Habari zilizopo ni kwamba hili sakata la Malima vs Spika lilikuwa linaelekea pabaya.
Kulikuwa na juhudi za chinichini zinazoongozwa na EL pamoja na RA na kundi lao za kutaka ku-empeach spika.The only problem is that,they needed 2/3 of the votes to proceed.On the contrary,zinahitajika signatures 65 tu za wabunge kum-empeach PM!
Mzee 6 na timu yake,ambayo walikuwemo almost wabunge wote wa upinzani(numbering 45 or so),na wengi wa CCM ambao hawana imani na PM,waliweza kukusanya hizo signatures na kuwa nazo tayari.
Then information was leaked delibarately to PM kuwa taa inakaribia kuzimika.Ikabidi yeye na timu yake ikiongozwa na RA watafute suluhu ya haraka sana na Spika.Matokeo yake ni wao na Malima kusalimu amri na kunyanyua kitambaa cheupe!
Kwenye Daily News leo kuna picha,ukurasa wa pili ikionyesha PM,Spika na Malima wakiwa pamoja wakicheka saana.
Inasemekana,baada ya kikao,Spika akitoka ukumbini,Malima akiwa na PM alimfuata Spika na kumkumbatia,huku akimuacha spika akishangaa,and the picture in the Daily News was taken moments after that.Hio yote ilikuwa ni PR stunt
Malima alikuwa amepangiwa ajali kubwa sana,na kwa waliotazama taarifa ya habari jana,watakumbuka kumuona Halima Mdee akisoma taarifa ndefu iliyokuwa ina lengo la kummaliza kabisa Malima.Inasemekana,yale aliyoyasoma Mdee yalitoka kwa Spika.
Kilichonimaliza mimi hapa ni jinsi EL na timu yake walivyom-underrate Spika,and how could they?
Slogan ya 'Kizazi Kipya,Nguvu Mpya,Kasi Mpya" ilitoka kwa Sitta,leo wanamuona chizi! Huyu ndio ilikuwa awe PM,lakini jamaa wakamuwahi na form za uspika na kumuahidi kuwa mkewe atapewa uwaziri!
Ile kauli ya kuwa huo mjadala kaumaliza,ilikuwa ni jeuri,na hakuna mtu atapinga,because theres a lot of stake in it.
Hii nchi yetu mimi naona sasa imekuwa ni kama soap opera.Drama ni kila siku.What amazes me about sisi watanzania,ni kuwa tunampa mtu mda mrefu sana kabla ya kugundua kuwa hatufai.Enzi za Sumaye,alichukiwa kiasi cha kwamba mpaka alikuwa anasakiziwa mambo ya ajabu,mara kanunua shamba Kibaha and so forth,lakini it seems huyu PM wa sasa bado hajawaingiwa watu kwenye damu,maana issue kama ya Richmond(dubbed Richmonduli),ni kimya sasa,ukifananisha na jinsi Sumaye alivyovaliwa bango na shamba lake la Kibaha!! Kuna siku labda watanzania wataona kuwa kweli labda EL ni bomu and all this Richmonduli business will start making some sense! Its high time the Prez made the re-shuffle we have all been anticipating for sometime