SI KWELI Barua ya CHADEMA ikionesha mikakati yao siku ya maandamano

SI KWELI Barua ya CHADEMA ikionesha mikakati yao siku ya maandamano

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Barua hii ikionesha Mpando wa CHADEMA kundamana ni ya kweli?

BARUA YA CHADEMA SI KWELI.jpg

 
Tunachokijua
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama cha kisiasa nchini Tanzania ambacho kulianza mwaka 2010 kuwa chama kikuu cha upinzani.

Kilianzishwa tarehe 28 Mei 1992 na mwanasiasa mkongwe Edwin Mtei, aliyewahi kuwa waziri wa fedha katika miaka 1977 hadi 1979.

Mnamo Septemba 11 2024 CHADEMA kilifanya mkutano katika ofisi zao zilizopo Mikocheni Dar Es Salaam, kufuatia kutekwa na kuuawa kwa baadhi ya watu hasa tukio la kutekwa na kuuawa kwa aliyekuwa Kiongozi wa CHADEMA Ali Kibao.

Miongoni mwa yaliyozungumzwa kwenye kikao hicho ni pamoja na maazimio ya kufanya mandamano ili kushinikiza hatua za uwajibikaji na kurejeshwa kwa waliopotea ambapo CHADEMA ilitangaza kufanya maandamano Septemba 23 2024

Mara baada ya kutangazwa maandamano hayo imeonekana barua ikisambaa mitandaoni (Tazama hapa, hapa, hapa, hapa, hapa, hapa na hapa) inayodaiwa kuwa ni ya CHADEMA ikitoa maelekezo ya namna ya kufanyika maandamano huku ikidai kutatolewa mafunzo maalumu kwa waandamaji ambapo walimu wa kufundisha mafunzo hayo watatoka Kenya.

Je, Ukweli ni upi?
JamiiCheck imefanya uhakiki kwa kukagua kwenye vyanzo vyote vya taarifa vya CHADEMA na kukuta hakuna barua kama hiyo au yenye ujumbe kama huo.

Aidha, tumebaini kuwa barua hii si halisi, haijatolewa na CHADEMA bali imetengenezwa na kutolewa na watu wenye nia ya kupotosha kwasababu barua inadai Viongozi wa BAVICHA na Red Brigedi watapatiwa mafunzo kwenye shamba la chama hali ya kuwa Red Brigedi ilifutwa mwaka 2019 kwenye marekebisho sheria ya vyama vya siasa, Sura namba 258 iliyofanyiwa Marejeo mwaka 2019 chini ya kifungu cha 8E (1)

1726574989687-png.3098662
Pia, JamiiCheck imebaini makosa kadhaa kwenye barua hiyo inayosambazwa ambayo yanathibitisha kuwa barua hiyo haijatolewa na CHADEMA.

Makosa yaliyo kwenye barua hiyo
1. Haina tarehe
2. Haina saini
3. Barua haina letterhead ya CHADEMA
4. Red brigedi haipo kwa sasa ilifutwa imefutwa kwenye Marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa ya Mwaka 2019(Haipo kwa sasa)
5. Kichwa cha barua za CHADEMA huwa hakipigiwi mstari hii ni kufuatia mlinganisho wa barua nyingi zilizotolewa na CHADEMA
6. Fonts zake ni tofauti na zile zinazotumiwa na CHADEMA
7. Ina makosa mengi ya kiuandishi, Mfano Atutegemei badala ya hatutegemei

Aidha Kwa mujibu wa Chanzo chetu cha kuaminika ndani ya CHADEMA kimethibisha kuwa barua hii si yao.
Back
Top Bottom