge wa Zanzibar kwenye mabaraza ya kutunga sheria ili afanikishe azma yake ovu anayoifikiria kwa hiyo ndo maana anataka kuwachagulia Zanzibar wajumbe kwenye mabaraza hayo.

Mwisho nimalizie kwa kukuasa na kuwaasa watendaji wote wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, Mtume Muhammad alisema.

"Muumini wa kweli ni yule ambaye waumini wenzie wamenusurika dhidi ya (shari za) mikono yao. Basi walindeni Wazanzibari wenzenu, Usikubali mtu kuumiza wenzenu.

Staafu huku umewatendea wema watu wako!

Ndugu rais Shein,
Ujumbe nimeufikisha kwako, ALLAH na Malaika wake wote Jibril (Gabriel) , Mikail(Michael), Israefeel, Israeel, na wengineo pamoja na Masihi(Yesu Kristo) wa ALLAH na wanadamu washuhudie kuwa ujumbe huu nimeufikisha kwako.
 
Kwa mtu mwenye hofu ya Mungu hawezi kubali kuingia ikulu kwa kumwaga damu za watu wasio na hatia tena walio kuwa wanadai haki yao ya kikatiba. Mwinyi kazi kwako
 
Mungu wetu na ashukuriwe.
Tatizo kubwa nimebaini wanasiasa wana mungu wao na Si huyu wa Vitabu vi takatifu. Ila kule huenda kujitakasa
 
Walionuia kumwaga damu ni wapemba (wafuasi wa ACT)...kwa hiyo uamuzi wanao wao wenyewe

Wakitimiza adhama yao ya kumwaga damu na kweli itamwagika
 
Shein wa watu wamwache kabisa

Wanalianzisha wenyewe na watalinywa wenyewe
 
Kwa mtu mwenye hofu ya Mungu hawezi kubali kuingia ikulu kwa kumwaga damu za watu wasio na hatia tena walio kuwa wanadai haki yao ya kikatiba. Mwinyi kazi kwako

Kwa kweli ni aibu kubwa sana wale walioapa kutawala kwa kutenda haki huku wameshika vitabu vitakatifu wanapokuwa wa kwanza kuvunja viapo vyao.
 
Shein mnamuonea bureee.....
Mauchafu na maovu yote ya kuiharibu Zanzibar yanaratibiwa kutoka chamwino
 
Ni rais wa Zanzibar, akisema No, Chamwino itarudi nyuma lakini naye akiwa mlegevu akakubali udhalimu, dhima iko kwake!
Ni kweli lkn hao wamekula viapo vya damu km majambazi wanavoapa kutotajana pindi mmoja wapo akikamatwa.....
Yani hapo damu itamwagika tuu....
 
Back
Top Bottom