Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu
Bandiko la binti ndo kama hilo
==================================================================
UMOJA WA WANAUME BAHILI TANZANIA UWABATA
S.L.P 444
Dar es Salaam, Tanzania
YAH: PONGEZI KWA USHUJAA WAKO LILIPOKUJA SUALA LA KULIPA KODI
Ndugu Diamond,
Kupitia kiti changu cha uenyekiti wa Baraza la Wanaume Bahili Tanzania (BWBATA), napenda kukupa pongezi za dhati kwa kuwa mfano bora wa kuigwa na wanaume wote wenye akili timamu.
Tumesikia kwa furaha kubwa jinsi ulivyokuwa na msimamo thabiti wa kujua thamani ya pesa hadi ikafikia hatua ya ‘kuchenga chenga’ kodi.
Huo ndio uanaume halisi – kujua kipi ni cha muhimu na kipi ni cha kupita.
Ndugu Diamond, kitendo chako kimeleta mwanga kwa vijana wengi ambao kwa sasa wanateseka kwa kuendekeza ‘michepuko’ huku wakijitwika majukumu yasiyowahusu.
Ulivyoamua kuweka mbele maslahi yako binafsi, umetufundisha kuwa sio kila aliye na hela anatakiwa kuzitumia kama maji ya kisima. .
Tunawahimiza vijana wengine kuiga mfano wako na kuacha tabia ya kuishi kwa kujitwika mizigo.
Wanaume wanatakiwa kujua kuwa kodi si dhambi kutolipa kama haijaandikwa kwenye jina lako.
Tunaendelea kukuombea uendelee kuwa imara kwenye msimamo wako na uendelee kutupa sababu ya kujivunia kuwa bahili.
Mungu akutangulie kwenye harakati zako za kibahili, na tunaamini siku moja utastahili tuzo ya ‘Bahili Bora wa Mwaka.’
Kwa heshima na taadhima,
Bakari Mchungahela,
Mwenyekiti,
Umoja wa Wanaume Bahili Tanzania (BWBATA).